Maadhimisho ya misa ya Papa Francisko huko  Yangon MYANMAR Maadhimisho ya misa ya Papa Francisko huko Yangon MYANMAR 

Mei 16 Papa ataadhimisha misa kwa ajili ya waamini wa Myanmar,Roma

Maadhimisho ambayo Papa ataongoza katika Kanisa kuu la Mtakatifu Petro,yanafuata miito mingi ya mazungumzo na mapatano katika nchi hiyo na wito wa mwisho ulikuwa Dominika tarehe 2 Mei wakati wa sala ya Malkia wa Mbingu amewaomba wote kusali kila siku salamu Maria moja wakati wa Rosari.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Tangazo la misa limemefika alasiri tarehe 3 Mei 2021 kutoka nyumba ya Kipapa kwamba Baba Mtakatifu Francisko ataadhimisha Misa kwa jumuiya ya waamini wa Myanmar wanaoishi Roma. Maadhimisho hayo yatafanyika tarehe 16 Mei 2021 katika Sherehe ya Kupaa kwa Bwana mbinguni, saa 4.00 asubuhi katika altare ya Mtakatifu Petro. Ilikuwa ni katika mazungumzo ya mpangilio  juu ya ibada ya utamaduni wa Maria kwa mwezi wa Mei na kufuatia mpango wa wa Rozari ambao unahusisha madhabahu makuu ya ulimwengu, ambapo Papa  Francisko aliitaja nchi hiyo kwa kusifu mpango wa Kanisa la Birmania tarehe 2 Mei. Papa alisema: “Katika muktadha huo kuna mpango ambao uko karibu sana  moyoni wangu:ule wa Kanisa la Birmania, ambalo ninawaalika tuombee amani kwa kuhifadhi Salamu Maria moja kila siku katika Rozari kwa ajili ya Myanmar. Kila mmoja wetu humwelekeea mama wakati anahitaji au ana shida; sisi, mwezi huu,tumuombe Mama yetu wa Mbinguni azungumze katika mioyo ya wale wote wanaohusika na Myanmar ili waweze kupata ujasiri wa kutembea njia ya kukutana na upatanisho na amani”.

Miito ni mingi ya Papa kwa ajili ya nchi hiyo

Ni miito mingi ya mazungumzo na utulivu illiyotolewa na Baba Mtakatifu Francisko tangu, Mosi Februari, wakati jeshi lilipindua serikali ya Aung San Suu Kyi inayodhibiti nchi. Maandamano ya idadi ya watu ambayo imeingia barabarani mara kadhaa dhidi ya mapinduzi ya kijeshi ambayo yamesababisha mapigano na vurugu na vifo kadhaa wakadhaa. Na mara kwa mara Papa Francisko amekuwa akiomba waandamanaji wasifanye vitendo vya vurugu na mamlaka wasilazimishe waandamanaji kwa kutumia nguvu.

Papa anaomba mazungumzo

Papa Francisko wakati wa katekesi yake mnamo tarehe 17 Machi alisema:“Mazungumzo juu ya ukandamizaji na maelewano juu ya mfarakano yashinde na jumuiya kimataifa itoe msaada unaohitajika ili matakwa ya watu wa Myanmar yasikubaliane na ghasia”.  Lakini alikuwa ametumia usemi wenye nguvu zaidi akisema: "Kwa mara nyingine tena na kwa huzuni nyingi nahisi udharura wa kuibua hali ya kushangaza huko Myanmar ambapo watu wengi, hasa vijana, wanapoteza maisha yao na tumaini kwa nchi yao. Mimi pia ninapiga magoti katika barabara za Myanmar na kusema: vurugu ziishe. Mimi pia ninyoosha mikono yangu na kusema: ruhusi mazungumzo yashinde. Damu haitasuluhisha chochote. Mazungumzo yanashinda”.

Vijana wa Myanmar na matumaini ya maisha baada ya amani

Na mnamo tarehe 3 Machi 2021 tena kwenye katekesi yake Papa alirudia kukumbuka idadi ya watu wa zamani wa Birmania ambapo habari za mivutano mikali zilikuwa bado zina cheche kubwa akitumaini suluhisho la amani. Mawazo yake yalielekezwa hasw kwa vijana na viongozi waliokamatwa:

Papa alisema:“Ningependa kutoa angalizo kwa mamlaka zinazohusika, ili mazungumzo yashinde ukandamizaji na maelewano juu ya mafarakano. Natoa rai pia kwa jumuiya ya kimataifa kuhakikisha kwamba matakwa ya watu wa Myanmar hayazuiliwi na vurugu. Waache vijana wa ardhi hiyo wapendwa wapewe tumaini la siku zijazo ambapo chuki na dhuluma haziwezi kuacha nafasi ya kukutana na maridhiano. Hatimaye  ninarudia tumaini lililooneshwa mwezi mmoja uliopita: kwamba njia kuelekea demokrasia iliyofanywa kwa miaka ya hivi karibuni na Myanmar inaweza kuendelea kupitia ishara thabiti ya ukombozi wa viongozi wa kisiasa waliofungwa”.

03 May 2021, 17:59