Tafuta

Monsinyo Diego Giovanni Ravelli ameteuliwa na Papa Francisko kuwa Mshereheshaji mkuu wa Liturujia za Kipapa. Monsinyo Diego Giovanni Ravelli ameteuliwa na Papa Francisko kuwa Mshereheshaji mkuu wa Liturujia za Kipapa. 

Monsinyo Diego Giovanni Ravelli Mshereheshaji Mkuu wa Liturujia

Monsinyo Diego Giovanni Ravelli alizaliwa tarehe Mosi Novemba 1965 huko Lazzate, Italia. Kunako mwaka 1991 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Mwaka 1998 aliteuliwa kuwa Afisa mwandamizi, Idara ya Mtunza sadaka ya Kipapa. Baadaye alijiendeleza na kujipatia Shahada ya uzamili katika Mbinu za Ufundishaji kutoka Chuo Kikuu cha Kipapa cha Wasalesian, Roma! Yaani!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko hivi karibuni amemteuwa Monsinyo Diego Giovanni Ravelli kuwa Mshereheshaji mkuu wa Liturujia za Kipapa na Mratibu mkuu wa Kwaya ya Kipapa (Cappella Musicale Pontificia). Monsinyo Diego Giovanni Ravelli anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Monsinyo Guido Marini (56) aliyeteuliwa na kuwekwa wakfu kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Tortona, nchini Italia. Monsinyo Diego Giovanni Ravelli alizaliwa tarehe Mosi Novemba 1965 huko Lazzate nchini Italia. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, mwaka 1991 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre na kuhamia Jimbo Katoliki la Velletri-Segni. Mwaka 1998 aliteuliwa kuwa Afisa mwandamizi, Idara ya Mtunza sadaka ya Kipapa.

Baadaye alijiendeleza zaidi katika masomo na hatimaye, kujipatia Shahada ya uzamili katika Mbinu za Ufundishaji kutoka Chuo Kikuu cha Kipapa cha Wasalesian, Roma. Waswahili wanasema, elimu haina mwisho, Monsinyo Diego Giovanni Ravelli alijiendeleza zaidi katika Liturujia ya Kanisa na hatimaye kujipatia Shahada ya Uzamivu kutoka Taasisi ya Kipapa ya Liturujia katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Anselmi kilichoko mjini Roma. Tarehe 25 Februari 2006 akateuliwa na Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI kuwa Mshereheshaji Mkuu wa Liturujia za Kipapa. Tarehe 12 Oktoba 2013 akateuliwa kuwa Afisa Mwandamizi Idara ya Mtunza sadaka ya Kipapa. Tarehe 11 Oktoba 2021, Baba Mtakatifu Francisko akamteuwa kuwa Mshereheshaji mkuu wa Liturujia za Kipapa na Mratibu mkuu wa Kwaya ya Kipapa (Cappella Musicale Pontificia).

Liturujia za Kipapa

 

24 October 2021, 08:10