2021.05.20 Kardinali Marc Ouellet 2021.05.20 Kardinali Marc Ouellet 

Kard.Ouellet:Umisionari unatokana na miundo mipya

Kardinali Ouellet,Rais wa Baraza la kipapa la Maaskofu katika Mkutano wa Baraza la Maaskofu barani Amerika Kusini amesema“Uongofu wa moyo huzaliwa kama tunda la roho ya umisionari na kutokana na uzoefu huu ndipo kunatokea msukumo wa kubadilika,kuunda miundo mipya.Ikiwa hii isingekuwa hivyo, tungeishia kusema tu juu ya shirika,juu ya uchambuzi wa kazi ambao unaacha matunda ya utume pembeni.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Roho ya umisionari ni nyenzo msingi ya kuhuisha miundo ya Baraza la Maaskofu la Amerika Kusini Celam na ndiyo muhtasari ambao ni kiini cha uingiliaji kati uliotolewa na Kardinali Marc Ouellet, Rais wa Baraza la Kipapa la Maaskofu na rais wa Tume ya Kipapa ya Amerika Kusini (Cal), wakati wa Mkutano Mkuu wa 38 wa Celam, unaendelea tangu tarehe 18 hadi 21 Mei na ambao kutokana na janga la virusi, unaendelea kufanyika kwa njia ya mtandao.  Matunda ya mkutano huu wa kanisa baada ya muda wa kusikiliza na kutafakari, itakuwa ishara ya Kanisa katika uongofu endelevu wa kichungaji na umisionari ambao unakua katika kuishi na kupitisha imani, matumaini na mapendo. Katikati, maneno ya Kardinali Ouellet, pia ni wito wa uinjilishaji na ushirikiano kati ya Makanisa ya bara hili, ili waweze kutimiza utume wao wa msingi na Yesu Kristo ajulikane, apendwe na kushuhudiwa na watu wa Mungu, amesema.

Rais wa Baraza la Kipapa la Maaskofu vile vile amerudia  kuelezea hitaji la kushinda jaribu la kuacha mwelekeo wa kulaani, badala yake, ni kusonga kwa ile ya tangazo la maisha mapya yanayotolewa na Kristo: kwa  maana hiyo, ametoa himizo la kutimiza kila linalowezekana la juhudi za kujenga madaraja kati ya kanisa, parokia na jumuiya ndogo ndogo za majimbo  pia kati ya Mabaraza  ya Maaskof, kwa sababu hii itakuwaishara ya kinabii ya Kanisa na chombo cha ushirikiano na Mungu na umoja wa jumuiya ya wanadamu. Kwa kuongezea, akiangalia ukweli wa kisasa, uliowekwa na na migawanyiko ya kisasa ambayo ni hatari ya kutawanyika na utupu, kardinali amesisitiza juu ya hitaji la kuendelea kutafuta umoja, ambao ni lazima.

Mkuu wa baraza la Maaskofu pia ameeleza ishara za motu proprio "Antiquum ministererium" ya hivi karibuni ambayo Baba Mtakatifu Francisko ameanzisha huduma ya kawaida ya katekista na ambayo amesema ni kitendo ambacho, kinaangazia umuhimu wa kujitoa kwa umisionari. Huduma inayoanza kutoka chini na ya ushirikiano kati ya wote. Uongofu wa moyo huzaliwa kama tunda la roho ya umisionari na kutokana na uzoefu huu ndipo kunatokea msukumo wa kubadilika, kuunda miundo mipya. Ikiwa hii isingekuwa hivyo, tungeishia kusema tu juu ya shirika, juu ya uchambuzi wa kazi ambao unaacha matunda ya utume pembeni

Hatimaye, kardinali amependekeza kwamba mchakato huu wote uishi katika hali ya kweli ya sala na utambuzi ambayo inaweza kuleta pamoja Kanisa la Amerika Kusini kutafakari juu ya umuhimu wa kufanya kazi kwa utamaduni wa kweli wa ufundi ambao huimarisha safari ya walei na kujitoa, watu katika kukutana kwao na Mungu . Wakati wa sasa, uliowekwa na janga la Covid-19, amesisitiza rais wa Maskofu, unahitaji kutazama kwa uangalifu hali halisi ya kijamii barani, na hitaji la kubadilika kujenga miundo mipya na kuendeleza mipango mipya katika huduma ya uinjilishaji. "Tuna imani katika Kristo Mfufuka ambaye, kati yetu, atatuongoza kutambua mpango wa Mungu kupitia huduma yetu ya kichungaji".

20 May 2021, 15:30