Papa Francisko na Askofu   Nunzio Galatino  Rais wa APSA Papa Francisko na Askofu Nunzio Galatino Rais wa APSA 

Ask.Galantino:shukrani kwa mageuzi haya kutakuwa na uwazi zaidi

Ni maneno ya Rais wa APSA akifafanua kuhusiana na barua ya Motu Proprio ya Papa Francisko ambayo imejikita katika kiini cha Utawala na usimamizi wa uchumi na Mali za Makao makuu zisizoshikika

VATICAN NEWS

Kulikuwa na hitaji la kubadilisha usimamizi wa fedha, uchumi na utawala, kuongeza uwazi na urekebishaji. Ni kwa mujbu wa Askofu Nunzio Galantino, Rais wa Utawala wa Urithi na usimamizi wa mali  za Kitume (APSA) akitoa maoni na Vatican News kuhuhus uchapishaji wa Motu proprio ya Baba Mtakatifu Francisko ambaye katika sehemu ya mwisho ya  mwaka 2020 ametekeleza mageuzi ambayo yanaweka usimamizi wa uwekezaji na fedha na mali isiyohamishika.

Je! Ni nini umuhimu wa uamuzi uliofanywa kujulikana na kanuni ya kipapa kuhamisha usimamizi wa fedha na mali ya Sekretarieti ya Nchi kwa APSA?

Ni kuendelea na  mchakato, ufafanuzi wa utendaji wa kile  ambacho Papa alikuwa ameonyesha  mwezi Agosti uliopita katika barua yake kwa Katibu wa Vatican. Ni matokeo ya tafiti na utafiti ambao umefanywa. Ni mchakato ulioanza kutokea mbali, ambao ulitamaniwa na Papa Mstaafu Benedikto XVI na umeonyeshwa kwa dalili kadhaa na makadinali katika majadiliano yaliyotangulia na mkutano wa mwisho. Kulikuwa na haja ya kubadilisha usimamizi wa fedha, uchumi na utawala, ili kuongeza uwazi  zaidi  na urekebishaji.

Je! Ni faida gani tunaweza kutarajia kutokana  na uhamisho huu?

Nadhani faida ni kwamba tayari imeonyeshwa vizuri katika barua ya Papa kwa Kardinali Parolin mnamo Agosti iliyopita yaani kuhusu urekebishaji wa utawala ulio wazi zaidi. Ikiwa kuna baraza la kipapa lililoteuliwa kwa usimamizi na usimamizi wa fedha na mali, sio lazima kuwa kuna wengine kufanya kazi hiyo hiyo. Ikiwa kuna idara ya kipapa iliyoteuliwa kwa udhibiti wa uwekezaji na matumizi, hakuna haja ya kazi hiyo hiyo kufanywa na wengine pia. Ni muhimu kukumbuka kuwa mwezi Oktoba iliyopita Papa alianzisha Tume ya Mambo ya Hifadhi muhimu: katika tukio hilo ikawa wazi kwa kila mtu kwamba hakuna tena uwezekano wa hiari wa usiri juu ya shughuli za kiuchumi na kifedha.

Ni kwa jinsi gani kumekuwa na uzito juu ya kuzingatia maamuzi ya tukio la mali isiyo hamishika ya jengo kwenye barabara ya Sloane huko London, katikati ya uchunguzi na mahakama ya Vatican?

Itakuwa unafiki kusema kwamba haikuwa na uzito. Hakika Papa alikuwa tayari amepanga njia, lakini suala la jengo la London ilisaidia kuwafanya watu waelewe ni njia gani za kudhibiti zinapaswa kuimarishwa. Ilitufanya tuelewe vitu vingi: sio tu ni kiasi gani tumepoteza , lakini  kipengele ambacho bado tunatathmini  na  lakini pia jinsi na kwa nini tumepoteza.

Ni mabadiliko gani kuhusu usimamizi wa  Mfuko wa Mtakatifu Petro?

Kwa upande wa mfuko wa Mtakatifu Petro, Papa kila wakati ameomba kwamba kuwepo na tofauti kubwa zaidi kulingana na mifuko mingine iliyopo, zilizounganishwa kimsingi na maelekezo yake. Mfuko wa mtakatifu Petro ullianzishwa  kama mchango wa waamini, wa Makanisa mahalia, kwa ajili ya utume wa Papa ambaye ni mchungaji wa ulimwengu wote, na kwa hivyo amekusudia kwa ajili ya upendo, uinjilishaji, maisha ya kawaida ya Kanisa na miundo inayomsaidia Askofu wa Roma kutekeleza huduma yake. Mfuko huo  utasimamiwa na kuendeshwa na APSA na Sekretarieti ya Uchumi kulingana na maelekezo ya moja kwa moja ya Papa, kama mfuko tofauti na fedha nyingine ambazo zina maeneo mengine ya kuelekezwa.

29 December 2020, 11:29