Tafuta

2019.12.04 kufika kwa wakimbizi uwanjani Fiumicino kupitia mkondo wa kibinadamu 2019.12.04 kufika kwa wakimbizi uwanjani Fiumicino kupitia mkondo wa kibinadamu 

Kard.Czerny:Utamaduni wa kukaribisha ndiyo utakaookoa wakati ujao!

Tafakari ya Katibu Msiaidizi katika Kitengo cha Wahamiaji cha Baraza la Kipapa cha Huduma ya Maendeleo Fungamani ya Binadamu iliyochapishwa katika Tovuti mpya ya Kamati ya Kimataifa ya wahamiaji anajikita kutazama Waraka wa Fratelli tutti wa Papa Francisko akikazia zaidi udugu na urafiki kwa watu wote.Anakumbusha vienzi vya kukaribisha,kulinda, kuhamasisha na kufungamanisha wahamiaji na wakimbizi.

Na Sr. Angela Rwezaula,-Vatican.

Katika Waraka mpya wa  Baba Mtakatifu Francisko, ‘Fratelli tutti’ yaani  ‘Wote ni  Ndugu’, unaelekezwa moja kwa moja furaha na matumaini, huzuni na uchungu wa wahamiaji, wakimbizi na watu wote waliohamishwa na waliotengwa. Moyo wa maandishi hayo ni wito  kwa ajili ya  udugu mkubwa na urafiki wa kijamii kati ya watu wote na mataifa. Hivi ndivyo Kadinali Michael Czerny, Katibu Mkuu Msaidizi wa kitengo cha Wahamiaji cha Baraza la Kipapa la  Maendeleo Fungamani ya Binadamu ameandika tafakari yake  kwenye Tovuti mpya ya Tume ya Kimataifa ya Uhamiaji Katoliki (ICMC). Tafakari ya Kardinali, Czerny aliyoipatia jina “Fratelli tutti na janga la waliokimbia makazi”, linajikita katika hatua msingi wa hati hiyo akikumbusha undugu ulio wazi, ambao unaruhusu kutambua, kuthamini na kumpenda kila mtu kupitia ukaribu wa mwili, mbali na sehemu katika ulimwengu ambapo alizaliwa au anapoishi”.

Haki ya maisha yenye hadhi

Kwa mujibu wa Kardinali Czerny, kila mtu ana haki ya kuishi maisha yenye hadhi na maendeleo fungamani  katika nchi yake ya asili. Hii inatia shaka uwajibikaji wa ulimwengu wote, kwani mataifa maskini lazima yasaidiwe kujiendeleza.  Uwekezaji ambao kwa walio wa mwisho wanahitaji  hauishi tu katika maendeleo endelevu ya uchumi, lakini pia hasa katika vita dhidi ya umaskini, njaa, magonjwa, uharibifu wa mazingira na mabadiliko ya tabianchi, anaandika.

Kukaribisha, kulinda, kuhamsiha na kufungamanisha

Katibu msaidizi wa kitengo cha Wahamiaji cha Baraza la Kipapa la Maendeleo Fungamani ya binadamu ameelekeza mwitikio wa kimaadili unaofaa kwa wale wote ambao wamelazimika kukimbia na kwamba unaweza kufupishwa kwa vitenzi vinne vya kazi: kuwakaribisha, kuwalinda, kuwahamasisha na kujumuisha au kufungamanisha. Lakini kuna vikwazo vingi vinavyojitokeza kando ya njia ya wahamiaji na wakimbizi. Ni vikwazo vilivyozaliwa na mawazo ya chuki dhidi ya wageni ambayo hayaendani na Ukristo amesisitiza.

Njia nyingi za kufungua milango

Kwa kufuatia mwongozo wa Waraka, Kardinali Michael Czerny anaonesha njia kadhaa za kufungua milango kwa wale ambao wametoroka kutokana na shida za kibinadamu na wamekuwa jirani wetu wapya. Hizi ni pamoja na kuongeza na kurahisisha utoaji wa visa, kupitisha mipango ya utetezi ya kibinafsi na ya kijamii, kufungua moìikonodo ya kibinadamu kwa wakimbizi walio katika mazingira magumu zaidi na kutoa makazi yanaofaa na bora kwao. Ni muhimu pia kuhakikisha usalama wa binafsi, upatikanaji wa huduma muhimu na haki. Pamoja na kuwapa uhuru wa kutembea na uwezekano wa kufanya kazi; kulinda watoto wadogo na kuhakikisha wanapata elimu kama kawaida.

14 January 2021, 16:50