Papa Francisko amemteua Monsinyo John Baptist Attakruh kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Sekondi-Takoradi nchini Ghana. Papa Francisko amemteua Monsinyo John Baptist Attakruh kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Sekondi-Takoradi nchini Ghana. 

Askofu John Baptist Attakruh Jimbo Katoliki la Sekondi-Takoradi

Askofu mteule John Baptist Attakruh alizaliwa tarehe 13 Oktoba 1957. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 30 Julai 1989 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Tangu wakati huo, amefanikiwa kuwa Makamu wa Gambera Seminari Ndogo ya St. Mary, Mkurugenzi wa Kituo cha Makatekista, Mkurugenzi wa Mashirika ya Kimisionari ya Kipapa, Mlezi na Mwalimu. Kumekucha!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.  – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amemteuwa Monsinyo John Baptist Attakruh kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Sekondi -Takoradi nchini Ghana. Kabla ya kuteuliwa kuwa Askofu mpya alikuwa ni Msimamizi wa Kitume wa Jimbo Katoliki la Sekondi -Takoradi “Sede Vacante ad nutum Sanctae Sedis”. Yaani kama Msimamizi wa Kitume, alikuwa anawajibika moja kwa moja na Vatican katika masuala yote ya uongozi na usimamizi wa Jimbo la Sekondi –Takoradi. Askofu mteule John Baptist Attakruh alizaliwa tarehe 13 Oktoba 1957. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 30 Julai 1989 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre.

Tangu wakati huo, amefanikiwa kuwa Makamu wa Gambera Seminari Ndogo ya St. Mary, Mkurugenzi wa Kituo cha Makatekista, Mkurugenzi wa Mashirika ya Kimisionari ya Kipapa, Mlezi na Mwalimu. Kati ya Mwaka 2004 hadi mwaka 2014 alikuwa anatekeleza utume wake nchini Marekani sanjari na kujiendeleza na masomo na hatimaye, akajipatia Shahada ya Uzamili katika Sayansi ya Elimu. Amekuwa pia Mratibu wa Sinodi ya kwanza ya Jimbo la Sekondi-Takoradi, Mwaka wa Jubilei ya Huruma ya Mungu, Paroko na Mwalimu wa Liturujia hatimaye, mwaka 2020 akateuliwa kuwa Msimamizi wa Kitume wa Jimbo Katoliki la Sekondi -Takoradi “Sede Vacante ad nutum Sanctae Sedis”.

Uteuzi Ghana
24 June 2021, 16:36