Tafuta

Baba Mtakatifu Francisko amemteuwa Askofu Fabio Fabene kuwa Katibu mkuu wa Baraza la Kipapa la Kuwatangaza waamini kuwa wenyeheri na watakatifu. Kabla ya hapo alikuwa ni Katibu mkuu msaidizi wa Sinodi za Maaskofu. Baba Mtakatifu Francisko amemteuwa Askofu Fabio Fabene kuwa Katibu mkuu wa Baraza la Kipapa la Kuwatangaza waamini kuwa wenyeheri na watakatifu. Kabla ya hapo alikuwa ni Katibu mkuu msaidizi wa Sinodi za Maaskofu. 

Askofu Fabene: Katibu mkuu: Baraza: Wenyeheri na Watakatifu

Askofu Fabio Fabene alizaliwa tarehe 12 Machi 1959 mjini Roma. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 26 Mei 1984 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Alijiendeleza na masomo na kubahatika kupata Shahada ya Uzamivu, Sheria za Kanisa kutoka Chuo Kikuu cha Kipapa cha Lateran. Akawekwa wakfu kuwa Askofu tarehe 30 Mei 2014 na Papa Francisko mjini Vatican.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu Fabio Fabene, kuwa Katibu mkuu wa Baraza la Kipapa la Kuwatangaza Waamini kuwa Wenyeheri na Watakatifu. Kabla ya uteuzi huu, Askofu Fabio Fabene alikuwa ni Katibu mkuu msaidizi wa Sekretarieti ya Sinodi za Maaskofu. Askofu Fabio Fabene alizaliwa kunako tarehe 12 Machi 1959 mjini Roma. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 26 Mei 1984 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Alijiendeleza na masomo na hatimaye, kubahatika kupata Shahada ya Uzamivu, Sheria za Kanisa kutoka Chuo Kikuu cha Kipapa cha Lateran. Amebahatika kuwa Jaalimu wa Sheria za Kanisa tangu mwaka 1984 hadi mwaka 1998.

Tarehe 1 Januari 1998 alianza utume wake kwenye Baraza la Kipapa la Maaskofu, huku akiteuliwa kuwa mkuu wa Ofisi. Tarehe 24 Aprili 2010 akateuliwa na Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI kuwa Katibu mwambata wa Baraza la Makardinali. Tangu mwaka 1996 amekuwa pia ni Hakimu wa Mahakama ya Jimbo kuu la Roma mintarafu masuala ya ndoa na familia. Ni mwandishi wa vitabu na makala nyingi kuhusu Daraja Takatifu ya Upadre. Tarehe 8 Februari 2014, Baba Mtakatifu Francisko akamteuwa kuwa Katibu mkuu msaidizi wa Sekretarieti ya Sinodi za Maaskofu na kumpandisha hadhi na kuwa Askofu. Tarehe 30 Mei 2014 akawekwa wakfu na Baba Mtakatifu Francisko kuwa Askofu. Na ilipogota tarehe 18 Januari 2021, Baba Mtakatifu Francisko akamteuwa kuwa Katibu mkuu wa Baraza la Kipapa la Kuwatangaza Waamini kuwa Wenyeheri na Watakatifu.

Askofu Fabene
19 January 2021, 14:26