Papa Francisko amemteuwa Monsinyo Visvaldas Kulbokas kuwa Balozi wa Vatican nchini Ukraine na kumpandisha hadhi kuwa Askofu mkuu. Papa Francisko amemteuwa Monsinyo Visvaldas Kulbokas kuwa Balozi wa Vatican nchini Ukraine na kumpandisha hadhi kuwa Askofu mkuu. 

Askofu mkuu Visvaldas Kulbokas Balozi wa Vatican Nchini Ukraine

Askofu mkuu mteule Visvaldas Kulbokas alizaliwa tarehe 14 Mei 1974 huko Klaipeda nchini Lithuania. Tarehe 19 Julai 1998 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Askofu mkuu mteule Visvaldas Kulbokas katika uwanja wa masomo, amekwisha kujipatia Shahada ya Uzamivu katika Masomo ya Taalimungu na Sheria za Kanisa. Tarehe Mosi Julai 2004 alijiunga na Diplomasia ya Kanisa.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amemteuwa Monsinyo Visvaldas Kulbokas, kuwa Balozi wa Vatican nchini Ukraine na kumpandisha hadhi kuwa ni Askofu mkuu. Hati kuteuliwa kwake, Askofu mkuu mteule Visvaldas Kulbokas alikuwa ni Mshauri wa Ubalozini. Askofu mkuu mteule Visvaldas Kulbokas alizaliwa tarehe 14 Mei 1974 huko Klaipeda nchini Lithuania. Baada masomo na majiundo yake ya Kikasisi tarehe 19 Julai 1998 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre.

Askofu mkuu mteule Visvaldas Kulbokas katika uwanja wa masomo, amekwisha kujipatia Shahada ya Uzamivu katika Masomo ya Taalimungu na Sheria za Kanisa. Tarehe Mosi Julai 2004 alijiunga na Diplomasia ya Kanisa na hatimaye kutumwa kufanya kazi zake nchini Lebanon, Uholanzi na Urussi. Baadaye alihamishiwa kwenye Sekretarieti kuu ya Vatican, Mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa Kimataifa na hatimaye, akatumwa nchini Kenya.

Uteuzi

 

16 June 2021, 07:49