Tafuta

2020.07.22maombi ya watawa katika huduma kwenye mahospitali na vituo mbalimbali  2020.07.22maombi ya watawa katika huduma kwenye mahospitali na vituo mbalimbali  

UISG washukuru Papa kwa barua ya Motu Proprio ‘Spiritus Domini’

Kwa kutoa shukrani kwa Baba Mtakatifu Francisko kuwezesha ushiriki wa wanawake katika Kanisa kupitia huduma za usomaji wa masomo(Lector)na huduma ya kutumikia altareni(Acolyte)kama inavyoeleza barua ya Motu Proprio ‘Spiritus Domini’,Umoja wa Wakuu wa Mashirika ya Kitawa Kimataifa(UISG) wanaonesha umuhimu wa wanawake kama wachangiaji wa utume wa Kanisa.

Na Sr. Angela Rwezaula, - Vatican.

Wakitoa shukrani kwa Baba Mtakatifu Francisko kwa kuweka ushirikishwaji wa wanawake katika Kanisa kupitia huduma za usomaji wa masomo (Lector) na kutumikia altareni (Acolyte) kama inavyobainisaha kwenye barua ya Papa ya Motu Proprio ‘Spiritus Domini’, iliyotolewa Jumatatu tarehe 11 Januari 2021, Umoja wa Wakuu wa Mashirika  ya kitawa kimataifa (UISG) wanaonesha jukumu la wanawake kama wachangiaji wa utume wa Kanisa. Kwa Barua yake Papa Francisko ya Motu Proprio, inaanzisha wazi kwa huduma ya wanawake katika taasisi kupitia agizo maalum kwa usomaji wa Neno na kutoa huduma altareni wakati wa ibada za misa na liturujia mbali mbali. Ingawa suala hilo sio jambo jipya katika jamuiya nyingi kuona wanawake wakitangaza Neno la Mungu wakati wa sherehe za liturujia au wakitoa huduma altareni wakati wa ibada ya Ekaristi, kwa sababu ilikuwa hadi sasa inafanyika bila mamlaka sahihi ya taasisi, bali kwa idhini ya Askofu mahalia.

Na walio wengi hawawezi kuona upya huo na utofauti, kwa maana walikwisha zoea kuona hilo. Na kumbe basi ni jambo ambalo sasa linatumika rasmi. Kufuatia na hili Umoja huu wa watawa UISG, katika taarifa yao iliyotolewa Jumanne tarehe 12 Januari kwenye tovuti yake wanabainisha kuwa:  “Tunafurahi kutambua kwamba jina la Motu Proprio ni ‘Spiritus Domini’,”. Na uamuzi ambao sio wanaume tu bali pia wanawake wanaweza kuanzishwa kama Wasomaji na watoa huduma altareni ambayo ni ishara na jibu la  nguvu ambayo inaelezea asili ya Kanisa;  nguvu ambayo ni kwa njia ya  Roho Mtakatifu kila wakati anatoa  changamoto kwa  Kanisa katika utii na kwa njia ya ufunuo na ukweli”, wanaandika

UISG pia inabainisha kuwa hati hiyo iliyotolewa katika muktadha wa  Sherehe ya Ubatizo wa Bwana, siku ambayo Mungu alijifunulia kuwa na muungano na Yesu ambaye alikuwa mtumishi.  “Kwa kumtazama Yesu tunasasisha hadhi yetu ya ubatizo kama wana na mabinti katika Yeye, kama kaka na dada. Kutokana na ubatizo na baadaye  upako wa kikrisma yaani kipaimara sisi, wanaume na wanawake wote waliobatizwa, tunakuwa washiriki katika maisha na utume wa Kristo na wenye uwezo wa kuhudumia jamuiya.”

Katika kuweza kuchangia utume wa Kanisa, kushiriki huduma, Wakuu wa Mashirika wanasisitiza, kuwa “itatusaidia kuelewa, kama Baba Mtakatifu anavyosema katika barua yake iliyosindikiza ya Motu Proprio, kwamba katika utume huu “tumewekwa wakfu kwa kila mmoja”, waliowekwa wakfu rasmi  na wasiowekwa, wanaume na wanawake, katika uhusiano wa pamoja. Kwa maana hii, Wakuu wa mashirika (UISG” wanasisitiza, kuwa hii inaimarisha ushuhuda wa umoja  wa kiinjili.

Umoja wa Wakuu wa mashirika kimataifa aidha (UISG)wanaonesha kwamba tabia ya Motu Proprio ni uthibitisho katika njia ya Kanisa kukubali huduma ya wanawake wengi ambao wamejali na wanaendelea kutunza huduma ya Neno na katika altare. Katika maeneo mengi, taarifa hiyo inabainisha, kuwa wanawake, na hasa wanawake wanaojitolea, hutimiza huduma tofauti za kichungaji kwa kufuata miongozo ya maaskofu, katika kujibu mahitaji ya uinjilishaji.

13 January 2021, 16:00