Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu Ignace Bessi Dogbo kuwa Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Korhogo, nchini Pwani ya Pembe Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu Ignace Bessi Dogbo kuwa Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Korhogo, nchini Pwani ya Pembe 

Uteuzi: Askofu mkuu mteule Ignace B. Dogbo Jimbo kuu la Korhogo!

Askofu mkuu mteule Ignace Bessi Dogbo alizaliwa mwaka 1961 huko Niangon-Adjamé, Pwani ya Pembe. Tarehe 2 Agosti 1987 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre, Jimbo Katoliki la Yopougon. Ilikuwa ni tarehe 19 Machi 2004, Mtakatifu Yohane Paulo II alipomteuwa kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Katiola nchini Pwani ya Pembe. Akawekwa wakfu kuwa Askofu tarehe 4 Julai 2004.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amemteuwa Askofu Ignace Bessi Dogbo kuwa Askofu mkuu mpya wa Jimbo Kuu la Korhogo lililoko nchini Pwani ya Pembe, (Ivory Coast). Kabla ya uteuzi huu, Askofu mkuu mteule Ignace Bessi Dogbo alikuwa ni Askofu wa Jimbo Katoliki la Katiola nchini Pwani ya Pembe. Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu mteule Ignace Bessi Dogbo alizaliwa tarehe 17 Agosti 1961 huko Niangon-Adjamé, nchini Pwani ya Pembe. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 2 Agosti 1987 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre, Jimbo Katoliki la Yopougon.

Ilikuwa ni tarehe 19 Machi 2004, Mtakatifu Yohane Paulo II alipomteuwa kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Katiola nchini Pwani ya Pembe. Akawekwa wakfu kuwa Askofu tarehe 4 Julai 2004 na hatimaye, akasimikwa rasmi kama Askofu Jimbo tarehe 10 Julai 2004. Tarehe 12 Oktoba 2017, Baba Mtakatifu Francisko akamteuwa kuwa ni Msimamizi wa Kitume, Jimbo kuu Katoliki la Korhogo, Pwani ya Pembe. Hatimaye, Jumapili tarehe 3 Januari 2021, Baba Mtakatifu Francisko akamteuwa kuwa Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Korhogo.

Uteuzi Pwani ya Pembe
03 January 2021, 14:24