Rais Alexander Van der Bellen wa Austria tarehe 7 Juni 2021 amekutana na kuzungumza na Papa Francisko mjini Vatican. Rais Alexander Van der Bellen wa Austria tarehe 7 Juni 2021 amekutana na kuzungumza na Papa Francisko mjini Vatican. 

Rais wa Austria Akutana na Papa Francisko Mjini Vatican: Mazingira!

Baba Mtakatifu Francisko na Rais Alexander Van der Bellen katika mazungumzo yao wameridhishwa na uhusiano mwema wa kidiplomasia kati ya nchi hizi mbili. Baadaye wamejielekeza zaidi katika masuala ya kijiografia katika Ukanda wa Bara la Ulaya na katika Jumuiya ya Kimataifa kwa ujumla wake. Wamepongeza mchango wa Kanisa katika ustawi, maendeleo na mafao ya wengi!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko, Jumatatu tarehe 7 Juni 2021 amekutana na kuzungumza na Rais Alexander Van der Bellen wa Austria. Baadaye alipata pia fursa ya kukutana na kuzungumza na Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican aliyekuwa ameambatana na Askofu mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu mkuu wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa mjini Vatican. Baba Mtakatifu Francisko na Rais Alexander Van der Bellen katika mazungumzo yao wameridhishwa na uhusiano mwema wa kidiplomasia kati ya nchi hizi mbili.

Baadaye wamejielekeza zaidi katika masuala ya kijiografia katika Ukanda wa Bara la Ulaya na katika Jumuiya ya Kimataifa kwa ujumla wake. Wamepongeza mchango wa Kanisa katika ustawi, maendeleo na mafao ya watu wa Mungu nchini Austria. Kanisa limekuwa mstari wa mbele kunogesha mchakato wa mshikamano wa udugu wa kibinadamu; kwa kusimamia misingi ya haki, amani na maridhiano sanjari na utunzaji bora wa mazingira nyumba ya wote.

Austria

 

08 June 2021, 14:54