Papa Francisko tarehe 3 Septemba 2021 amekutana na kuzungumza na B Ingrida Šimonytė, Waziri mkuu wa Lithuania. Papa Francisko tarehe 3 Septemba 2021 amekutana na kuzungumza na B Ingrida Šimonytė, Waziri mkuu wa Lithuania. 

Waziri Mkuu wa Lithuania Akutana na Papa Francisko Mjini Vatican

Baba Mtakatofu Francisko na Waziri mkuu wa Lithuania: Kanisa Katoliki limekuwa na mchango mkubwa katika ustawi, maendeleo na mafao ya wengi nchini Lithuania. Imani ya Kanisa Katoliki imechangia mchakato wa kuendeleza kanuni maadili na utu wema; kwa kulinda na kudumisha utu, heshima na haki msingi za binadamu kama mtu mmoja mmoja na familia katika ujumla wake.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. –Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko, Ijumaa tarehe 3 Septemba 2021 amekutana na kuzungumza na Bi Ingrida Šimonytė, Waziri mkuu wa Lithuania pamoja na ujumbe wake. Baadaye amekutana pia na kuzungumza na Kardinali Pietro Parolin Katibu mkuu wa Vatican aliyekuwa ameambatana na Askofu mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu mkuu wa mambo ya nje na ushirikiano ya Kimataifa mjini Vatican. Baba Mtakatifu na mgeni wake, katika mazungumzo yao, wameridhishwa na uhusiano wa kidiplomasia kati ya Vatican na Lithuania.

Kanisa Katoliki limekuwa na mchango mkubwa katika ustawi, maendeleo na mafao ya wengi nchini Lithuania. Imani ya Kanisa Katoliki imechangia mchakato wa kuendeleza kanuni maadili na utu wema; kwa kulinda na kudumisha utu, heshima na haki msingi za binadamu kama mtu mmoja mmoja na familia katika ujumla wake. Baadaye, Baba Mtakatifu na mgeni wake, walijikita zaidi katika masuala yanayohusu ushirikiano wa Kimataifa miongoni mwa nchi mbalimbali, ili kukabiliana na changamoto mamboleo. Ugonjwa wa Virusi vya Korona, UVIKO-19, amani na usalama kikanda pamoja na kipeo cha machafuko ya kisiasa nchini Afghanstan ni kati ya mada zilizojadiliwa na viongozi hao wawili.

Lithuania
04 September 2021, 15:24