RV miaka ya 30, Radio Vatican RV miaka ya 30, Radio Vatican  Tahariri

Miaka 90 ya Radio Vatican&sababu za utume wake

Ni katika huduma ya Papa na ya udugu kati ya watu.Kwa njia hiyo utangazaji kwa utashi wa Papa Pio XI umefikiriwa kwa mara nyingine tena wakati wa janga.

Na Andrea Tornielli

Radio Vatican, iliyoanzishwa kwa hekima ya kuona upeo mbali, iko katika huduma ya mawazo na sauti ya Papa, ili kueneza mwangwi wake kwa kasi na ufanisi kwa wakati; na ni uthibitisho fasaha wa uhuru wa Makao makuu ya Kitume, chombo cha kusambaza mafundisho ya kipapa. Tangu mwanzo, tunda hili la teknolojia ya kisasa pia lilikuwa katika huduma ya umoja kati ya watu, kwa maana ya udugu wa ulimwengu. Hayo ni maneno yaliyosemwa mnamo tarehe 12 Februari 1961 na Mtakatifu Yohane  XXIII ambayo yanaweka umuhimu wake  katika siku ambazo Radio Vatican inasherehekea miaka yake tisini na Kanisa linafafanua katika ujumbe wa Waraka wa Papa  wa ‘Fratelli tutti’.

Siku hii maalum ya kuzaliwa kwa utangazaji kwa utashi wa Papa Pio XI, na ambao uliendelezwa na Guglielmo Marconi na kukabidhiwa kwa Mapadre wa Kijesuit, unajikuta kwa sasa katika wakati mgumu wa historia ya ubinadamu kwa sababu ya janga. Vita dhidi ya virusi vya corona inayoambukiza mapafu, na virusi vya kutokujali ambavyo mara nyingi vinatuzuia kujitambua kama ndugu, vimefafanua kwa upya mipango, ratiba na maana ya utume. Katika mwaka wa Covid-19, utangazaji wa Papa umejaribu kuunda mtandao na kuunganisha watu waliotengwa wakiwa karantini. Umesimulia juu ya uzoefu wa wema na wingi wa ubunifu ulioibuka ulimwenguni.

Kuna tukio ambalo zaidi ya wakati mwingine wowote limeonekana katika historia ya Radio Vatican, mwaka uliopita. Huu ni ushuhuda wa Padre Luigi Maccalli, aliyekuwa amefungwa na wanajihadi kati ya Niger na Mali kwa miaka miwili. Mmisionari huyo alikuwa amepata radio kutoka kwa waliomfunga. Kwa maelezo yake anasema: “Niliweza kusikiliza tafakari juu ya Injili ya Jumapili kutoka Radio Vatican kila Jumamosi. Mara moja hata Misa ya moja kwa moja… ilikuwa hasa Misa ya Papa ya Pentekoste mwaka 2020”

Kwa maneno hayotunapata sababu zahuduma inayotolewa na mtangazaji, mafundi wake na wahariri wake kutoka nchi 69 mbali mbali  ambao kila siku hupeleka ujumbe wa Mfuasi  wa Petro na historia za maisha ya Kanisa ulimwenguni, kuingia katika lugha tofauti na tamaduni tofauti, bila tamaa ya watazamaji, napenda (like) au mhusika anayejitegemea. Hatari ambazo Baba Mtakatifu Francisko alikuwa ameonya mnamo Septemba 2019, wakati akikutana na wafanyakazi wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano: “Je! Mawasiliano yanapaswa kuwaje? Moja ya mambo ambayo hampaswi kufanya ni kujitangaza ... Hampaswi kufanya kama wafanyavyo makampuni ya biashara ambayo hujaribu kujitangaza ili wapate watu wengi ... Ninapendelea mawasiliano yetu yawe ya Kikristo na sio sababu ya kugeuza propaganda”. Kufuatana maelekezo hayo, Radio Vatican inaendelea kupelekea ujumbe wa Papa kwa mababa wengi kama vile Padre Maccalli ambao katika pembe zilizo mbali zaidi za dunia wanathubuti maisha yao kwa ajili ya Injili. Na inasimulia katika ulimwengu, ikitoa umakini kwa kila mtu, na historia zao.

11 February 2021, 18:44