Tafuta

2021.01.14 Monasteri ya Mater Ecclesiae katika Bustani za Vatican. 2021.01.14 Monasteri ya Mater Ecclesiae katika Bustani za Vatican. 

Papa Mstaafu Benedikto XVI,janga na Noeli ya kwanza bila kaka yake

Askofu Georg Gänswein anaelezea jinsi Papa Mstaafu,ambaye amepewa chanjo Alhamisi tarehe 14 Januari 2021,alivyopitia wakati huu mgumu bila kuwa na kaka yake karibu kama alivyokuwa amezoea kipindi cha Noeli.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Kile ambacho kimetokea kwa Papa Mstaafu Benedikto XVI kufanya siku kuu ya Noeli bila kuwa na kaka yake Georg, kwa namna moja au nyingine ukosefu wake ameuhisi kwa mara ya kwanza. Haya yamezungumzwa kwa Vatican News na Askofu Georg Gänswein, Rais wa Nyumba ya Kipapa na Katibu binafsi wa Papa mstaafu Benedikto XVI na ambaye tarehe 14 Januari 2021 amepata chanjo akiwa katika Monasteri ya ‘Mater Ecclesiae’ jijini Vatican.

Katika kuelezea jinsi  Papa Mstaafu alivyo sherehekea siku kuu hizi amesema “Kaka yake Papa Mstaafu Benedikto XVI kwa kawaida alikuwa amezoea kuja kukaa na kaka yake, lakini kutokana na kifo chake, kipindi chote cha siku kuu za Noeli, kwa mara ya kwanza, Papa Mstaafu amehisi ukosefu wake na kwa njia hiyo tuliweza kusikiliza mara nyingi kupitia CD japokuwa siyo za mtunzi Bach lakini pia hata tamasha la nyimbo za Noeli  ambazo aliongoza kaka yake Georg Ratzinger kwaya ya Regensburger Domspatzen.

Katibu wake Papa Mstaafu aidha amesema kuwa ukosefu wa kaka yake ni kama jeraha ambalo limesababisha uchungu katika siku kuu hizi walakini, amwambia kuwa alihisi faraja ya Bwana, na kwa hakika kwamba kaka yake sasa anaishi katika kukumbatiwa na yeye. Askofu Gänswein pia ameelezea jinsi wakati huu wa janga wanavyoishi ndani ya monasteri ya Mater Ecclesiae. Utararibu wa shughuli za kila siku haujabadilika sana, kwani mtindo wa siku umebaki vile vile, hata kama ziara zimepunguzwa sana. Aidha amebainisha kuwa Papa Mstaafu Benedikto anafuatilia habari zinazowafikia kupitia vyombo vya habari na anashiriki wasiwasi wa wote juu ya janga hilo, na kwa kile kinachotokea ulimwenguni, kwa watu wengi wanaopoteza maisha yao kwa sababu ya virusi. Kuna watu anaowafahamu ambao wamefariki kutokana na Covid-19 ”.

Hatimaye  katibu wa Papa Mstaafu Benedikto XVI, baada ya kusambazwa kwa picha zinazohusiana na mkutano na Baba Mtakatifu Francisko na makadinali wapya mnamo Novemba iliyopita, anathibitisha kuwa kimwili  ni dhaifu lakini anachangamka sana kiakili. "Kwa mtazamo wa mwili, yeye ni dhaifu sana na anaweza kutembea kidogo tu na kifaa maalum za kuegemea". Sauti yake pia ni dhaifu. Inaongezeka hasa wakati wa mapumziko lakini anaendelea kutoka wakati wa mchana licha ya baridi, kwenye bustani za Vatican. Na katika sala sala ya kila siku Askofu anadhimisha misa na Yeye anakuwa karibu amekaa kwa kufuatilia vizuri Liturujia ya Misa. Na kwa sala za kila siku, wameandaa maandishi makubwa ili aweze kufuatilia vizuri Masifu yote na kuendelea baadaye na chakula pamoja kama ambavyo wamekuwa wakifanya kila wakati

14 January 2021, 16:19