Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu mkuu Francisco Escalante Molina kuwa Balozi mpya wa Vatican  nchini Haiti Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu mkuu Francisco Escalante Molina kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Haiti 

Askofu Mkuu Francisco Gerardo Escalante Molina, Balozi Haiti

Askofu mkuu Francisco Gerardo Escalante Molina alizaliwa tarehe 29 Januari 1965, Jimboni San Cristóbal de Venezuela nchini Venezuela. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi tarehe 26 Agosti 1989 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Tarehe 13 Juni 1998 akajiunga na Utume wa Diplomasia ya Kanisa. Tarehe 28 Mei 2016 akawekwa wakfu kuwa Askofu mkuu. 4 Juni 201, Balozi Haiti!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amemteuwa Askofu mkuu Francisco Gerardo Escalante Molina kuwa ni Balozi mpya wa Vatican nchini Haiti. Kabla ya uteuzi huu, Askofu mkuu Francisco Gerardo Escalante Molina alikuwa ni Balozi wa Vatican nchini Congo Brazzaville na Gabon. Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu Francisco Gerardo Escalante Molina alizaliwa tarehe 29 Januari 1965, Jimboni San Cristóbal de Venezuela nchini Venezuela. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi tarehe 26 Agosti 1989 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre.

Tarehe 13 Juni 1998 akajiunga na Utume wa Diplomasia ya Kanisa na kutumwa huko nchini: Sudan, Ghana, Malta, Nicaragua, Japan and Slovenia. Tarehe 21 Mei 2016 akateuliwa kuwa Balozi nchini Congo Brazzaville na Gabon na kupandishwa hadhi kuwa Askofu mkuu. Akawekwa wakfu tarehe 28 Mei 2016. Na tarehe 4 Juni 2021, Baba Mtakatifu Francisko akamteuwa kuwa ni Balozi mpya wa Vatican nchini Haiti.

05 June 2021, 14:51