Tafuta

Ratiba ya Misa za Papa kwa mwezi Novemba Ratiba ya Misa za Papa kwa mwezi Novemba 

Maadhimisho ya Liturujia za Papa mwezi Novemba

Ratiba ya matukio ya Papa kwa mwezi Novemba ambayo miongoni mwake ni Misa ya Siku ya Maskini ulimwenguni aliyoanzishwa mnamo 2016 wakati wa kuhitimisha Jubilei ya Huruma.

Na Sr. Angella. Rwezaula- Vatican.

Kwa mujibu wa ratiba ya Maadhimisho ya Kiliturujia ya Kipapa iliyowakilishwa kwenye vyombo vya habari katika ukumbi wa Makao makuu kuna mambo makuu katika mwezi Novemba. Katika siku ya kukumbuka Marehemu wote, mnamo tarehe 4 Novemba 2021,  saa 5.00 asubuhi , Papa Francisko anatarajia kuongoza misa kwa ajili ya makardinali na maaskofu walioaga dunia ndani ya mwaka huu, katika Altare ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro.

Siku itakayofuata tarehe 5 Novemba, Baba Mtakatifu atakwenda kwenye makao makuu ya Chuo Kikuu Katoliki cha Moyo Mtakatifu, Roma kwa maadhimisho ya misa Takatifu, saa 4.30 asubuhi katika fursa ya maadhimisho ya miaka 70 tangu kuzinduliwa kwa Kitivo cha Madawa na Upasuaji. Tarehe 14 Novemba katika Dominika ya  XXXIII  ya Kipindi cha Mwaka, Papa Francisko anatarajia kuongoza Misa katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, saa 4.00 asubuhi katika fursa ya Siku ya V ya Maskini duniani.

Katika ujumbe wake uliochapishwa mnamo mwezi Juni, mwaka huu Papa alikuwa ameandika kuwa “Ni matarajio yangu kuwa siku ya maskini duniani ambayo imefikia toleo la tano, inaweza kuenezwa daima katika makanisa yetu mahalia na kujifungulia katika harakati za uinjilishaji ambao unakutana awali ya yote maskini mahali popote walipo. Hatuwezi kusubiri, kwamba wabishe hodi milangoni mwetu kwani ni dharura ambayo iweze kuwafikia katika nyumba zao, katika mahospitali na katika nyumba za kutunza wazee, njiani na katika maeneo ya giza ambayo wakati mwingine wanajificha, kwenye vituo vya kimbilio na vya makaribisho.

Ujumbe wa Papa Francisko kwa siku hiyo ya Maskini duniani 2021, unaongozwa na kauli mbiu “Maana siku zote mnao maskini pamoja nanyi” Mk 14:7.  Huo ni mwito kwa waamini wote na wenye mapenzi mema , kumtazama Kristo katika maneno yake na matendo yake kupitia maskini na kumkumbatia maskini kwa kumsikiliza kilio na kujibu kilio hicho.

23 October 2021, 16:53