Tafakari ya kwanza ya Kardinali Cantalamesaa ya majilio kwa ushiriki wa Papa Francisko katika ukumbi wa Paulo VI Tafakari ya kwanza ya Kardinali Cantalamesaa ya majilio kwa ushiriki wa Papa Francisko katika ukumbi wa Paulo VI 

Tafakari ya kwanza ya Majilio:Kard.Cantalemessa afafanua dada kifo ni kiini cha maisha!

Mhubiri wa Nyumba ya kipapa Kardinali Raniero Cantalamessa,wakati wa tafakari yake ya kwanza ya kipindi cha majilio kwa uwepo wa Papa Francisko kwenye Ukumbi wa Paulo VI amewataka washiriki wote watafakari maana ya kifo kwa maana ya kwamba maisha ya mwaamini ni ya milele.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Utufundishe ufupi wa maisha yetu ili tuweze kuwa na hekima ya moyo ni kufungu kutoka Zab 90,12 ambayo imezinduliwa tarehe 4 Desemba inayoongaza mzunguko wa tafakari za kipindi cha Majilio, ambayo itaendelea siku ya  Ijumaa tarehe 11 na 18 Desemba 2020. Hata kwa mwaka huu, Mhubiri wa nyumba ya kipapa, Kardinali Raniero Cantalamessa amefafanua kwa ufasaha wake kwenye takafakari hiyo katika Ukumbi wa Paulo VI kwa uwepo wa Papa Francisko. Kwa kunukuu mara nyingi mtunzi wa mashairi wa kiitaliano Giuseppe Ungaretti ameweza kufafanua hisia za moyo wa wanjaeshi wakati wa mapamban ya vita vya kwanza vya dunia kwa shairi liitwalo  ‘Askari’. Yupo kama kipindi cha kupukutika kwa majani ya miti”.

Katika mfano huo amesema leo hii ni binadamu wote wanaofanya uzoefu wa maana ya kuanguka kwa maisha, ni katika  mtazamo wa janga tunaloishi kwa sasa. Na kwa maana hiyo  Kardinali ameshauri kutafakari juu ya kifo na maono katika maisha ya kila mtu.  Amekumbusha kuwa maisha ya mwanadamu hayaishii na kifo tu,  kwa sababu mtu huyo anatarajia maisha ya milele.  Kwa mujibu wa maandiko ya  Baba wa Kanisa Mtakatifu Agostino alisema “ kifo ni ugonjwa wa kifo unachokumbana nacho wakati unazaliwa”.  Hivyo kwa kuongezea amesema dada kifo kiukweli ni dada mkubwa mwema na ambaye ni mwalimu mwema. Anatufundisha mambo mengi. Kifo ambacho kinafuatwa  hukumu ya Mungu ni jambo muhimu la kutazama, amesisitiza Kardinali Cantalamessa. Kifo ni mwasho  wa mateso yote na ukosefu wa haki ambao umo katikati ya watu. Kifo ni mwisho wa tofauti zote na dhuluma zilizopo kati ya wanaume na wanawake . “Kifo, alisema muigizaji wetu wa vichekesho Totò, ni kipimo, maana  huondoa marupurupu yote”. Kwa  kutafakarisha amesisitiza “Ni vita ngapi, ni unyama wa kiasi gani umefanywa duniani ikiwa ni pamoja na wanyanyasaji wa watu wakidhani kwamba wao  hawatakufa hivi karibuni!  Kwa kuangalia maisha kutokana  na maono ya kifo yangeweza kuwa msaada mkubwa wa kuweza kuishi vizuri  sasa”, amesisitiza Kardinali Cantalamessa.

Je! Unasumbuliwa na shida na matizo? Peleka mbele, na jipeleke mahali pazuri: Je! ungependa kuchukua hatua wakati huo? Je! ni umuhimu gani ungetoa kwa vitu hivi? Je! una mgogoro na mtu? Angalia  kitanda cha kifo. Je! Ungefanya nini wakati huo: umeshinda, au umejidhalilisha? Baada ya kushinda, au kusamehewa? Kardinali amesema “Mawazo ya kifo hutuzuia kushikamana na vitu, na kutaka  kurekebisha nyumba ya moyo hapa chini, tukisahau kwamba hatuna nyumba thabiti hapa chini. Kuna kifo kimoja tu, Kadinali amesisitiza , kwamba mtu lazima aogope kwa sababu sumu yake inaua mtu kweli: Kifo cha milele! Ni kifo cha pili, katika kitabu cha Ufunuo anakiita (Ufu 20, 6). Ni kimoja tu ambacho kinastahili jina la kifo, kwa sababu siyo hatua ya Pasaka, bali ni kituo cha mwisho cha kutisha. Katika  kuokoa wanaume na wanawake kutokana na janga hili ni kwamba lazima turudi kuwahubiria Wakristo juu ya kifo. Hakuna mtu aliyejua sura mpya ya Pasaka ya kifo cha Mkristo kuliko Mtakatifu Francis wa Assisi. Kifo chake kiukweli kilikuwa hatua ya kipasaka, "transitus", kama inavyoadhimishwa katika ibada ya Wafransiskani. Alipohisi karibu na mwisho, wake maskini huyo wa Assisi alisema: “Karibu, dada yangu kifo!" na zaidi katika Wimbo wake wa sifua ya viumbe vyote anaimba matendo mazuri sana juu ya  kifo:

“Sifa iwe kwako  wewe, Bwana wangu, kupitia kifo dada yetu, ambaye hakuna mtu aliye hai anayeweza kukimbia: ole wao wanaokufa katika dhambi za mauti; heri wale watakaopata katika mapenzi yako matakatifu sana, kwani kifo cha pili hakitawadhuru ”.

Kardinali aidha amesema “Ole wao watakufa katika dhambi za mauti! Mtu akiishi katika dhambi ya mauti, kwake mauti bado yana uchungu na sumu! Kuondoa dhambi maana yake ni kuondoa uchungu wake kutoka mautini”.  Na kuna njia ya upendeleo, amekumbuka mhubiri wa Nyumba ya  Kipapa, kujiandaa kwa ajili ya kifo kwamba: “Kwa kuanzisha Ekaristi, Yesu alitatabiri  kifo chake mwenyewe. Tunaweza kufanya vivyo hivyo. Kiukweli, Yesu aligundua hii na kutufanya sisi tushiriki katika kifo chake, na  kutuunganisha yeye mwenyewe. Kushiriki katika Ekaristi ni njia ya kweli, ya haki na bora zaidi ya kujiandaa kwa ajili ya kifo”.  Vile vile “ndani yake pia tunasherehekea kifo chetu na tunajitoa, siku kwa siku, kwa Baba. Katika Ekaristi tunaweza kusema amina, yaani  ndiyo na  kuinua kwa Baba, kwa kile kinachotungojea, katika aina ya kifo ambacho atataka kuturuhusu”. Kardinali ameongeza “Lakini ndani mwake sisi tunafanya  agano la  kuamua ni nani wa kuacha katika maisha, na ni nani afe” .

04 December 2020, 17:29