Kardinali Pietro Perolin Katibu wa Vatican Kardinali Pietro Perolin Katibu wa Vatican  

Kard.Parolin:hakuna ombi la kuzuia muswada wa Zan

Mahojiano na Katibu wa Vatican baada ya mjadala juu kumbu kumbu iliyotolewa kwa mamlaka ya Italia.“Tunapinga mtazamo wowote au ishara ya kutovumiliana au chuki kwa watu kwa sababu ya mwelekeo wao wa kijinsia.Wasiwasi wetu unahusu shida za tafsiri”.

NA ANDREA TORNIELLI

Hakuna ombi la kusimamisha sheria dhidi ya ushoga au shinikizo lisilostahili juu ya kazi ya Bunge la Italia, lakini ni kuripoti masuala kadhaa kuhusu ufafanuzi wa vifungu kadhaa vya Muswada DDL wa Zan. Na uamuzi wa kuelezea ndani ya mantiki za kawaida za kidiplomasia. Kwa muhtasari huu ndiyo simulizi ambayo inatoka katika maneno ya Katibu wa Vatican Kardinali Pietro Parolin, ambaye alikuwa huko Mexico wakati wa uchapishaji wa vifungu na baada ya kurudi Roma, Kardinali Parolin ameelezea sababu za mpango wa Vatican.

Mwashamu, ulitarajia kile kilichotokea?

Nilikuwa nimeidhinisha maelezo ya maneno yaliyotumwa kwa balozi wa Italia na kiukweli nilidhani kwamba kunaweza kuwa na matokeo. Ilikuwa, hata hivyo, hati ya ndani iliyobadilishwa katika tawala za serikali kupitia njia za kidiplomasia. Ni nakala iliyoandikwa na kufikiriwa kuwasilisha wasiwasi kadhaa na kwa hakika haikuwa si kwa ajili ya kuchapishwa.

Je! asili yake ni nini na ni wasiwasi gani wa Vatican juu ya Muswada DDL wa Zan?

"Kwanza kabisa, ningependa kuelezea kwamba hakuna njia yoyote iliyoombwa kuzuia sheria. Tunapingana na mtazamo wowote au ishara yoyote ya kutovumiliana au chuki kwa watu kwa sababu ya mwelekeo wao wa kijinsia na pia kabila lao au imani zao. Wasiwasi wetu unahusu shida za kutafsiri ambazo zinaweza kutokea ikiwa maandishi yaliyo na yaliyomo wazi na yasiyo na uhakika yangepitishwa, ambayo yangeishia kubadilisha ufafanuzi wa uhalifu na sio hatua ya mahakama, lakini bila kumpa hakimu vigezo muhimu vya kutofautisha. Dhana ya ubaguzi bado haijulikani sana katika yaliyomo. Kwa kukosekana kwa maelezo ya kutosha, kuna hatari ya kuweka tabia tofauti zaidi na kwa maana hiyo kufanya tofauti yoyote inayowezekana kati ya mwanamume na mwanamke iadhibiwe na matokeo ambayo yanaweza kuwa ya kutatanisha na ambayo kwa maoni yetu yanapaswa kuepukwa, muda mrefu wakati bado kuna muda. Hitaji la ufafanuzi ni muhimu sana kwa sababu sheria huhamia katika eneo la umuhimu wa jinai ambapo, kama inavyojulikana, ni nini kinaruhusiwa na kile kinachokatazwa kufanya lazima kiamuliwe vizuri".

Maoni mabaya yalitolewa ya uingiliaji wa “kuzuia” juu ya sheria ambayo bado inajadiliwa. Je unajibuje?

“Uingiliaji ulikuwa ndiyo kinga, lakini hasa kuwasilisha shida kabla ya kuchelewa. Muswada huo tayari umeidhinishwa, hata hivyo na tawi la Bunge. Uingiliaji unaofuata tu, ambao ni, mara tu sheria itakapopitishwa, ingekuwa imepigwa kura. Vatican ingeweza kushtakiwa kwa ukimya wa hatia, hasa wakati suala hilo linahusu mambo ambayo ni makubaliano.

Mpango wa Vatican unazingatiwa na watoa maoni kama usumbufu usiofaa...

"Haikuingiliwa. Serikali ya Italia ni ya kidunia, sio serikali ya  kukiri, kama Waziri Mkuu alivyosema. Nakubaliana kabisa na Waziri Draghi juu ya hali ya kidunia ya serikali na juu ya enzi kuu ya Bunge la Italia. Kwa sababu hii, chombo cha maelezo ya kukumbuka kilichaguliwa, ambacho ndiyo njia sahihi ya mazungumzo katika uhusiano wa kimataifa. Wakati huo huo, nilithamini mwito uliotolewa na Waziri Mkuu wa kuheshimu kanuni za kikatiba na ahadi za kimataifa. Katika muktadha huu kuna kanuni msingi, ambayo ni 'pacta sunt servanda'. Ni kwa sababu hii kwamba katika maandishi ya maelezo tulijizuia kukumbusha maandishi ya vifungu vikuu vya Mkataba na Serikali ya Italia ambavyo vinaweza kushambuliwa".

"Tulifanya hivyo katika uhusiano wa ushirikiano mwaminifu na ningeweza kuthubutu kusema juu ya urafiki ambao umeonesha na kutambulisha uhusiano wetu. Ninasema pia kwamba hadi sasa suala la makumbalinao lilikuwa halijazingatiwa wazi katika mjadala wa sheria. Kumbuka maelezo katika maandishi nilitaka kutilia maanani hatua hii, ambayo haiwezi kusahauliwa. Kama ilivyodhihirishwa pia na baadhi ya wafafanuzi, suala la uhuru wa maoni haliwahusu Wakatoliki tu, bali watu wote, wakigusa kile cha Mtaguso wa Pili la Vatican linafafanua kama 'kaburi la dhamiri'.

Kwa nini Vatican iliingilia kati na sio Baraza la Maaskofu wa Italia? Je! Kuna maoni tofauti?

“Baraza la Maaskofu wa Italia limefanya kila linalowezekana kuleta pingamizi kuhusu muswada huo. Kulikuwa na taarifa mbili juu ya mada hiyo na Gazeti Katoliki la Italia la kila siku, 'Avvenire', lilifuata mjadala huo kwa karibu sana. Hata Baraza la Maaskofu Italia (CEI), ambalo lina mwendelezo kamili wa maoni na hatua, haikuomba sheria kuzuiwa, lakini lilipendekeza mabadiliko. Kwa hiyo pia maelezo katika maandishi yanahitimisha na ombi la mabadiliko tofauti ya maandishi. Majadiliano ni halali kila wakati”.

25 June 2021, 16:31