Umakini unahitajika katika mgogoro wa kiafya dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona Umakini unahitajika katika mgogoro wa kiafya dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona 

Ask.Mkuu Jurkovič:Msidharau athari mbaya za kusambaa kwa janga!

Kuwa na mazungumzo ya dhati ni kama zana kwa ajili ya matokeo chanya ya ulimwengu ndiyo ushauri wa Mwakilishi wa Kudumu wa Vatican katika Ofisi za Umoja wa Mataifa huko Gineva Uswiss wakati wa kikao kuhusu Majadiliano ya Kidini kwa kuongozwa na mada “nafasi ya dini katika kipindi cha virusi vya corona.

Na Sr. Agela Rwezaula- Vatican.

Katika hotuba ya Askofu Mkuu Ivan Jurkovič, Mwakilishi wa Kudumu wa Vatican katika Ofisi za Umoja wa mataifa huko Geneva, amejikita kufafanua kwamba lazima kuwa makini kuhusu athari za kusambaa kwa janga. Ni katika kikao hicho kilicho fanyika tarehe 25 Februari 2021, kwa kuongozwa na mada "nafasi ya dini katika kipindi cha virusi vya corona".  Kiongozi huyo alianza kwa kuwashukuru watu wengine mashuhuri waliokuwepo kwenye mkutano huo, huku  akisisitiza imani ya pamoja  iliyowasababisha kushiriki, kwamba Kila mmoja anajua, kutokana na uzoefu wa kibinafsi, dhamana na umuhimu wa dini yao katika maisha ya kila mmoja. Mkutano huu wa kila mwaka unaruhusu kushiriki kile kilicho muhimu zaidi kwao kwa roho ya uaminifu na udugu, ili kuweza kujifunza kutoka kwa kila mmoja, kusaidiana na kukua pamoja kwa kuheshimiana .

Moja kwa moja akianza kujikita na mada  ya mkutano huo, amebainisha jinsi ambavyo wote wanajua janga la virusi vya corona limekuwa baya sana na ​​inashangaza kutafakari juu ya ukweli kwamba zaidi ya mwaka mmoja uliopita hakuna mtu aliyejua juu ya ugonjwa huu ungeweza kushtua ulimwengu mzima. Kila hali ya maisha yetu imesumbuka: mamia ya maelfu ya watu wamekufa; isitoshe wengine wanakabiliwa na shida mbaya  za kiafya; biashara nyingi zimefungwa ulimwenguni kote, ambazo zingine hazitaweza kufunguliwa tena; uchumi wa kitaifa umeharibiwa; uzalishaji umesimamishwa; katika maeneo mengi, elimu imepunguzwa kwa ujifunzaji kawaida au imesimama kabisa na hali za umaskini zimesukumwa kufikia hatua ya kuvunja fola. Kiongozi huyo aidha  hakusahau hata matokeo mengine ya janga, yasiyoweza kulinganishwa lakini yenye madhara sawa:"Athari za kusumbua zaidi za virusi ni mizozo ya ndani ya hila. Matokeo ya  kiafya ambayo yamejionesha katika a ulimwenguni  huu ni mabaya sana hasa ambauyo yanahitaji  kuhakikisha mazingira salama kwa wote, hata hivyo kutengwa katika nyumba, na vile vile kuvaa vibarakoa, kuteseka kazini pamoja na kutoweza kushirikiana na familia na marafiki imekuwa na inaendelea kuwa na athari kubwa ya kisaikolojia , kihemko na kiroho kwa kila mmoja wetu.

Kwa mtazamo wa Kikristo, kanuni msingi ya kale ya Aristoteli ambayo inataka mwanadamu kama kiumbe wa kijamii inachukua maana zaidi, kulingana na Mwakilishi wa kudumu, Mungu anataka muungano. Mwenyezi ameumba sisi wanadamu ili tuweze kuwa na uhusiano wa kina na wa maana na Muumba wetu na sisi kwa sisi. Ni kwa njia ya muungano  huo wa pamoja na wa wazi tutapata utimilifu wa kweli na amani ya kweli ”. Janga la Covid-19, hata hivyo, kulingana na tafakari ya askofu mkuu, limezidisha mivutano iliyopo na kuongeza vitisho dhidi ya umoja kati ya watu, tamaduni na mataifa, kuongezeka ukosefu wa usawa. Wakati rasilimali na huduma ya matibabu ni dogo, inaeleweka kuwa kila mtu na kila taifa linajaribu kupata na kukusanya kile wanachoweza kwa wapendwa wao, amesema Askofu Mkuu na kuongeza  kwamba hata hivyo, njia hii ya ubinafsi ni tofauti kabisa na umoja. Ni muungano ambao kweli huleta utimilifu kwa moyo wa mwanadamu.

Askofu Mkuu Jurkovič aidha  amesema imani inatufundisha si kujitazama sisi wenyewe tu na mahitaji yetu ya haraka, lakini  kwa  bahati mbaya sehemu kubwa ya  tamadunu ya imani imejionesha kuwa na  upendo wa kujitoa, bila kuwa na uwajibikaji wa kusaidia ndugu kaka na dada. Papa Francisko na mwakilishi wa kudumu wanapenda sana kuhakikisha kuwa janga la Virusi vya corona visilete matokeo hayo ya  kuzorota kwa mwingiliano halisi wa kibinadamu. Kwa maana hiyo iliundwa Tume ya dharura ndani ya Makao makuu ya Baraza la Kipapa la Maendeleo Fungamani  ya Binadamu, kwa lengo la kukuza utunzaji halisi na kamili kwa wale wote walioathiriwa na janga la sasa, na zaidi  ilitiwa saini hasa kabla ya janga hilo Hati kuhusu Udugu wa Binadamu wa Amani na urafiki kijamii na Papa Francisko na Sheikh Ahmed el-Tayeb, Imam  Mkuu wa Al Azhar, mnamo tarehe 4 Februari 2019.

Kuna  umuhimu wa udugu  wa kibinadamu na jukumu la tamaduni za kidini katika kuhamasisha ambayo ni kiini cha  Waraka wa hivi karibuni ya Papa Francisko wa "Fratelli tutti ", yaani "Wote ni ndugu". Katika waraka huu, Papa anasisitiza kwamba dini mbali mbali, kwa msingi wa heshima yao kwa kila mwanadamu kama kiumbe aliyeitwa kuwa mwana wa Mungu, zinachangia kwa kiasi kikubwa kujenga udugu na kutetea haki katika jamii, amesisitiza Mwakilishi wa Vatican.

26 February 2021, 14:07