Tafuta

Kampeni dhidi ya biashara mbaya ya ya binadamu na utumwa inayoendeshwa na Chama cha Talitha Kum Kampeni dhidi ya biashara mbaya ya ya binadamu na utumwa inayoendeshwa na Chama cha Talitha Kum 

Biashara ya binadamu:vijana wanaweza kuwa mstari wa mbele kupambana nayo!

Ili kumaliza balaa la biashara mbaya ya watu inahitaji mafunzo kwa kizazi kipya.Haya yamezunguzwa katika katika mkutano Roma uliondaliwa na Umoja wa Wakuu wa mashirika kimataifa.Sr Bottan anasema vijana ndio walio wa kwanza kuathirika na biashara hiyo na utumwa lakini pia ni muhimu kwa rasilimali ya kupambana dhidi yake kwa sababu wana uwezo wa kiteknolojia.

Na Sr. Angella Rwezaula - Vatican

Biashara ya binadamu ni mgogoro wa ulimwengu mbele ya mateso yasiyoelezeka, ambayo yanawatazama watu milioni 25 ulimwenguni kote, na asilimia 70 ya hao ni wanawake na wasichana na robo tatu yao ni watoto. Hii ni dhararu kwa hadhi na utu wa kibinadamu na kuna wajibu wa kuwa na maadili na sio tu kupambana, lakini pia kuelimisha kizazi kijacho katika vita dhidi ya usafirishaji haramu ya binadamu. Huu ni mpango  mpya sasa wa kazi ya ujasiri ya watawa wanaohusika katika mapambano dhidi ya utumwa mambo leo,  mashujaa mashuhuri wa kimataifa, ambao wameanzisha tena kujitoa kwao wakati wa mkutano wao wa hivi karibuni uliongozwa na kauli mbiu: “Kuwawezesha Kizazi Kipya ili Kupambana na Utumwa wa Kisasa”, ulioandaliwa na Umoja wa Kimataifa wa Wakuu wa Wakuu, UISG, kwa kushirikiana na Ubalozi wa Marekani na Ubalozi wa Ireland, wanaowakilisha nchi zao Vatican.

Ni mpango ambao umeona mazungumzo ambayo yalizingatia njia za kuhamasisha kizazi kipya ili kupambana na janga la usafirishaji haramu wa binadamu ambapo Sr. Imelda Poole,  anayejikita nchini Albania na utume huo  dhidi ya biashara ya binadamu na Rais wa Renate, yaani Mtandao wa Ulaya wa Watawa wanaojikita katika mapambano dhidi ya biashara ya watu  na wakati hauo huo unyonyaji wa binadamu, suor Gabriella Bottani, Mratibu wa Kimataifa wa Talitha Kum, Mtandao wa mashirika ya Maisha ya Kitawa ambao wanajikita dhidi ya biashara  ya binadamu, Blessing Okaedion, mwathirika wa zamani na  ambaye leo hii ni mpatanishi wa kiutamaduni, mwanzilishi na rais wa Shirika lilisilo la Kiserikali (Weavers of Hope) na Sr. Monica Chikwe, makamu rais  wa Chama cha ‘ Slave No More’ kilichoanzishwa na Sr. Eugenia Bonetti, walifungua nafasi mpya za kuingilia kati katika hotuba zao ili kuwezesha kizazi kipya kiweze kupambana na utumwa mambo leo, kiasi cha kuwafanya vijana  hao kuwa viongozi wa harakati ya kupambana dhidi ya  usafirishaji haramu wa binadamu, shukrani pia kwa uwezo mkubwa wa kiteknolojia walionao vijana wengi.

Wote tunalo jukumu mbele ya kizazi hiki cha kesho ambacho kinahitaji kusikiliza vijana kwa ajili ya baadaye kuwasindikiza na kuwasaidia katika matendo yao. Vijana wanapaswa wajumuishwe katika kufanya maamuzi yanayotolewa ndani ya mapambano dhidi ya biashara mbaya  ya binadamu na wanapaswa wapokee imani na kuwa baadaye wawajibikaji . Lazima wafundishwe nao  kuwa mtandao na kujua misingi ya sababu za biashara hii mbaya ya binadamu. Umaskini, ukosefu wa elimu, hukosefu wa haki msiniu za binadamu, ukosefu wa fursa za ajira halali, amani, haki na usawa ni mambo na mengi hayo yanayawafanya watu wengi wawe katika mazingira magumu. Vijana wanapata kujifunza na kutambua sheria zilizopo, ingawa katika hali nyingi haizitekelezwa, na ambazo zinakusudia kuharibu mtandao huo mbaya wa biashara, ambayo huwaadhibu wateja na lazima pia waelewe kuwa kuna haja kubwa ya sheria za kulinda wahanga.

Sr. Bottani,akifafanua zaidi  amesema wao  kama watawa wanajaribu kutembea pamoja na kuwasindikiza waathiriwa na watu wote ambao wamejikuta katika hali kama hiyo. Wako na vijana wengi kizazi kipya kwa sababu biashara hii unawakumba  vijana katika ulimwengu, na inawagusa watoto na ndiyo linbaki kuwa lengo la wahalifu hao wa biashara. “Vijana ndio wahanga wakuu wa usafirishwaji haramu, lakini pia ni rasilimali muhimu ambazo zinaweza kupata lugha ya kutosha kuwasiliana na vijana wengine leo hii. Kwa hiyo kazi hiyo inapaswa kufanywa na vizazi vipya, zaidi ya nyanja zao, ambazo wanajikita nazo katika maisha ya kidini, katika maisha ya raia, shuleni na vyuo vikuu, na hii ni muhimu sana kwa sababu tutaweza kuimaliza tu ikiwa kutakuwa na kubadilisha mawazo ya unyonyaji kuwa mawazo ya utunzaji, ambayo huenda zaidi ya majaraha yaliyosababishwa na vurugu, na ambayo lazima kwanza yapine na kupata ​​tiba ambayo inabadilisha njia ya kufikiria na kuishi”.

“Kuna mengi ya kufanya, anakiri mtawa huyo, ambaye, hata hivyo, amebanisha kuwa na mshangao wa kila siku, kutokana na kwamba kuna  aliyefika kutoka shule ya sanaa na ubunifu huko Massachusetts nchini Marekani ambaye aliamua kutekeleza mpango  wa kisanii kuanzia Talitha Kum, kutokana na kazi ya watawa. Pia kuna shule kadhaa za Italia ambazo zinaomba USMI, na Umoja wa wakuu wa Wata wa Italia, kuweza kutekeleza habari na shughuli za kuhamasisha uelewa juu ya suala hili na bado mifano mingi na mingi, yote ya vijana, yenye msingi, iwezekanavyo kuwa wapatanishi wa kiutamaduni, na muhimu kwa ajili ya kufikia ulimwengu wao, ulimwengu wa vijana shuleni, vyuo vikuu, jamii.

17 October 2021, 14:00