Kampeni ya Chanjo dhidi ya virusi vya Corona au Covd-19 Kampeni ya Chanjo dhidi ya virusi vya Corona au Covd-19 

Covid-19:Caritas Internationalis,yaangazia janga katika nchi za kusini mwa dunia!

Kuzuia janga la Covid lisiponyokee mikononi mwa nchi za Kusini mwa ulimwenguni,kuzingatia tena deni na suala la hati miliki kwa nchi hizo ndiyo wito Caritas Internationalis na Baraza la Kipapa la Maendeleo Fungamani ya Binadamu katika muktadha wa kampeni ya chanjo ulimwenguni.

Na Sr. Angela Rwezaula -Vatican.

Mgogoro wa sasa wa chanjo lazima ufikiriwe katika muktadha mpana wa hali halisi ya kiafya ulimwengunu. Ndiyo mapendekezo ya Caritas Internationalis, wakati wa kuzungumzia juu ya masuala ya chanjo na kwamba kama ilivyo mataifa mengine yanayoendelea wanakosa bado miundo ya kitibabu msingi na zana za kuweza kihifadhi chanjo. Na zaidi watu ambao wanaishi katika maeneo ya vijiji vya mbali ambao hawakuhamasishwa na wakati huo huo wako hatari ya kupata maambukizi mengine ya magonjwa. Katika muktadha huo Jumuiya ya kimataifa inapaswa kuwa na njia kamili na ya pande zote ili kuepusha hatari kwamba janga hilo linaweza kuponyoka mikononi mwa kusini mwa dunia  ambapo inaweza kusababisha mgogoro wa kibinadamu ulimwenguni.

Deni la nchi zenye kipato cha chini zinapaswa kuzingatiwa tena, caritas inapendekezo: “Msamaha wa deni unaweza kuwa njia ya kutengeneza mfuko wa pesa kwa wahusika tofauti, hasa mashirika ya kidini, ili kuboresha huduma za matibabu na vifaa katika nchi hizi. Pesa ambazo zinatakiwa kulipa deni la nchi maskini zinaweza kutumika katika kuimarisha usalama wa afya. Suala la hati miliki ya chanjo lazima pia lizingatiwe haraka ili kutambua vituo vya uzalishaji vilivyoko Afrika, Amerika Kusini na Asia na kuharakisha upatikanaji wa chanjo kabla ya kuchelewa. Kwa njia hiyo hitaji la kuwashirikisha wahusika wa ndani, hasa mashirika ya kidini kwa sababu wana miundo msingi na mawasiliano muhimu na watu walio katika mazingira magumu kama wahamiaji, wakimbizi wa ndani na waliotengwa.

Kwa mtazamo wa watoa maamuzi na Umoja wa Mataifa, Caritas Internationalis inaomba hatua madhubuti: Iitishe mkutano wa Baraza la Usalama ili kushughulikia suala la upatikanaji wa chanjo kama shida ya usalama wa ulimwengu na maamuzi thabiti ya kisiasa kulingana na pande nyingi; kutoa msamaha wa deni kwa nchi maskini haraka iwezekanavyo na kutumia pesa zilizopatikana ili kuimarisha mifumo ya matibabu na afya ya nchi hizi; kuhamasisha uzalishaji wa ndani wa chanjo katika nyanja msingi za kiufundi barani Afrika, Amerika Kusini na Asia na kuzifanya zipatikane katika miezi sita ijayo kwa kushughulikia suala la hati miliki na ushirikiano wa kiufundi na mataifa maskini zaidi; kupeana msaada wa kifedha na kiufundi kwa asasi za kijamii, na kwa mashirika ya kidini hasa, kuhakikisha maandalizi ya mwamko wa jamii na maendeleo ya uwezo wa kuwaandaa kupata huduma ya kinga ”.

 

07 February 2021, 15:28