27 Februari ni kumbu kumbu ya Mtakatifu Gregori wa Narek 27 Februari ni kumbu kumbu ya Mtakatifu Gregori wa Narek 

Kumbu kumbu ya kwanza ya Mtakatifu Gregori wa Narek

Jumamosi tarehe 27 Februari imeadhimisha kumbu kumbu ya kwanza kiliturujia ya mtakatiu Gregory wa Nareki,Abati na mwalimu wa Kanisa.Kardinali Sandri katika mahubiri amesema”Kusherehekea kumbukumbu ya kiliturujia ya Mtakatifu inatoa chachu na kuwafanya wawe na utulivu, kama Waarmenia na kama waamini wa Yesu,katika ushuhuda wake na ambao anawauliza kama wanataka kuwa wakristo wa jina tu au kwa tamaduni za zamani.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Kwa mujibu wa Kalenda ya Kanisa ya Kirumi, baada ya Kuchapishwa kwa Hati ya Papa Francisko kuhusu kuwekwa rasimi kila tarehe 27  Februari,  kuwa ya  kumbu kumbu ya kiliturujia ya Mtakatifu Gregori wa  Narek, Abati na Mwalimu wa Kanisa, Baraza la Kipapa kwa ajili ya Makanisa ya Mashariki na Baraza la  Kipapa la kuhamasisha Umoja wa Kikristo, wameandaa maadhimisho mjini Vatican  Jumamosi tarehe 27 Februari  2021, kwa ushirikiano na Ubalozi wa Jamhuri ya Armenia jijini Vatican. Maadhimisho ya misa takatifu yameongozwa na Kardinali Leonardo Sandri, Rais wa Baraza la Kipapa la Makanisa ya Mashariki, katika Kanisa kuu la Mtakatifu Petro na badaye yamefuata  sala ya kiekumene mbele ya sanamu ya Mtakatifu Gregori wa Narek iliyobarikiwa na Papa Francisko mnamo 2018, katika bustani za Vatican. Pamoja na Kardinali Sandri wameshiriki misa hiyo, Askofu mkuu Lévon Bogos Zékyian, wa  Istanbul ya Kiarmenia na Mwakilishi wa Kipapa wa Shirika la Kiarmenia pamoja na Askofu Mkuu Brian Farrell, Katibu wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Umoja wa Kikrsito. Katika Sala ya kikumene imeongozwa na Khajag Ian,  ambaye ni Mwakilishi wa Kanisa la kitume la Kiarmenia, Roma  kwa uwepo wa Kardinali Kurt Koch, Rais wa Baraza la Kipapa la Uhamasishaji wa Umoja wa Kikristo.

Kard.Sandri:thamani za utamaduni na ukaribu wa Kanisa la kiarmene a katoliki

Karibu baada ya miaka sita tangu kufanyika sherehe isiyosahaulika iliyoongozwa na Baba Mtakatifu Francisko mnamo tarehe 12 Aprili 2015, katika Kanisa kuu la Mtakatifu Petro, Vaticaan imesikika tena kuimbwa nyimbo za thamani za utamaduni wa Kiarmenia. Ndiyo alivyoanza Kardinali Leonardo Sandri, katika mahubiri yake, akikumbuka nyakati nyingi ambazo zimekuwa na ukaribu kati ya Makanisa hayo mawili Katoliki na Waarmenia. Kwa namna ya pekee  amekumbusha  ziara ya Baba Mtakatifu Francisko nchini Armenia mnamo 2016. Kardinali amechukua fursa hii ya kuwaalika kusali  kwa ajili ya Papa katika ziara  yake ya kitume nchini Iraq inayotarajiwa kuanza tarehe 5 hadi 8 Machi 2021. Kardinali amesema, Papa ambaye mara kwa mara anaomba kwa ajili ya kusitisha 'vita vya ulimwengu vilivyoganyika vipande vipande' na ambaye alioneesha Mtakatifu Gregori wa Narek kama nyota katika anga la madaktari, anaruka kwenda  katika nchi ambazo pamoja na Siria, licha ya mateso, wanaomba  kwa Mtakatifu Ephrem kama baba na kutoa msukumo kwenye njia panda ya historia, mateso, utakatifu na hekima.

Wakristo wasiwe wa jina na tamaduni za kijazamani bali wawe wanafunzi wa Bwana

Kusherehekea kumbukumbu ya kiliturujia ya Mtakatifu Gregori wa Narek, inatoa chachu na kuwafanya wawe na  utulivu, kama Waarmenia na kama waamini wa Yesu, “katika ushuhuda wake kwa hakika  mtakatifu huyo anauliza  ikiwa wanataka kuwa Wakristo kwa jina tu au kwa tamaduni za zamani, au kwanini wanataka kuwa wanafunzi wa Bwana leo hii, kama alivyofanya, kuwa mwalimu wa hekima na mafundisho, amesisitiza Kardinali Sandri. Na amenukuu maneno kadhaa ya Mtakatifu aliyeandika wakati wa siku za ugonjwa wake: “nikiwa nimelala na uhalifu wangu, juu ya kitanda cha magonjwa yangu na kinyesi cha dhambi zangu, mimi si kitu zaidi ya maiti aliye hai, mtu aliyekufa na ambaye bado anazungumza. [...] Basi, kama kijana uliyemwita maishani ili kutuliza maumivu ya mama yake, Unanirudishie roho yangu yenye dhambi iliyosasishwa kama yako. ” Mtakatifu Gregori wa Narek, amethibitisha Kardinali Sandri kuwa anaendelea kufundisha kwamba hekima ya kweli ni ile ya wanafunzi waliobaki, kujua jinsi ya kuishi na Yesu na kila wakati wa historia.  Mahubiri yake yamehitimishwa kwa kutoa mwaliko wa matumaini: “kuombea Armenia katika siku hizi za machafuko na dhiki na kwa wote kupitia  Maria Mama Mtakatifu wa Mungu pamoja na Mtakatifu Gregori wa Narek ambaye alimwomba hivi:"Mama wa jengo lisiloharibika na Kanisa”.

Sura ya Mtakatifu  Gregori na ujumbe wake

Katika kuelewa  vizuri sura ya Mtakatifu Gregori wa Narek, kuna  Kitabu cha Maombolezo, kilichoandikwa na yeye wakati wa  juhudi kubwa ya uchungu wa ugonjwa kwamba ni jiwe la kumbukumbu ya  fasihi ya Kiarmenia ambayo  mvutano upo, hata mkubwa, kati ya ufahamu wa dhambi na sherehe ya  huruma  kama mchango wa sifa na tukufu zaidi kwa Mungu, ambaye ni huruma. Ni mtu ambaye kwa mana hiyo alitoa sauti ya kilio cha ubinadamu, mateso na dhambi, lakini akiangazwa na uzuri wa upendo wa Mungu.

27 February 2021, 17:29