Vatican yatoa msaada wa dhati kwa Ifad ili kupambana na njaa
Kwa upande wa Shirika la Mpango na Chakula IFAD linatoa shukrani na maelezo kwamba msaada wa dola za kimarekani 25,000 ambazo zimetolewa na Vatican zinaweza kusaidia na kuendeleza shughuli za Shirika la Umoja wa Mataifa ambalo linajikita katika mapambano dhidi ya njaa na umaskini ulimwenguni kote.
Jumuiya kimataifa iunganishe nguvu zake
Kwa mujibu wa Gazeti la Osservatore Romano, hata hivyo linaonesha jinsi ambavyo katika tovuti ya IFAD, imetaja barua ya Kardinali Parolin kwamba anasisitiza umuhimu wa kuanzisha jambo hili. “Haiwezekani kwa urahisi tu kubaki kimya mbele ya mateso mengi haya namna hii. Leo hii kuliko hapo awali, Jumuiya ya kimataifa lazima iunganishe nguvu zake ili kuwandaa na kutimiza wakati ujao ambao uwe endelevu, jumuishi na wenye haki kwa wote. Haya ndiyo tunapaswa kufanya na ndiyo wajibu wetu wa kusaidia watu walio maskini zaidi na waathirika katika ulimwengu huu”. Kwa mujibu wa Kardinali katika barua yake.
Umuhimu wa kufanya kazi pamoja
Tangazo la mchango wa Vatican limetolewa tarehe 11 Desmba katika mutadha wa mchakato mpya wa hukusanyaji wa fedha kwa ajili ya IFAD kwa upandw wa Nchi wanachama. Kwa mtzamo huo, Rais wa IFAD, Bwana Gilbert F. Houngbo, amesea kuwa “ni muhimu kufanya kazi pamoja kwa ajili ya kubadili mifumo yetu ya chakula na kuongeza matarajio na ustawi wa watu wa vijijini ambao wanamazingira magumu zaidi ulimwenguni”.