Umati wa watu ukisubiri nje ya Uwanja wa ndege huko Kabul, nchini Afghanistan. Umati wa watu ukisubiri nje ya Uwanja wa ndege huko Kabul, nchini Afghanistan. 

Vatican:Mons.Putzer,amani na suluhisho kwa ajili ya kumaliza mivutano Afghanistan

Vatican inaendelea kufuatilia kwa umakini kuhusu hali halisi ya Afghanistan.Papa Francisko aliwaalika watu kusali naye kwa Mungu wa amani ili milio ya salaha iweze kusitishwa na suluishi zipatikane katika meza ya mazungumzo.Amesema hayo Monsinyo Putzer Mwakilishi wa Kudumu wa Vatican katika Makao ya Umoja wa Mataifa huko Geneva katika kikao cha Baraza kwa ajili ya haki za Binadamu kuhusu hali ya Afghanistan.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican.

Monsinyo John Putzer Mwakilishi wa kudumu wa Vatican katika ofisi za Umoja wa Mataifa huko Geneva, Jumanne tarehe 24 Agosti 2021 ametoa hotuba wakati wa kikao maalum cha Baraza kwa ajili ya Haki za binadamu kuhusu hali ya Afghanistan. Akianza hotuba yake amesema siku hizi, Vatican inaendelea kufuatilia kwa umakini kuhusiana na hali halisi ya Afghanistan.  Kwa hakika Papa Francisko hata hivyo amewaalika watu kusali naye kwa Mungu wa amani ili milio ya salaha iweze kusitishwa na suluishi ziweze kupatikana katika meza ya mazungumzo. Ni njia hiyo tu inaweza kuruhusu watu katika nchi, wanaume, wanawake, wazee na watoto kurudi katika nyumba zao na kuishi kwa amani na usalama na kuishi kwa kuheshimiana.

Kuna haja ya kuheshimu haki za binadamu

Mwakilishi wa Vatican aidha amewaalika sehemu zote kuheshimu haki ya kibinadamu na haki msingi ya kila mtu ikijumuisha haki kwa maisha, uhuru wa dini, haki ya uhuru wa kuzunguka na  haki ya mkutano wa  amani. Katika wakati huu mgumu amesema ni jambo muhimu sana kuwasaidia katika kupata matokeo na usalama kwa ajili ya juhudi za huduma ya kibinadamu  zilizomo nchi humo, katika roho ya mshikamano kimataifa, ili kutopoteza maendeleo yaliyofikiwa hadi sasa, hasa katika sekta ya afya na elimu. Ni matumaini ya Vatican kuwa amani na suluhisho kwa ajili ya kumaliza mivutano na kubaki na kwa kuamini kuwa ni mazungumzo shirikishi yanawakilisha zana msingi kwa ajili ya kufikia malengo ya amani. Hatimaye umetolewa wito kwa Jumuiya ya kimataifa kupitia mikataba ya matendo kwa kuwakaribisha wakimbizi katika roho ya udugu kibinadamu.

25 August 2021, 15:36