Kila tarehe 27 Septemba ya kila mwaka ni siku ya Utalii duniani:Baraza la Kipapa la Maendeleo Fungamani ya binadamu mwaka huu ujumbe unaangazia mkwamo wa sekta hii kutokana na janga Kila tarehe 27 Septemba ya kila mwaka ni siku ya Utalii duniani:Baraza la Kipapa la Maendeleo Fungamani ya binadamu mwaka huu ujumbe unaangazia mkwamo wa sekta hii kutokana na janga 

Siku ya Utalii duniani:Kard.Turkson anasema ujumuishwaji unahitajika!

Katika Ujumbe wa Baraza la Kipapa la Maendeleo fungamani ya Binadamu katika fursa ya Siku ya Utalii Duniani itakayoadhimishwa Septemba 27,linatoa kipaumbele cha sekta ya utalii iliyojaribiwa na janga kwamba ubinafsi na utaifa ni vishawishi hatari,kwamba watu na maeneo wana hatima moja na utawala wao lazima ufuate mitindo ya maisha ya heshima.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Njia shirikishi ya utalii ndiyo inazungukia ujumbe kutoka Baraza la Kipapa la  kuhamasisha Maendeleo Fungamani ya Binadamu kwa matazamio ya Siku ya Utalii Duniani mnamo tarehe 27 Septemba, iliyotangazwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii. Na njia inayojumuisha kwa maana hiyo ndiyo inatoa mwaliko, kama ilivyo kwenye Mafundisho ya Kanisa ambayo mara nyingi huoneshwa na Baba Mtakatifu Francisko, "kwa ajili ya uchumi wenye heshima na usawa, kwa ustawi wa kijamii na kiuchumi wa wanadamu wote, wa kuwa na  fursa ya kila mtu katika maendeleo fungamani. Baada ya janga hatuwezi kurudi kwenye usalama huo huo wa uwongo wa miundo iliyopita; tunahitaji mifumo inayoweza kupatikana inayojibu mahitaji msingi ya maisha ambayo ni ardhi, nyumba na kazi". Hii ndiyo aina ya ukuaji na maendeleo ambayo Baraza la Kipapa la kuhamasisha maendeleo fungamani ya binadamu unakusudia kukuza katika Siku ya Utalii Duniani.

Katika maandishi ya ujumbe huo uliotiwa saini na Mkuu wa Baraza hilo, Kardinali Peter Turkson, unabainisha kuwa athari kubwa ambayo janga limeleta kwa wafanyabiashara na wafanyakazi wa sekta hiyo, hasa wakati wa muda mfupi (part time) wa mshahara mdogo, ni kusisitiza kwa upya hasa thamani ya mtu na hadhi ya kibinadamu zaidi ya urasimu; takwimu na idadi ya uchumi wa watalii, kuhimiza zoezi la ubunifu ili kutoka nje ya mkwamo na baadaye umekumbisha jinsi ambavyo sisi sote tunayo hatima ya pamoja kama vile janga lilivyotufundisha na kwa hivyo lazima tupinge vishawishi vya ubinafsi na utaifa ambavyo vimeenea sana katika jamii nyingi za  kisasa. Ni kwa njia hiyo tu tunaweza kuepuka 'tofauti' ya virusi vinavyoenea wakati tunachochea uchumi mbovu  ambao unaruhusu watu wachache matajiri kumiliki zaidi ya kile walicho nacho wanadamu wengine, na wakati mifumo ya uzalishaji na matumizi huharibu sayari.

Kwa njia hiyo, katika tukio la Siku ya 42 ya Utalii Duniani mwaka huu, Baraza a Kipapa la Maendeleo Fungamani ya binadamu linatia moyo na kutoa wito.  Kwa kutia moyo utalii ambao unaoruhusu mkutano wa watu na maeneo ambapo usimamizi wa uzuri unafungua mitindo mipya  ya maisha yanayoheshimu wengine na sayari. Wito  kwa upande mwingine, ni kwa maaskofu na wale wanaohusika na usimamizo wa utalii kushirikiana na serikali mahalia katika kupendelea shughuli za kitalii zinazoendeleza uchumi wa haki na umoja, kumheshimu mwanadamu na mazingira. Utalii tu ulio na sifa hizi unaweza kuchangia ulimwengu ambao mwanadamu anahisi kutambuliwa kikamilifu, usnasomeka ujumbe huo.

Hatimaye katika ujumbe huo, Kardinali Turkson kwa niaba Baraza nzima anataja mfano halisi wa maendeleo fungamani ya udugu  uliozalishwa karibu na visa vingi vya shida ambazo janga hilo limesababisha. Tunaelezea shukrani zetu za dhati kwa wale wote ambao katika kipindi hiki muhimu kilicholetwa na janga hilo, wamefanya kusaidia mali na kiroho, watu ambao wanajikuta katika shida ya kiuchumi kwa sababu ya kusimamishwa kwa shughuli za watalii. Ujumbe huo unataja juhudi nyingi za suluhisho bora ambazo katika makanisa mengi wachungaji na washirika wao, wanaoungwa mkono na vyama vya kitaifa na vya mahalia, hasa Caritas, wamefanya ili kurekebisha shida ya kijamii. Huo ni mfano halisi wa maendeleo fungamani na kwamba udugu mpya wenye uwezo wa kusaidiana na kuheshimiana ambao tunahitaji haraka

11 September 2021, 16:08