Tafuta

Al-Tayyeb:Wote ni ndugu ni waraka muhimu hata kwa waislamu

Dk.Tornielli,Mhariri Mkuu wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano akihojiana na Imam Mkuu wa Al-Azhar akiwa studio za Vatican News amezungumza juu ya uhusiano na Papa Francisko, kuwa "angu dakika ya kwanza ya kukutana naye ilinipa uthibitisho kuwa yeye ni mtu wa amani na ubinadamu.Waraka wa Wote ni ndugu ni wito wa kuunda udugu wa kweli mahali ambapo hakuna nafasi ya ubaguzi katika misingi ya tofauti ya dini,rangi,jinsia au aina nyingine za kutovumiliana.lama

Na Andrea Tornielli

Kila mmoja wetu aligundua uwelewano wa kiroho na kimawazo mbele ya migogoro unaosumbua binadamu wa sasa” ... Ahmad Muhammad Al-Ṭayyeb, Imam Mkuu wa Al-Azhar, katika siku hizi akiwa Roma ameshiriki baadhi ya matukio muhimu akiwa karibu na Papa Francisko na viongozi wengine wa kidini, ambapo ametembelea studio za Radio Vatican- Vatican News na kujibu baadhi ya maswali kuhusu uhusiano na Baba Mtakatifu baada ya mwaka mmoja wa uchapishwaji wa Waraka wa ‘Fratelli tutti’. Yafuatayo ni mahojiano hayo yaliyo fanyika kati ya Dk. Andrea Tornielli, Mhariri Mkuu wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano.

Awali ya yote unaweza kusimulia ulivyoanza na kuendelezwa urafiki wa Papa Francisko? Ni nini maana yake urafiki huo kwako?

Awali ya yote asili yake inaweza kupatikana katika mwanzo wa uhusiano wa Kiislamu na Kikriso, wakati Nabii Mohamedi alipowatuma wanafunzi wake huko Abyssinia, ambapo kulikuwa akitawala  mfalme wa Kikristo Negus, waliodhulumiwa na maskini na wafuasi ambao waliteswa vibaya na wapagani huko Makka. Mfalme huyo aliwakaribisha Waislamu, akawapa kimbilio na ulinzi, na walirudi kwenye Peninsula ya Arabia mara tu baada ya jamii ya Waislamu kupata nguvu. Kwa hivyo ilikuwa ngumu, au isingewezekana kwao kuteswa au kuacha dini yao. Uhusiano huo kati ya wakristo na Waisla ulindelea kwa karne kumi na heka heka, lakini pia katika nyakati za giza, kama vita na migogoro ya kisilaha, kulikuwa na mazungumzo. Falsafa ya kipindi cha zamani ya kati kimajaa urthi huo. Katika enzi ya sasa aumenzishwa huko Al-Azhar tume kwa ajili ya mazungumzo na Vatican na ambayo inaendelea kuunganika pamoja hapa jijini Vatican na mwaka mwingine huko Al-Azhar.  Shughuli ya tume hiyo ilikatizwa kwa kipindi cha miaka sita au saba hivi hadi ilipoanza tena kwa upya baada ya uchaguzi wa Mpendwa Papa Francisko. Huko Al-Azhar katika mpango huo ulimpongezwa na mimi pia tulianza kupata jibu zuri kutoka kwa Papa. Jibu ambalo linatutia moyo wa kuanza uhusiano huo mpya. Na kwa namna hiyo niliamua kumtembelea Papa mjini Vatican mnamo Mei 2016.

Katika ziara hiyo kila mmoja wetu aliweza kugundua maelewano makubwa ya kiroho na wazo mbele ya migogoro ambayo inasumbua ubinadamu wa sasa kwa namna ya pekee kwa maskini, yatima, wagonjwa, wajane, waathiriwa wa vita na wasio na makazi maalumu. Maelewano haya kati yetu na yeye yameweza kutoa jambo muhimu zuri kwa ajili ya kutoa faraja katika mgogoro huo. Na tangu wakati huo hapajawa na kikwazo chochote. Binafsi, sijasita kunyoosha mkono wangu. Kuanzia dakika ya kwanza kabisa ya mkutano wetu na yeye, nilikuwa na uthibitisho kwamba yeye ni mtu wa amani na ubinadamu ulio ubora. Mambo yalikwenda vizuri na katika miaka mitatu tu tulikuwa na mikutano sita. Katika mkutano wa tano kati ya hizi tulisaini Hati juu ya Udugu wa Binadamu. Maelezo juu ya mada hii yanaweza kupatikana katika kitabu cha “The Imam, the Pope”, yaani “Imam na Papa” na mchakato wa njia yenye miiba, ambayo imetafsiriwa hivi karibuni kwa lgha ya Kiitaliano, iliyoandikwa na mwanafunzi wangu na mtoto wangu hakimu Mohammad Abdelsalam.

Kwa nini ulitaka kushiriki binafsi katika njia hii isiyokuwa ya kawaida?

Shukrani kwa mafunzo yangu huko Al-Azhar na pia shukrani kwa kuwa nimekulia katika mji wa kitalii wa Luxor, tangu utoto nilijua kupitia uvumbuzi wa akiolojia wa mafarao ambao dini zinachanganywa na sayansi na ustaarabu kwa njia ya kushangaza. Kwa maana hiyo nilikua na imani, ambayo hadi leo hii inaingia kwenye mishipa yangu, ya umuhimu mkubwa wa dini katika kujenga ustaarabu na maendeleo ya mali na kiroho. Na pia jukumu ladini katika kulinda mafanikio haya ya ustaarabu, ili yasibadilike na hivyo kuwa mabaya kwa mwanadamu, na sio kwa mwanadamu tu bali pia kwa wanyama, mimea na hata mawe. Baadaye iulendelea kukua ufahamu kamili wa umuhimu wa dini ndani yangu na masomo yangu ya sayansi ya Kiislamu na utaalam katika kitivo cha taalimungu huko Al-Azhar. Niligundua kuwa ujumbe wa dini unaweza kuzaa matunda yanayotarajiwa ikiwa tu yatatangazwa na wamini waaminifu, kwanza wamepatanisha kati yao. Kati ya wale wanaoleta ujumbe huu kwa watu lazima kuwe na amani, maelewano na ushirikiano. Kwa sababu ikiwa mgawanyiko na mzozo unatawala kati yao, hawawezi kufikisha ujumbe wa amani kwa watu.

Tunajua methali maarufu isemayo: Yeyote ambaye hana kitu, hawezi kutoa chochote. Hii ndio sababu nilifikiri kwamba Al-Azhar inapaswa kuchukua hatua ya kuwasiliana na wawakilishi wa dini ili kwanza kufikia maridhiano kati yao na baadaye kwenda ulimwenguni kutangaza ujumbe wa amani. Nilielewa kuwa dini za tauhidi ambazo zimeonekana katika historia zote zina chanzo kimoja tu, Mungu, Mtukufu, Aliye Juu. Tunayo maandishi wazi katika Quran Tukufu ambayo yanasema kwamba kile kilichofunuliwa na Mungu kwa Muhammad ni sawa na kile ambacho kilifunuliwa kwa Ibrahimu na Musa na Yesu. Kuna chanzo kimoja. Yote ni muhimu kwa ubinadamu kama vile maadili, mafundisho na amri, ambazo sio tofauti kati ya dini moja na nyingine. Hii ndio iliniongoza kuanzia na kujiweka karibu na ndugu zangu na wenzangu wanaowakilisha dini, ili kugundua mambo haya ya pamoja, na ashukuriwe Mungu tumepatanishwa na watu, tukitumaini kuwa hii itasaidia kupunguza maumivu ya mtu wa leo.

Mahojiano na Imam wa Al- Azhar Ahmad Al-Tayyeb
Mahojiano na Imam wa Al- Azhar Ahmad Al-Tayyeb

Je! Ni mchango gani wa waraka wa ‘Wote ni ndugu’ wa Baba Mtakatifu Francisko ambao unaona kuwa ni muhimu zaidi? Je! Huu ni ujumbe ambao pia unapendeza kwa Waislamu?

Waraka huu ni muhimu sana, hasa wakati huu, kwa Waislamu na wasio Waislamu. Ninaweza kusema kwamba waraka huu unafaa katika mfumo wa mikutano yetu na umeongozwa na wao. Papa mwenyewe anaitaja, naamini katika dibaji. Waraka huo  una kwenda  katika mwelekeo huo huo, ule wa mazungumzo na kuishi kati ya watu: kwa kifupi, ni wito wa  kutumia kanuni za maadili za dini ili kuunda undugu wa kweli ambapo hakuna nafasi ya ubaguzi kwa msingi wa tofauti ya dini, imani, rangi, jinsia, au aina zingine za kutovumiliana. Waraka huu ni muhimu kwa Waislamu na wakati huo huo kwa wengine, kwa sababuuinasema kwamba sisi sote ni ndugu. Na Korani inawaambia Waislamu: mna ndugu na ninyi ni sawa katika ubinadamu. Sisi tunasema kwamba mtu huyo ni sawa au ni sawa na mimi na ni ndugu  yangu katika ubinadamu. Anaweza kuwa ndugu wa dini, lakini pia anaweza kuwa ndugu wa ubinadamu kwangu. Hiki ndicho kitovu cha ‘Fratelli tutti’ yaani ‘Wote ni ndugu’.

Viongozi  na  Imam wa Al- Azhar Ahmad Al-Tayyeb
Viongozi na Imam wa Al- Azhar Ahmad Al-Tayyeb
08 October 2021, 15:51