Siri za majumba ya makumbusho Vatican zaanza kuoneshwa kwenye safu za video!
Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.
Siri na historia zisizojulikana, udadisi huliofichika nyuma ya uzuri unaotambulika ulimwenguni wa kazi bora za makusanyo ya Vatican. Celata Pulchritudo.( calata pulkritudo ), Siri za Makumbusho ya Vatican”, ni mpango mpya wa vyombo vya habari ulioundwa kwa ushirikiano kati ya Radio Vatican na Makumbusho ya Vatican. Kuanzia tarehe 20 Aprili 2021 safu ya video fupi zimeanza kutolewa zikikusudia kuelezea sanaa ya makusanyo ya kipapa kwa njia mpya.
Kutoka katika vyanzo vya msukumo wa walimu wakubwa kama vile Michelangelo au Raphaeli, hadi haiba na siri ya ustaarabu wa zamani kabla ya Ukristo; kutoka nyuma ya pazia la Jumba la makumbusho limezingatiwa na vizazi vya wasanii kuwa shule ya ulimwengu, kwa urithi wa maarifa, utafiti, uhifadhi na urejeshwaji na kuorodhwa hadi kufikia sisi kupitia karne zote.
Mchakato wa kusimulia hayo utaendelezwa kila mwezi kwa mwaka mzima kupitia matoleo mawili ya video: moja iliyo na maelezo ikiambatana na nakala ya maelezo, nyingine fupi inayolenga hadhira ya mitandao wa kijamii. Yaliyomo yatasambazwa kupitia tovuti na mtandao wa kijamii wa Vatican News na Makumbusho ya Vatican.
Itakuwa njia ya kutoa mwonekano mpya kwenye Makumbusho ya Vatican ambayo, yalifungwa katika miezi ya hivi karibuni kufuata kanuni za sasa juu ya janga la Covid-19, hata hivyo hawajawahi kuacha, kwa kujibu wito wao kama mahali pa kuishi. “Celata Pulchritudo” pia ni fursa ya kujifunza juu ya wataalamu na ujuzi tofauti ambao kila siku hujiweka katika huduma ya taasisi iliyoundwa kudhihirisha uzuri kwa ulimwengu, na kwa maana nyingine ni njia ya upendeleo ya kukutana na Mungu.
Hata kazi zinazojulikana zaidi na zilizopigwa picha zaidi kwa mujibu wa Andrea Tornielli, mkurugenzi wa wahariri wa vyombo vya habari, Vatican amesema kuna habari ambazo hazijulikani na ambazo zinahitaji udadisi na mambo ya kugundua: shukrani kwa msaada wa wale wanaojifunza, kutunza, kurejesha na kuhifadhi, jaribu hili linafanikiwa ili kuwaleta karibu watu wengi iwezekanavyo katika hazina hizi za uzuri.
Jumba la makumbusho kwa hakika hasa watu wote kwa mujibu wa maoni ya Monsinyo Paolo Nicolini naibu mkurugenzi wa majumba ya Makumbusho ya Vatican amesema ni wanawake na wanaume wanaofanya kazi kila siku kuhifadhi na kukuza moja ya makusanyo maarufu ya kazi bora ulimwenguni. Ni kwao hao wahusika wakuu wa mpango huu, ambao shukrani zake zinawaendea