Tafuta

Ziara ya Kipapa nchini Iraq kuanzia tarehe 5-8 Machi 2021 Ziara ya Kipapa nchini Iraq kuanzia tarehe 5-8 Machi 2021 

HIJA YA KITUME YA PAPA FRANCISKO IRAQ:Tumaini la Askofu Mkuu Warda

Askofu Mkuu wa Erbil ameelezea matumaini yake ya kufika kwa Papa Francisko katika Nchi yake Iraq kwamba kwa kufanya mikutano na hotuba zake zitachangia juhudi kwa viongozi wenye mamlaka na ufahamu zaidi wa uwepo wa wakristo nchini Iraq ulivyo wa asili na wala si wageni.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Askofu Mkuu Bashar Warda, Kikaldayo huko Erbil  akisungumza na Shirika la Kipapa la Kanisa Hitaji (ACS) kuhusu ziara ya  kitume nchini Iraq ya Papa Francisko iliyopangwa kuanzia tarehe 5 hadi 8 Machi 2021 amelezea matumaini ya kwamba taifa zima litahasisha maono ya umma kuhusu umwep wa Wakristo nchi humo. Heshima ya watu wa Iraq kwa  upande wa Jumuiya  ya Kikristo amesema itakua. Watu nchini Iraq wanajua kitu kidogo juu yao. Kwa maana hiyo ni matumaini kwamba wengi watatambua jinis ambavyo wao sio  wageni bali ni wenyeji wa asili wa nchi hiyo. Askofu Mkuu Warda pia amesisitiza umuhimu wa mkutano wa Papa  Francisko na kiongozi wa Washia, Ayatollah Ali Al Sistani, uliopangwa kufanyika tarehe 6 Machi. Nchini Iraq kuna  Washia wengi. Na Al Sistani anachukuliwa kuwa ni mtu wa amani ambaye analaani  ufisadi uliokithiri wa taifa kwa mujibu wa askofu mkuu wa Kikaldayo wa Erbil. Mkutano kati ya sura  hizi mbili kwa hakika utakuwa na matokeo nzuri katika wazo kwamba Washia wanao uelewani na Wakristo ".

Kwa mujibu wa Askofu Mkuu Warda hakuficha ugumu wa ziara hiyo Shirika hili  ACS ambapo linaripoti kuwa  dini fulani la kihitikadi linaendelea kuwa na  mtazamo wa uadui kwenye mitandao ya  kijamii kuhusu safari ya Papa, na kwamba kitu chochote kinachokuja kutoka Magharibi kinachukuliwa kama vita na  kwa watu hawa wanafikiria  Papa ndiye mfalme wa wanajeshi wa Kikristo ambao hufika  nchini kama wamisionari. Kwa upande mwingine, lakini vijana wa Iraq, wana maoni tofauti juu ya Papa Fransisko, kwa sababu, wamegundua ni mara ngapi na kwa huruma gani Papa amezungumzia juu ya hali ya Siria na Iraq, amebainisha kiongozi huyo wa kikaldayo.

Baada ya kushindwa kijeshi kwa serikali  linalojiita la Kiislamu, kwa msaada wa wafadhili wa Shirika la Kipapa la Kanisa hitaji, makumi ya maelfu ya Wakristo wamerudi makwao, ambao walikuwa wameondoka mnamo 2014 kwa sababu ya uchokozi wa wanajihadi. Shirika hili (ACS) liliunga mkono Wakristo waliochache wakati wa uhamisho na katika awamu ya ujenzi wa nyumba kwa ufadhili wa zaidi ya euro milioni 48. Askofu Mkuu  Warda anasema kwamba Wakristo wangependa Papa atembelee idadi kubwa ya maeneo, lakini hata hivyo wanaelewa shida zinazohusiana na janga lilopo la sasa.

Idadi ya maambukizo, kwa sasa kiukweli imeongezeka tena, huko Baghdad na Erbil, na kwa sababu hiiyo katika Misa kwenye  uwanja wa Erbil , wakati ambapo sanamu ya Bikira wa Karemlesh iliyoharibiwa na magaidi itarudishwa tena watashiriki watu elfu 10, tu  ingawa kuna uwezo wa kuingia  watu elfu 30. Hatimaye  kuhusu ushirikiano wa maafisa wa eneo lenye uhuru la Kikurdi kwa ajili ya ujio wa Papa Fransisko, kiongozi huyo amethibitisha kwamba mamlaka hizi zinashughulikia usalama wa Papa kwa umakini sana, kupitia kwa wafanyakazi elfu 10 wa usalama na ameaarifu kwamba vyombo vya habari vitatangaza tukio hili kwa ufafanuzi wa hali ya juu.

26 February 2021, 13:53