Kardinali Mauro Gambetti ameteuliwa na Papa Francisko kuwa Mhudumu Mkuu wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican na Rais wa Kiwanda cha Mtakatifu Petro. Kardinali Mauro Gambetti ameteuliwa na Papa Francisko kuwa Mhudumu Mkuu wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican na Rais wa Kiwanda cha Mtakatifu Petro. 

Kardinali M. Gambetti Mhudumu Mkuu Kanisa Kuu la Mt. Petro!

Kardinali Mauro Gambetti alizaliwa tarehe 27 Oktoba 1965 huko Castel San Pietro Terme, Bologna, Italia. Baada ya majiundo yake ya kitawa, tarehe 20 Septemba 1998 akaweka nadhiri za daima kwenye Shirika la Wafrancisko Wakonventuali. Tarehe 8 Januari 2000 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Tarehe 22 Novemba 2020 akawekwa wakfu kuwa Askofu na 28 Novemba 2020 Kardinali.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko ameridhia ombi lililowasilishwa kwake na Kardinali Angelo Comastri, Mhudumu mkuu wa Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican la kutaka kung’atuka kutoka madarakani. Wakati huo huo, Baba Mtakatifu amemteua Kardinali Mauro Gambetti, O.F.M, CONV., kuwa Mhudumu mkuu wa Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican. Itakumbukwa kwamba, Shirika la Ndugu Wadogo Wafrancisko Wakapuchini lilianzishwa rasmi mnamo mwaka 1528. Hili ni tawi mojawapo la familia tatu za Shirika la kwanza la Mtakatifu Francisko wa Assisi yaani: Wafrancisko Wakapuchini, OFM Cap, Wafrancisko Wakonventuali, OFM Cov., na Wafrancisko, OFM.

Kumbe, Kardinali Mauro Gambetti ni kutoka Shirika la Wafranciskani Wakonvetuali, aliyezaliwa tarehe 27 Oktoba 1965 huko Castel San Pietro Terme, Bologna, Italia. Baada ya majiundo yake ya kitawa, tarehe 20 Septemba 1998 akaweka nadhiri za daima kwenye Shirika la Wafrancisko Wakonventuali. Tarehe 8 Januari 2000 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Tangu wakati huo ametekeleza utume wake kama mkurugenzi wa miito Kanda ya Emilia-Romagna. Mwaka 2009 alichaguliwa kuwa Mkuu wa Kanda ya Wafranciskani Wakonvetuali wa Mtakatifu Anthony wa Padua hadi tarehe 22 Februari 2013 alipong’atuka kutoka madarakani. Kati ya mwaka 2013 hadi mwaka 2017 aliteuliwa na Mkuu wa Shirika kuwa Mlinzi Mkuu wa Kaburi la Mtakatifu Francisko wa Assisi.

Mwaka 2017 alichaguliwa kuwa Rais wa Wakuu wa Kanda za Wafrancisko Wakonventuali, OFM Cov kuzunguka Bahari ya Mediterrania na utume huu, umalizika mwezi Septemba 2017. Kati ya Mwaka 2017 hadi tarehe 31 Oktoba 2020 alikuwa ni Mlinzi mkuu wa Kaburi la Mtakatifu Francisko wa Assisi. Tarehe 13 Oktoba 2020 Baba Mtakatifu Francisko akamteuwa kuwa Askofu na kuwekwa wakfu tarehe 22 Novemba 2020 na Kardinali Agostino Vallini. Baba Mtakatifu Francisko akamteuwa na kumsimika kuwa Kardinali tarehe 28 Novemba 2020. Na hatimaye, Tarehe 20 Februari 2021 Baba Mtakatifu Francisko amemteuwa kuwa Mhudumu mkuu wa Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican na Rais wa Kiwanda cha Mtakatifu Petro.

Kanisa Kuu

 

22 February 2021, 13:34