2021.04.20 COP15 Mkutano kuhusu Bioanuwai kwa kuongozwa na Laudato sì 2021.04.20 COP15 Mkutano kuhusu Bioanuwai kwa kuongozwa na Laudato sì 

Mkutano kuhusu Bioanuwai kwa kuongozwa na Laudato sì

Kwa kutumia maneno ya Madhumuni,Kanuni,Uchochezi,Mazoezi na Mapendekezo, kwa kuongozwa na Waraka wa Laudato, umefanyika mkutano kwa kushirikiana ili kuonesha kuwa Laudato si' inatumika katika bioanuwai kati wahusika wa kikanisa,watendaji wa kisayansi na waamuzi.Watoa mada ni Kardinali Turkson Rais wa Baraza la Kipapa la maendeleo Fungamani ya binadamu na Dk. Jane Goodall,Mwanzilishi wa Taasisi ya Jane Goodall & Mjumbe wa Amani wa Umoja wa Mataifa.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Tarehe 20 Aprili 2021, umefanyika mkutano juu ya Bioanuwai kwa njia ya mtandao, ambao umeongozwa na Waraka wa Laudato si'. Tukio hilo limeandaliwa na Baraza la Kipapa la Huduma ya Maendeleo Fungamani ya binadamu na Tume ya Vatican ya  COVID-19, pamoja na kikundi cha Nguvu kazi ya Ekolojia. Waliotoa mada katika mkutano huo ni Kardinali Peter K. A. Turkson,  Rais wa Baraza la Kipapa la Kuhamasisha maendeleo Fungamani ya Binadamu, na  Dk. Jane Goodall ,DBE, Mwanzilishi wa “Jane Goodall Institute”,  yaani Taasisi ya Jane Goodall na Mjumbe wa Amani wa Umoja wa Mataifa. Leo hii tunajikuta tunakabiliana na migogoro mingi migogoro ya afya ambayo imetokana na COVID-19, migogoro ya mabadiliko ya tabia nchi na mgogoro wa baioanua, kwa maana hiyo ni migogoro mitatu inayosukana na  ambayo inatoa mwaliko wa nguvu wa kubadilisha mwelekeo ili kwenda katika ustaarabu mwema ili kuwa na maisha ya kiekolojia fungamani.

Ripoti  kuhusu baioanuai ulimwenguni ya Umoja wa Mataifa inabainisha juu ya umuhimu wa bioanuwai katika kushughulikia mabadiliko ya tabianchi, usalama wa chakula wa muda mrefu na inahitimisha ikibanisha kuwa hatua ya kulinda bioanuwai ni muhimu ili kuzuia magonjwa ya mlipuko ya baadaye. Wahusika wa ulimwengu wa masomo, utafiti wa kisayansi na mihimili ya Kanisa wanahisi kweli hitaji la kuanza wakati wa kutafakari, kwani matokeo ya mizozo ya sasa yanabadilisha maisha na kuhitaji jukumu la kutenda kwa haraka bila kupoteza wakati.

Hii inahitajika sana kwa kufuata mafundisho ya Baba Mtakatifu Francisko yaliyomo katika Waraka wake wa  Laudato si ' ili  kuunda uhusiano muhimu na uumbaji na kuhamasisha maelfu ya watu kupitia elimu na kuzaliwa kwa upya kwa mifumo ya ekolojia yenye afya duniani. Wakati bioanuwai inastawi, maisha ya mwanadamu hustawi. Kwa kutumia maneno matano: Purposes, Principles Provocations Practices Proposals yaani Madhumuni, Kanuni, Uchochezi, Mazoezi na  Mapendekezo,  wakuu hawa katika mkutano  wao wameyafanyia  kazi kwa kushirikiana ili kuonesha  kuwa inawezakana kwa dhati Laudato si 'inayotumika katika bioanuwai kati wahusika wa kikanisa, watendaji wa kisayansi na waamuzi

Na hii ni kutoka katika Mapendekezo, Kushiriki hekima, uelewa, uzoefu, mifano na ufahamu wa pande zote, hasa kwa kuzichota kutoka katika sehemu ambazo maarifa hukomaa, tamaduni asili na za kisayansi, Maandiko Matakatifu, Mafundisho Jamii ya Kanisa kama vile (Laudato si ') juu ya bioanuwai. Watoa mada hawa pia wamesaidia na kuhamasisha juu ya ulinzi na urejesho wa bioanuwai katika mikutano ya COP15 na COP26; Aidha wamewaalika Jumuiya ya kikanisa kwa ngazi ya ulimwengu ili kuanzisha mazungumzo juu ya bioanuwai kwa namna ya kupata njia mpya za Kanisa na familia ya wanadamu ili kuponya na kurejesha uhusiano na kazi ya uumbaji. Nguzo ya 4 ilikuwa ni kuweka upya mifumo ya kijamii na maumbile kulingana na janga la COVID-19. Kwa mfano, mapendekezo mapya ya maendeleo fungamani ya binadamu.

20 April 2021, 15:56