Papa na Mkesha wa Pasaka:Kristo anaishi leo hii na daima anasaidia kuanza kwa upya!

Katika mkesha wa Pasaka 2021,Papa Francisko amewaalika waamini wote ulimwenguni kwenda Galilaya kama tangazo la Yesu kwa maana kuna uwezekano wa kuanza upya daima kwa sababu daima kuwa maisha mapya ambayo Mungu anauwezo wa kutufanya tuanze tena licha ya kushindwa kwetu.Video fupi inaonesha matukio ya mkesha huo katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro.

Na Sr Angela Rwezaula- Vatican.

Inawezekana kuanza kila wakati, kwa sababu kila wakati kuna maisha mapya ambayo Mungu anauwezo wa kuanza upya ndani yetu zaidi ya kushindwa kwetu. Hata katika vifusi vya moyo wetu kila mmoja wetu anajua, anajua vifusi vya moyo wake, Mungu anaweza kujenga kazi ya sanaa, hata kutoka katika vipande vilivyoharibika vya ubinadamu wetu, Mungu huandaa historia mpya. Yeye hututangulia kila wakati: katika msalaba wa mateso, ukiwa na kifo, na vile vile katika utukufu wa maisha ambayo yamezaliwa upya, ya historia inayobadilika, ya tumaini lililozaliwa upya. Ni uthibitisho wa kina wa Papa Francisko wakati wa mahubiri yake ya Mkesha wa Pasaka tarehe 3 Aprili 2021 katika Kanisa kuu la Mtakatifu Petro.

Video fupi hapo juu inaonesha baadhi ya matukio muhimu ya Ibada kuu hiyo ya mkesha wa Ufufuko wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliyeteswa, akafa Msalabani na kufufuka siku ya tatu kama ilivya. Uwepo wa waamini wachache katika Kanisa Kuu ni kutokana na kanuni zilizoweka za kufuata hatua za kuzuia maambukizi ya janga la sasa la ulimwengu.

MKESHA WA PASAKA 2021
MKESHA WA PASAKA 2021

Papa Francisko akiendelea kufafanua juu ya Injili iliyosomwa amesema”:”Kwenda Galilaya, kwa upande mwingine, inamaanisha kujifunza kwamba imani,ili iwe hai, lazima ijikite katika mchakato wa safari. Lazima ifufue mwanzo wa safari kila siku, mshangao wa kukutana kwa mara ya kwanza. Na baadaye ujiaminishe, bila dhana ya kujua tayari kila kitu, lakini kwa unyenyekevu wa yule anayejiachia kushangazwa na njia za Mungu. Sisi tunaogopa mshangao wa Mungu; kwa kawaida tunaogopa kwamba Mungu anaweza kutushangaza. Na leo hii Bwana anatualika tuaache tushangazwe”.

MKESHA WA PASAKA KATIKA KANISA KUU LA MTAKATIFU PETRO
MKESHA WA PASAKA KATIKA KANISA KUU LA MTAKATIFU PETRO

Aidha Papa Francisko amesisitiza kwamba“Tunakwenda Galilaya kugundua kwamba Mungu hawezi kuwekwa kati ya kumbukumbu za utoto lakini yeye yuko hai, kila wakati haishi kutushangaza. Mfufuka, haachi kutushangaza. Tazama hapa kuna tangazo la pili la Pasaka: imani siyo marudio ya wakati uliopita. Yesu sio mtu aliyepita. Yeye ni hai, hapa na sasa. Anatembea na wewe kila siku, katika hali unayoiishi,  katika jaribio unalopitia, katika ndoto unazobeba ndani mwako. Anafungua njia mpya ambayo inaonekana kwako kuwa haiwezekani na anakusukuma kwenda dhidi ya wimbi la majuto ya tayari nilishaona. Hata ikiwa kila kitu kwako kinaonekana kupotea, tafadhali jifungulie mwenyewe katika mshangao wa mapya: atakushangaza”.

04 April 2021, 16:24