Tafuta

MKUTANO WA COP26 HUKO SCOTLAND KUHUSU MABADILIKO YA TABIANCHI. MKUTANO WA COP26 HUKO SCOTLAND KUHUSU MABADILIKO YA TABIANCHI. 

Kutoka Vatican kwenda Glasgow atashiriki Kardinali Parolin

Kwa mujibu wa Msemaji wa vyombo vya habari Vatican,ametoa taarifa kuwa atakuwa Katibu wa Vatican atakaye kwenda Scotland kwenye Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya tabianchi (COP26) unatakaofunguliwa kuanzia 31 Oktoba hadi 12 Novemba 2021.

Vatican News.

Kwa mujibu wa Msemaji wa Vyombo vya Habari Vatican kwa waandishi wa habari Dk. Matteo Bruni: amesema: “kwa kujibu maswali ya waandishi wa habari kuhusiana na ushiriki wa Vaticana katika kikao cha Mkutano wa Vyama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa juu ya Mabadiliko ya Tabianchi (COP26), unaotarajia kuanza tarehe 31 Oktoba hadi 12 Novemba, ninaweza kuthibitisha kuwa Ujumbe huo utasindikizwa na Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican wa Baba Mtakatifu”.

Wiki iliyopita, vijana wapatao 400 waliunganika huko Milano ili kujadili utetezi wa mazingira katika mtazamo wa Mkutano ujao huko Glasgow nchini Scoltland. Na wakati huo huo, Vijana wa “Youth4Climate: Driving Ambition”, Jamatatu iliyopitia wakati wa Mkutano jijini Vatican wa Imani na Sayansi, Papa alitoa wito wake kwa wahusika wa COP26 akiwaomba majibu ya kutosha mbele ya mgogoro wa Ikolojia.

Ni mada hata hivyo ambayo ilichukuliwa tena katika Hati ya Pamoja ambayo Papa Francisko, Patriaki wa Kiekumene Bartolomeo I na Mkuu wa Kanisa la Kianglikani Justin Welby walitia saini.  Ni matashi mema kwamba nikitumaini kuwa muunganiko wa kimataifa juu ya mada za ulinzi wa kazi ya uumbaji na mazingira pia ni pamoja na kusikiliza kilio cha maskini.

08 October 2021, 15:52