A man walks his dog along the beach as the sun rises at New Brighton A man walks his dog along the beach as the sun rises at New Brighton 

Askofu Mteule Paul Siphiwo Vanga Jimbo Katoliki la Queenstown

Askofu mteule Paul Siphiwo Vanga alizaliwa tarehe 16 Juni 1955 huko Xonxa, Jimboni Queenstown. Baada ya masomo na malezi yake ya kitawa, tarehe 6 Oktoba 1985 akaweka nadhiri zake za daima na hatimaye, kupewa Daraja Takatifu ya Upadre tarehe 5 Julai 1986. Hadi kuteuliwa kwake alikuwa ni msimamizi wa Kitume Jimbo Katoliki la Queenstown, Afrika ya Kusini! Mwanzo Mpya!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amemteuwa Mheshimiwa Padre Paul Siphiwo Vanga, S.A.C, Shirika la Wapallotini, kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Queenstown, Afrika ya Kusini. Kabla ya uteuzi huu, Askofu mteule Paul Siphiwo Vanga, alikuwa ni Msimamizi wa Kitume wa Jimbo Katoliki la Queenstown. Itakumbukwa kwamba, Askofu mteule Paul Siphiwo Vanga alizaliwa tarehe 16 Juni 1955 huko Xonxa, Jimboni Queenstown. Baada ya masomo na malezi yake ya kitawa, tarehe 6 Oktoba 1985 akaweka nadhiri zake za daima na hatimaye, kupewa Daraja Takatifu ya Upadre tarehe 5 Julai 1986.

Tangu wakati huo kama Padre ametekeleza utume mbalimbali kama: Paroko-usu, Mlezi, Paroko, Mshauri na Msaidizi wa mkuu wa Shirika nchini Afrika ya Kusini. Tangu mwaka 2015 akateuliwa kuwa Msimamizi wa Kanisa kuu la “Christ the King” Jimbo Katoliki Queenstown hadi kuteuliwa kwake kuwa Askofu. Kuanzia mwaka 2011 hadi 2019 aliteuliwa kuwa Makamu Askofu na kuanzia mwaka 2019 hadi kuteuliwa kwake, aliteuliwa kuwa ni Msimamizi wa Kitume Jimbo Katoliki la Queenstown.

Queenstown
13 March 2021, 14:49