Papa katika Maadhimisho ya Misa Takatifu katika Madhabahu ya Huruma ya Mungu 2020 Papa katika Maadhimisho ya Misa Takatifu katika Madhabahu ya Huruma ya Mungu 2020 

Sikukuu ya Huruma:Papa ataongoza Misa katika Kanisa la Roho Mtakatifu

Tarehe 11 Aprili ni Siku Kuu ya Huruma ya Mungu ambapo kwa mara nyingine tena ya pili,Papa Francisko hata mwaka huu ataongoza Liturujia ya Ekaristi katika Madhabahu ya Huruma ya Mungu karibu na Vatican.

Na Sr Angela Rwezaula -Vatican.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa msemaji wa vyombo vya habari Vatican, kwa waandishi wa habari ametaarifu kuwa hata mwaka huu, Papa Francisko anarudi kuadhimisha Misa Takatifu ya faragha saa 4.30 asubuhi majira ya Ulaya katika Kanisa la Roho Mtakatifu, Sassia, karibu na Vatican, ambalo ni Madhabahu ya Huruma ya Mungu. Ni katika fursa ya Siku Kuu ya Huruma ya Mungu.

Hiyo ni Dominika ya Huruma ya Mungu iliyotangazwa miaka 21 iliyopita na Mtakatifu Yohane Paulo II ambayo huadhimisha katika Dominika ya Pili ya Pasaka. Mwisho wa misa Takatifu hiyo katika Kanisa hilo hilo, Papa ataongoza Sala ya Malkia wa Mbingu,  amebainisha msemaji.

Mwaka jana, katika tukio hilo kiukweli,  Papa aliadhimisha Ekaristi, kwa faragha, katika Kanisa la Roho Mtakatifu,  Sassia ambalo,  Papa Wojtyla yaani Mtakatifu Yohane Paulo II alilitolea ibada iliyohamasishwa na  Mtakatifu Faustina Kowalska. Ilikuwa ni katikati ya janga ambapo mwaka jana Papa Francisko alikumbuka kwamba huruma ya Mungu ni mkono ambao siku zote hutuinua. Mungu hachoki kunyoosha mkono wake ili kutuinua kutoka katika maporomoko yetu”.

Mawazo yake kwa maana hiyo Papa yalikuwa yamewaendea wale wote walio katika  hali ngumu iliyotokea na kuenea kwa Covid-19 na kusisitiza hatari ya kusahau waliobaki nyuma, walio  hatarini na pia  ambao walikumbwa na virusi  vya ubinafsi. Wasiojali na ambao wanapata kuchagua watu, kuwatupa maskini, kutoa kafara wale walio nyuma katika mwavuli wa madhabahu ya maendeleo.

Janga hilo alisisitiza kuwa linatukumbusha, kwamba hakuna tofauti na mipaka kati ya wale wanaougua. Sisi sote ni dhaifu, sawa, wote tunathaminiwa. Kinachotokea kinatutikisa ndani. Ni wakati sasa wa kuondoa ukosefu wa usawa, kuponya dhuluma inayodhoofisha afya ya wanadamu wote! Papa alitoa mwaliko wake wa nguvu ili kuonesha huruma kwa wale waliodhaifu na mshikamano . “Ni kwa njia hiyo tu  alisema tutaweza kujenga upya ulimwengu mpya”.

Ikumbukwe kwamba Misa Takatifu na sala ya Malkia wa Mbingu Dominika ya Pili ya Pasaka, tarehe 11 Aprili 2021 vitatangazwa moja kwa moja kwenye Vyombo vya Habari vya Vatican na mtiririko kwenye Habari ya Vatican na wakati huo huo tafsiri mbashara kwa Kiitaliano, Kifaransa, Kiingereza, Kijerumani, Kihispania, Kireno na Kiarabu.

08 April 2021, 17:02