MIAKA 90 YA KUZALIWA UTUME WA UTANGAZAJI WA RADIO VATICAN MIAKA 90 YA KUZALIWA UTUME WA UTANGAZAJI WA RADIO VATICAN 

Miaka 90 ya Radio Vatican:Ruffini anasema Radio haina haraka inahitaji umakini!

Katika maadhimisho ya Radio Vatican ya kutimiza miaka 90 ya utangazaji habari ulimwenguni,Rais wa Baraza la kipapa la Mawasiliano anakumbusha asili na utambulisho wa sauti ya Papa kwa ajili ya ulimwengu.Ni mchakato mrefu ambao karibu kwa karne umefungamanisha na watangazaji wengine wa kimataifa kwa maonoya siku zijazo kama alivyoeleza hata Ghisani,Mwakilishi wa masuala ya Sheria wa Radio ya Vatican na mjumbe wa Bodi ya Utendaji ya Umoja wa Utangazaji Ulaya.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Ni nguvu ya upole wa neno lililonenwa na kusikilizwa ambalo linaipatia Radio Vatican, miaka 90 tangu kuanzishwa kwake katika utume huo na matarajio ya siku zijazo za umisionari. Amekumbusha hayo katika taarifa ya maadhimisho ya sauti ya Papa kwa ulimwengu wote Rais wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano  Bwana Paolo Ruffini. Uzuri wa Radio ni kwamba inaingia kwa kina kwa sababu unasikia sauti. Unazingatia sauti hiyo. Radio haina haraka. Inaomba umakini. Na baada ya karibu karne moja, radio iliyoanzishwa na Papa  Pius XI iliyopangwa  na kujengwa na Guglielmo Marconi, inabaki kuendelea kuwa na maono ya siku zijazo, ikihifadhi asili yake na utambulisho. Katika DNA yake, Kwa mujibu wa Bwana Ruffini, kuna huduma kwa Kanisa, kwa Papa na kwa ajili ya mwanadamu mahali popote alipo, kwa dini yoyote au utamaduni wowote na maana ya historia ambayo imeenea karibu karne yote ya ishirini, ambayo ilivumilia ufashisti na ukomunisti, ambayo ilishinda Vita vya II vya Dunia na vita baridi. Ni mzizi wenye nguvu, ambao ni mti huo wa Habari za Vatican unazidi  kukua tovuti yake  ambayo inasimulia historia za Kanisa na mafundisho ya Papa katika lugha 43, na ambayo mnamo 2020 ilikuwa na kurasa milioni 250 zilizosomwa ulimwenguni kote, amebainisha.

Ushirikiano na radio nyingine ulimwenguni

Radio Vatican pia imejumuishwa kikamilifu katika jumuiya ya kimataifa ya watangazaji wa radio za umma na huduma ya runinga, hasa katika Umoja wa utangazaji Ulaya ambayo ni mwanachama mwanzilishi, na Umoja wa Utangazaji Afrika, kwa mujibu wa maelezo ya Giacomo Ghisani, Mwakilishi wa  masuala ya Sheria ya Radio ya Vatican na mjumbe wa Bodi ya Utendaji ya Umoja wa Utangazaji ya Ulaya. Ushiriki katika jumuiya hizi za kimataifa za utangazaji, ambayo ni sehemu ya utume wa Radio ya Papa ambayo, katika huduma yake ya msaada ya Utume wa wa Petro na kiunganishi kati ya kitovu cha ukatoliki na nchi tofauti ulimwenguni, kina fungamanisha, kinashirikisha na kinajadili na watangazaji wa nchi nyingine juu ya mantiki kuu na maadili ambayo huhamasisha shughuli zake, kwa mtazamo wa kutoa habari sahihi kwa huduma wema wa wote. Kwa mujibu wa Bwana Ghisani amesema “Mtandao huu mkubwa wa uhusiano pia unaoneshwa kupitia uhusiano wa ushirikiano ambao Radio Vatican inadumisha na radio nyingi, Katoliki na zisizo  Katoliki, mikoa na wilaya pia tovuti ambazo zinahamisha programu za lugha ya Mtangazaji  na hivyo kuiruhusu ifikie mbali zaidi ukweli kwa ufanisi zaidi

Kuanzishwa kwa Webradio tarehe 12  Februari

 Muungano kati ya tovuti na radio ni hatua inayofuata kuelekea siku zijazo. Kiukweli, safari ya radio ya tovuti inaanza tarehe 12 Februari (https://www.vaticannews.va/it/epg.html). Kwa maana hiyo tunaweza kusema kwamba kandanda ya kwanza itakuwa kwa lugha ya Kiitaliano, Kifaransa, Kiingereza, Kihispania, Kireno, Kijerumani na Kiarmenia. Kwa mwaka huu karibu programu 30 ya moja kwa moja zitaundwa sawa na lugha nyingi ambazo zinaweza kusikilizwa wote kwenye tovuti ya redio na kupitia Programu ya sasa ya Radio Vatican. Kwa mujibu wa Rais wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano Bwana Ruffini ameeleza kuwa hii ni aina ya matumizi ambayo, yatamruhusu mtu yeyote ulimwenguni, kupitia simu yake ya smartphone au kompyuta yake, kusikiliza radio Vatican kwa lugha yake. Kila lugha  na radio, ratiba, ni dhamana ambayo inaimarishwa na wasikilizaji. Ikumbukwe kwamba Radio Vatican, leo hii inatangazwa kupitia satelaiti, DAB +, ulimwengu wa kidigitali, mtandao wa inteneti na masafa ya Hertzian. Hatupaswi kusahau kwamba ni masafa  mafupi yanayo jumuisha kile ambacho Baba Mtakatifu Francisko anaomba sana ili kufikia pembezoni mwa ulimwengu.

 

10 February 2021, 16:27