Pope Francisko na Patriaki Sako Pope Francisko na Patriaki Sako  

Iraq,Sako:Papa ataleta ujumbe wa matumaini tunayotarajia!

Patriaki wa Wakaldayo,Kardinali Sako analaani vikali shumbulio la hivi karibu la kigaidi ambalo lilisababisha vifo na majeruhi kadhaa wasio na hatia.Alitoa wito kwa sera za kisiasa hasa kuwajibika na kufanya kazi kufikia amani,usalama na maisha ya hadhi kwa raia wake.Katika mahojiano na Vatican News ameelezea juu ya ongezeko la mivutano na hali halisi ya wakristo wakati huu wa maandalizi ya ziara ya Papa.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Hivi karibuni nchini Iraq kumetokea shambulizi la kigaidi ambalo limesasababisha vifo na majeruhi kadhaa. Katika taarifa yake Patriaki nchini Humo Kardinali  Louis Raphaël Sako alikuwa ametoa wito kuwa “baada ya miaka 18 ya mizozo na mateso, ni wakati wa Wairaq kujipatanisha na kutembea katika kuifufua nchi hiyo ikiachilia mbali na mivuta ya kisiasa na ya vyama, udini na upendeleo. Ni wakati mgumu na mzuri, kila mwiraq anaalikwa leo kugeuza ukurasa na kuchangia kwa shauku katika ujenzi wa nchi yenye afya na nguvu, kujenga jamii yetu na utamaduni wa uraia, uvumilivu, utofauti, kuheshimu sheria na heshima ya Serikali”.

Kardinali katika kujibu swali jinsi wanavyoishi kwa sasa mara baada ya tukio hilo mwisho na mivutano amekiri jinis walivyo na wasi wasi hata huzuni kwa upande wa watu. Hawa waliua watu wengi wasio na hatia, ambao kweli ni maskini. Kwa bahati mbaya machambulizi haya yana lengo la kisiasa na yanatoa ujumbe kwa serikali hata kwa rais mpya wa Marekani. Wakati huo huo, serikali imechukua hatua. Kardinali Sako, aidha mesema liha ya wakati mgumu huo raia wanaendelea kuwa na matumaini, na wanaomba kila siku ni lini amani itakuwapo, ulinzi wa hadhi ya binaamu, hata kama karibu kwa miaka 20 bado wako katika hali hii na ya kuchanganyikiwa. Kwa maana hiyo inahitaji muda. Japokuwa kabla ya muda inahitajika mapenzi mema kwa upande wa será za kisiasa. Ikiwa hakuna hilo, hakuna amani. Wanamgambo lazima pia watii serikali ya Iraq na serikali lazima ilazimishe kuondolewa kwa silaha. Kila kitu lazima kiwe mikononi mwa serikali na sio vyama vya siasa, amesisitiza Kardinali Sako.

Kwa upande wa kuanzisha sala na kufunga kwa siku tatu kama ilivyo oombwa kwa wakristo wote wanavyoishi Kardinali amesema kuwa dhidi yao  hadi sasa hakuna kitu, na hii imekuwa kwa miaka kadhaa. Lakini wao ni sehemu ya Iraq, hawaishi peke yao, bali wako na kila mtu. Maumivu yao ni ya kila mmoja. Kwa njia hiyo wao ni ndugu na dada wa familia kubwa inayoitwa Iraq. Pamoja na siku tatu za maombi wanataka kusema kwamba wote ni watoto wa Mungu, Mungu wa wanadamu wote. Ishara ya kwenda Ninawi katika maombi ina maana maradufu. Kwanza kabisa kudhibitisha kwamba Mungu humtazama kila mtu bila ubaguzi; na hivyo ni ombi la nguvu kwa Bwana awaokoe na janga linaloendelea. Na wa naishi leo hii na hofu kubwa ya virusi vya corona. Kwa maana hii pia lazima waombe na kuomba msaada wa Mungu kuokolewa na kumaliza janga hili la ulimwengu wote. Hawajifikiriri wao tu wa  Iraq, bali kwa ajili ya watu wote ulimwenguni. Hadi sasa kuna maambukizi kati ya  500 au 600 yanayo rekodiwa kila siku, amefafanua Kardinali Sako.

Na hatimaye akijibu swali kuhusu maandalizi ya ziara ya Papa Francisko nchini Iraq mwezi wa tatu ujao yanavyo endelea, Kardinali Sako amethibitisha kwamba wanaendelea kuandaa pamoja na serikali. Ni tukio maalum. Kardinali amesema kuwa anafikiri Papa atakwenda kusema inatosha vita, vurugu ili kutafuta amani na udugu wakati huo huo kulinda hadhi ya binadamu. Kwa maoni ya Patriaki anasema pia  atawapelekea mambo mawili yaani “faraja na tumaini, ambavyo hadi sasa wamekosa na kukataliwa.  Kwa njia hiyo ni ziara ya kiroho, zaidi ya  kupewa sifa  sikukuu. Kwa kufanya hivyo inaweza kupoteza maana halisi ya ziara hiyo. Ni tukio muhimu sana kwao Wakristo, lakini kila mtu nchini Iraq anasubiri mkutano huu, pamoja na Waislamu, hali nyingine za kidini na viongozi wa serikali.

26 January 2021, 14:51