Tarehe 2 Aprili 2021 ni miaka 16 tangu kifo cha Mtakatifu Yohane Paulo II

Ilikuwa mnamo tarehe 2 Aprili 2005,Jumamosi ambapo maelfu ya waamini walikuwa wamekusanyika wakiwa wanasali hadi walipotangaziwa habari za kuhuzunisha za kifo cha Mtakatifu Yohane Paulo II.Video fupi inaonesha akifuatilia njia ya msalaba siku ya Ijumaa Kuu tarehe 25 Machi akiwa katika Kikanisa cha Jumba la Kitume.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican.

Ilikuwa mnamo tarehe 2 Aprili 2005, siku ya Jumamosi Kuu ambapo maelfu ya waamini wakiwa wamejumuika katika Uwanja wa Makatifu Petro wanasali hadi walipoona anatokeza Katibu wa Vatican wa wakati huo alikuwa Kardinali Leonardo Sandri, alipotoa usiku ule tangazo la huzuni lifuatalo:  “Ndugu kaka na  dada wapendwa, saa 3:37 usiku huu, Papa wetu mpendwa Yohane Paulo II amerudi nyumbani kwa Bwana. Tumuombee.”

 “Mtakatifu haraka”

Maneno ya Kardinali Sandri yalifuatwa na simanzi kubwa na kutoka hapo sauti ya “mtakatifu haraka” ilienea kati ya mahujaji waliokuwa hapo Roma ili kumuaga Papa mpendwa sana wa Kipoland. Kutangazwa kwake kuwa mtakatifu,  hata hivyo kulifanyika mnamo tarehe 27 Aprili 2014, na Baba Mtakatifu Francisko, pamoja na uwepo wa Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI.

MTAKATIFU YOHANE PAULO II AKIFUATILIA NJIA YA MSALAMBA AKIWA KIKANISA CHA JUMBA LA KITUME 25 MACHI 2005
MTAKATIFU YOHANE PAULO II AKIFUATILIA NJIA YA MSALAMBA AKIWA KIKANISA CHA JUMBA LA KITUME 25 MACHI 2005

Miaka kumi na sita bila Yohane Paulo II

Pasaka ya 2005 haitasahulika kamwe maana iliacha alama kama ya mwisho ya Mtakatifu Yohane Paulo II. Kwa namna ya pekee, ya picha za Njia ya Msalaba mnamno tarehe 25 Machi 2005 ambazo hazikuweza kufutika na Mtakatifu wa baadaye, alifuatilia tafakari wakati huo akiwa katika Kikanisa cha Jumba la Kitume iliyokuwa imeandikwa na Kardinali wa wakati ule Joseph Ratzinger, na ambaye baadaye alichaguliwa kuwa Papa. Katika video inaonesha na kukumbuka Njia ya Msalaba ya mwisho ya Mtakatifu Yohane Paulo II akifuatilia kutokea Jumba la Kitume.

02 April 2021, 14:40