Baba Mtakatifu Francisko amemtea Monsinyo Raphael P'Mony Wokorach kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Nebbi, nchini Uganda. Baba Mtakatifu Francisko amemtea Monsinyo Raphael P'Mony Wokorach kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Nebbi, nchini Uganda. 

Askofu Raphael P'Mony Wokorach Jimbo Katoliki la Nebbi, Uganda

Askofu mteule Raphael P’Mony Wokorach, M.C.C.J. alikuwa ni Kamishna wa Kitume wa Shirika la Mitume wa Yesu, AJ. Alizaliwa tarehe 21 Januari 1961 Jimbo Katoliki la Arua, Uganda. Baada ya majiundo yake ya kikasisi na kitawa, tarehe12 Oktoba 1992 akaweka nadhiri za daima. Na tarehe 25 Septemba 1993 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. 31 Machi 2021 akateuliwa kuwa Askofu.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.  – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Monsinyo Raphael P’Mony Wokorach, M.C.C.J. wa Shirika la Wamisionari wa Comboni, kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Nebbi, nchini Uganda. Kabla ya uteuzi huu, Askofu mteule Raphael P’Mony Wokorach, M.C.C.J. alikuwa ni Kamishna wa Kitume wa Shirika la Mitume wa Yesu, AJ. Alizaliwa tarehe 21 Januari 1961 huko Ojigo, Jimbo Katoliki la Arua, Uganda. Baada ya masomo na majiundo yake ya maisha ya kitawa katika Shirika la Wamisionari wa Wacomboni wa Moyo Mtakatifu wa Yesu akaweka nadhiri zake za daima tarehe12 Oktoba 1992. Kunako tarehe 25 Septemba 1993 alipewa Daraja takatifu ya Upadre.

Tangu wakati huo kama Padre amefanya utume wake wa kimisionari katika nchi mbalimbali kama vile: DRC na Togo. Na kati ya mwaka 2003 hadi mwaka 2007 alitumwa nchini Marekani, kuwa ni mlezi kwenye Chuo cha Wacomboni Kimataifa. Kati yam waka 2007 hadi mwaka 2015 alikuwa nchini Kenya kama mlezi na jaalimu kwenye Chuo Kikuu cha Tangaza. Kati yam waka 2011 hadi mwaka 2013 alichaguliwa kuwa ni kati ya Washauri wa Kanda ya Shirika la Wamisionari wa Wacomboni wa Moyo Mtakatifu wa Yesu nchini Kenya. Kati ya Mwaka 2015 hadi mwaka 2018 aliteuliwa na Vatican kuwa ni Kamishna wa Kitume wa Shirika la Mitume wa Yesu, AJ. Na hadi kuteuliwa kwake ameendelea kuwa ni Kamishana wa Shirika la Mitume wa Yesu, AJ lenye Makao yake makuu Lang’ata, Jijini Nairobi.

Uteuzi Uganda
01 April 2021, 16:31