Wazee ni waathirika hasa wakati wa janga la virusi vya corona lakini hai na wapo katika jamii ya Ulaya. Wazee ni waathirika hasa wakati wa janga la virusi vya corona lakini hai na wapo katika jamii ya Ulaya. 

Hollerich: Wazee ni ubinadamu na kesho ya Ulaya

Umefanyika mkutano kwa njia ya mtandao tarehe Mosi Machi ulioandaliwa na Kamati ya Maaskofu wa Umoja wa Ulaya (Comece)na Shirikisho la Vyama katoliki vya familia barani Ulaya (Fafce).Mada iliyowaongoza ni"Wazee na wakati ujao wa Ulaya".Ni katika Muktadha wa tafakari juu ya janga ambalo limewakumba kwa kiasi kikubwa wazee na udhaifu wa kijamii.Katika takafakari ni Kardinali Hollerich na Katibu Msaidizi wa Baraza la Kipapa la Walei.

Na Sr. Angela Rwezaula -Vatican.

Wazee ni waathirika hasa wakati wa janga la virusi vya corona, lakini wapo hai katika jumuiya ya Ulaya ili kuweza kuwa kisima cha matumaini kwa walio vijana zaidi. Ilikuwa ni hali halisi ya wazee ambayo imekuwa kiini cha mkutano kwa njia ya mtandao ulioandliwa na Kamati ya Mabaraza ya aaskofu wa Umoja wa Ulaya (COMECE na Shirikisho la Vyama katoliki vya familia Ulaya (FAFCE). Tafakari yao imeangazia sehemu ya hati iliyochapishwa mnamo tarehe 3 Desemba 2020 ikiongozwa na kauli mbiu: Wazee na mustakabali wa Ulaya: mshikamano wa kizazi na huduma wakati wa mabadiliko ya ufupungufu wa idadi ya watu. Ni hati ambayo inafuatiwa kuchapishwa kwa Ripoti juu ya mabadiliko ya upungufu wa idadi ya watu na kitabu cha kijani kuhusu uzee ambacho kinatoa mwanga zaidi juu ya athari za kiuchumi na zile nyingine ambazo zinahusu  jamii inayozeeka. Makadirio ya hivi karibuni yanaoneesha kuwa katika miongo ijayo idadi ya watu wazee katika Jumuiya ya Ulaya itaongezeka: wenye zaidi ya  miaka 65 sasa ni asilimia 20% ya idadi ya watu, ambapo wataongezeka hadi asilimia 30% ifikapo 2070; watu wenye zaidi ya umri wa miaka 80 wanatarajiwa kuzidi mara mbili kwa wakati mmoja, na kuwa asilimia 13% ya idadi ya watu ifikapo mwaka 2070. Utabiri pia unaoneesha kuongezeka kwa idadi ya watu wanaoweza kuhitaji huduma ya muda mrefu ambayo itaongezeka  Ulaya kutoka watu 19.5 mnamo 2016 hadi milioni 23.6 mnamo 2030, kufikia milioni 30.5 mnamo 2050.

Katika mahojiano na Rais   Mabaraza ya Maaskofu wa Umoja wa Ulaya (COMECE) amesema: “Bila idadi ya wazee hatuwezi kudumisha ubinadamu na kwamba kudumisha ubinadamu ni jambo muhimu zaidi, pia kwa siku zijazo za Ulaya. Ni lazima tuanze kwa kuthamanisisha idadi ya wazee, kwa sababu hadi sasa uboreshaji huu haujafanywa. Mara nyingi tumewatenga katika nyumba za kustaafu, kama vile ilivyo hata kutengwa kwa watoto, kwa sababu wanahesabiwa tu wale ambao wana manufaa katika ukuaji wa uchumi na ambao uko katikati ya sera. Hii sio haki. Tunapaswa kurekebisha dhana yetu ya ukuaji wa uchumi, lazima tuingize ubinadamu katika dhana za kiuchumi. Mara nyingi mimi ninakutana na vijana, na vijana wanahitaji bibi na babu. Upendo wa wazazi daima ni upendo na mamlaka, lakini vijana wanahitaji kusikiliza bibi na babu na wakiongea na kuhisi kupendwa, kwa vizazi vyote. Ikiwa hatujali idadi ya wazee, vijana wetu hawatakuwa na maisha mazuri ya baadaye”.

Akizungumzia juu ya janga ambalo limetoa funzo kuhusu wazee na mbele ya mgogoro wa kiafya, Kardinali Jean-Claude Hollerich amesema: “Ni ngumu sana kukosoa kile kilichofanyika kwa sababu hata hivyo watu wameitikia mgogoro. Lakini sasa kwa kuwa tumeiishi kwa karibu mwaka, tunaweza kutoa tafakari. Kwa mfano, kuwatenga watu wazima ni mbaya sana. Kila mwanadamu anahitaji kukumbatiwa, maneno ya moja kwa moja, sio kwenye inteneti tu, na pia kuna watu wazee ambao mara nyingi hawajui kutumia mtandao. Leo kuna vipimo ambavyo vinatoa matokeo ya haraka sana na tunahitaji kuwa na vipimo vingi zaidi ili kuwatoa wazee kutoka kwa kutengwa kwao. Kulinda na kujitenga kulionekana kuwa vyote ni sawa, lakini sasa tunajua zaidi na tunahitaji kuwa wabunifu zaidi ili kupata njia nyingine za kulinda bila kuwatenga”.

Katika mkutano huo ameshiriki Bi. Gabriella Gambino, Katibu Msaidizi wa Baraza la Kipapa la Walei, Familia na Maisha. Katika mahojiano ameulizwa juu ya mchango wa Vatican katika mkutano huo. Hati ambayo ilijadiliwa ilikuwa inalenga hasa kwa watunga sera wa Jumuiya ya Ulaya, kwa hivyo sio maandishi tu ya kichungaji, kama yale ambayo kawaida  ya miaktaba yao hufafanua, lakini itakuwa muhimu kwa dalili kwamba Kanisa linataka kubadilishatafakari ya kisiasa kwa maana ya juu ya neno hilo, imani hiyo imepandikizwa katika utamaduni na siasa. Kwa sababu hiyo walikaribisha kwa furaha kuchapishwa kwa hati  ambayo, zaidi ya hayo, imejikita katika mafundisho jamii ya Kanisa  na kwenye mafundisho ya familia. Kwa namna ya pekee kuna jambo muhimu la swali ambalo alipendaa kushirikisha hasa la kuishi kwa muda mrefu na kwamba ni habari njema. Maisha daima ni zawadi, hatuwezi kuyachukulia kama jambo la kutisha ambalo litaweka mifumo yetu ya ustawi katika shida tangu uzee, baada ya yote, kiukweli ni kutimiza hamu ya kibinadamu ya uze ile ya kuishi kwa muda mrefu  kwa upande mwingine ni hamu ambayo kila mmoja wetu anayo kwa ajili yake mwenyewe.

Kwa upande mwingine, kinachosababisha wasiwasi ni kupungua kuzaliwa kwa watoto, hii ina maana kwamba, sio wazee ambao ni wengi sana lakini ni vijana ambao ni wachache. Uendelevu wa jamii zetu hakika unahitaji mchango mzuri kati ya idadi ya watu wenye umri wa kufanya kazi na wale ambao wameacha mzunguko wa uzalishaji, lakini tutapata suluhisho ikiwa tunaweza kuhusisha suala la kuzeeka na ile ya msimu wa baridi wa kupungua kwa idadi ya watu, kama alivyoeleza  Baba Mtakatifu Francisko katika  Waraka wa Fratelli tutti. Na hapo ndipo kuna kitovu ambacho lazima tukifanyie kazi pamoja. Akitilia mkazo juu ya Papa Francisko kuhusu umuhimu wa mshikamano wa kizazi kati ya vijana na wazee, Bi Gambino anaamini kuwa:  “vijana na wazee, wajukuu na bibi na babu  lazima wakutane. Inahitajika kwamba wapendekeze kwa vijana kwenda nje kukutana na wazee, kufungua mazungumzo na kusikiliza na kama  watu wazima ndio kwanza tunapaswa kufanya hivyo ili kutoa ushuhuda kwa maana  hii kwa watoto wetu, na lazima kupendekeza kwao wafanye kile ambacho kiukweli Baba Mtakatifu Francisko alifanya katika siku za hivi karibuni, kumtembelea Bi Edith Bruck nyumbani  kwake ili kusimulia hadithi ya maisha yake. Katika fursa hhiyo, Baba Mtakatifu alisisitiza umuhimu wa babu na bibi, kama bibi yake Rosa, alizungumza na wajukuu zao na kuwasindikiza katika safari ya maisha”.

Bi Gambino akindelea na maelezo amesema kuwa: “Kuna hadithi ambazo haziwezi kupotea, katika miezi hii wakati mawasiliano ya karibu hayawezekani ni muhimu kusisitiza kwamba uhusiano kati ya vijana na wazee haukatiki. Tunahitaji kuzungumza juu ya familia, katika familia. Kwa njia ya Makao Makuu ya Walei, Familia na Maisha,  katika mahubiri , kujikita katika kazi za kichungaji.  Kwa kupitia baraza la kipapa la Walei, Familia na Maisha kwa mfano, katika miezi ya hivi karibuni tumezindua mipango miwili ya kijamii hasa kuuliza vijana  watume kwa njia ya mtandao mikumbatio kwa wazee walio peke yao wakati huu wa janga na kukusanya maneno yao ya hekima. “Tunaanza kuandaa Siku ya Mababu na Wazee Duniani, ambayo Baba Mtakatifu ameanzisha, na mipango kadhaa ambayo tutapendekeza katika mwaka Amoris Laetitia  amabi utaunganishwa hasa na mazungumzo kati ya vizazi. Kwa uchunguzi wa karibu kila kitu tunachozungumza, ambacho ni hali ya wazee, maswala ya idadi ya  kupungua kwawatu, mazungumzo ya vizazi yote yako katika mazungumzo mapana juu ya familia na ndio sababu ninachukua fursa hii kukukumbusha kuwa Mwaka wa Familia ya Amoris laetitia  ambamo tunaweza kuwa na hali halisi ya utunzaji maalum wa kichungaji wa familia, pamoja na babu na bibi”.

03 March 2021, 18:13