Kuhakikisha chanjo kwa wote ni haki Kuhakikisha chanjo kwa wote ni haki 

Vatican:Kuhakikisha chanjo kwa kila mtu ni suala la haki!

Hati ya pamoja ya Tume ya Vatican ya Covid-19 na Taasisi ya Kipapa ya Elimu ya Maisha wanathibitishwa kuwa ni jukumu la maadili kukubali chanjo na sio tu kwa ajili ya afya ya mtu binafsi bali pia kwa ajili ya afya ya umma.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Chanjo zimetengenezwa kama faida ya umma na lazima zipatikane kwa wote kwa njia ya haki na usawa, ikipewa kipaumbele kwa wale wanaozihitaji zaidi. Hivi ndivyo Tume ya Vatican ya Covid-19 na Taasisi ya Kipapa ya Elimu ya Maisha wanakumbuka, huku wakisisitiza, katika hati ya pamoja, jukumu muhimu la chanjo katika kushinda janga hilo. Katika maandishi hayo, wanarudia ujumbe wa Papa Francisko  wa hivi karibuni wa Krismasi, wakiwashuri viongozi wa ulimwengu wahimize kupinga vishawishi vya kufuata utaifa wa chanjo na serikali za kitaifa kushirikiana.

Kanuni

Haki, mshikamano na ujumuishaji ndio vigezo vikuu vya kufuatwa ili kukabili changamoto zinazosababishwa na dharura hii ya sayari. Makampuni ambayo yanaweza kutathminiwa vyema, Baba Mtakatifu alikuwa amesema katika Katekesi yake mnamo Agosti 19, kuwa ni yale  ambayo "yanachangia ujumuishaji wa waliotengwa, kuhamasishwa watu walio wa mwisho, kwa ajili ya faida ya wote na utunzaji wa kazi ya uumbaji”. Dira muhimu kwa maana hiyo ni upeo ambao umeunganishwa na kanuni za Mafundisho Jamii ya Kanisa, kama vile utu wa kibinadamu na chaguo  zaidi kwa maskini, mshikamano na ushirikiano kwa ajili ya faida ya wote na utunzaji wa nyumba yetu ya pamoja, haki na hatima ya mali ya ulimwengu wote.

Utafiti, uzalishaji na vifaa vya kibaolojia

Hivi karibuni Taasisi ya Kipapa ya Elimu ya Maisha ilirudia  kwenye mada katika aandishi mawili, bila kujumuisha pamoja na mambo mengine, kwamba "kuna ushirikiano wa kimaadili kati ya wale ambao leo hi hutumia chanjo hizi na mazoezi ya utoaji mimba kwa hiari". Kwa maana hiy. hati hiyo inasomeka kuwa  inaaminika kwamba “chanjo zote zinazopendekezwa katika kliniki zinaweza kutumika kwa dhamiri thabiti, kwamba utumiaji wa chanjo kama hizo haimaanishi ushirikiano katika utoaji mimba kwa hiari”. “Licha ya jitihada za pamoja katika kuhakikisha kuwa kila chanjo haina rejeo la utayarishaji wake wa nyenzo yoyote inayotokana na utoaji mimba na limethibitishwa jukumu la uwajibikaji maadili wa chanjo ili kutosababisha hatari kubwa za kiafya kwa watoto na idadi kubwa ya watu kwa jumla."

Hati miliki

Madhumuni pekee ya unyonyaji wa kibiashara “haikubaliki kimaadili katika uwanja wa dawa na huduma za afya”. “Uwekezaji katika uwanja wa matibabu unapaswa kupata maana yake ya kina katika mshikamano wa kibinadamu”. Inahitajika kutambua “fursa za mifumo inayofaa na inayopendelea uwazi na ushirikiano, badala ya uhasama na ushindani”. Na lazima ishinde kila aina ya “utaifa wa chanjo”. Uzalishaji wa viwandani wa chanjo unaweza kuwa “operesheni ya ushirikiano kati ya mataifa, makampuni ya dawa na mashirika mengine”.

Idhini na usimamizi

Kuhusiana na usimamizi, Tume ya Vatican ya Covid-19 na Taasisi ya Kipapa ya Elimu ya Maisha vinaunga mkono nafasi zinazobadilika juu ya vipaumbele  hasa “kutengwa kwa vikundi vya kitaalam vinavyohusika katika huduma ya pamoja ya masilahi, kwa namna ya pekee wafanyakazi wa afya, lakini pia katika shughuli nyingine ambazo zinahitaji kuwasiliana na umma kwa ajili ya huduma muhimu (kama vile  shule na usalama wa umma); aidha kwa vikundi vilivyo hatarini zaidi (kama vile wazee na wagonjwa walio na magonjwa fulani.” Usambazaji wa chanjo pia unahitaji safu za zana nyingi zinazoruhusu “upatikanaji  wake ulimwenguni”.

Chanjo na masuala ya maadili

Na kuhusu jukumu la maadili ya kupatiwa chanjo, Tume ya Vatican ya Covid-19 na Taasisi ya Kipapa ya Elimu ya Maisha kwa pamoja vinathibitisha kuwa suala hili linamaanisha “uhusiano kati ya afya kibinafsi na afya ya umma, kwa kuonesha kutegemeana kwao kwa karibu”. Kukataa chanjo pia kunaweza kusababisha hatari kwa wengine. “Hii inatumika pia ikiwa ni kwa kukosekana kwa njia mbadala, motisha ulikuwa kuzuia kufaidika na matokeo ya utoaji mimba kwa hiari”.

Mpango wa utekelezaji

Chanjo salama, inayofaa na inayopatikana kwa kila mtu, hasa aliye katika mazingira magumu zaidi na kwa bei ambayo inaruhusu usambazaji wa haki. Hivi ndivyo vipaumbele vya kuhakikisha utunzaji wa ulimwengu ambao “unazingatia na kuongeza” hata katika hali za kawaida. Katika hatua hiyo Hati hiyo inabainisha kwamba, lengo ni kuongeza rasilimali kwa ajili ya kusaidia Makanisa mahalia katika kandaa maanzisho yote na protokali ambazo zinatazama jumuiya maalum. Kanisa liko katika huduma ya “uponyaji wa ulimwengu” kwa kutumia sauti zake ili kueneza katika sayari yote,” kwa kuzungumza, kuhamasisha na kusaidia kuhakikisha kuwa chanjo bora na huduma zinapatikana kwa familia yetu ya ulimwengu, hasa kwa watu wanyonge”.

Kujenga ulimwengu baada ya Covid

Rais wa Baraza la Kipapa la Huduma ya Maendeleo Frngamani ya Binadamu, Kardinali Peter Turkson, ametoa shukrani “kwa jumuiya ya wanasayansi kwa kutengeneza chanjo hiyo katika muda mfupi wa rekodi”. “Lazima tuoneshe, mara moja na kwa wote, kwamba sisi ni familia moja ya wanadamu”. Naye Askofu Mkuu Vincenzo Paglia, Rais wa Taasisi ya Kipapa ya Elimu ya Maisha, amesisitiza kuwa janga hilo limeangazia hali ya unganisho linalo unganisha ubinadamu wote. 

29 December 2020, 17:19