Kampeni ya chanjo ya kuzuia Covid-19 Kampeni ya chanjo ya kuzuia Covid-19 

Mpango wa chanjo ya kuzui covid kuanza mjini Vatican!

Kampeni ya chanjo dhidi ya virusi vya corona ua covid-19 itaanza ndani ya Serikali ya Jiji la Vatican katika miezi ya kwanza ya 2021.

Na Sr. Angela Rwezaula -Vatican.

Tayari kuanzia miezi ya kwanza ya mwaka ujao jijini Vatican itawezekana kupata chanjo ya kupambana na Covid-19. Ni matarajio kwamba kwa wakati mfupi sana wataweza kupanga na kusimamia maandalizi. Mpango wa chanjo, ulioanzishwa na Mfuko wa Msaada wa Afya na Kurugenzi ya Afya na Usafi wa Utawala, utawahusu raia, wafanyakazi, lakini pia hata wanafamilia ambao wanapata msaada kutoka kwa FAS. Kwa sasa, inashauriwa kutochanja watoto chini ya miaka 18, lakini ni vema kutathmini fursa hiyo mbele ya magonjwa fulani. Mwaliko kutoka tawala za Jiji la Vatican na Vatican  ni kumjulisha kila mtu kuwa chanjo sio tu kwa ajili ya ulinzi wa afya yake mwenyewe, bali pia ni kwa ajili ya watu wengine. Kwa mujibu  wa Profesa Andrea Arcangeli, mkurugenzi mpya wa Kurugenzi ya Afya na Usafi wa Utawala wa Jiji la Vatican, ameulizwa na Vatican News  kwanini uchaguzi huu na kijibu kuwa:

Tunaamini ni muhimu sana kwamba hata katika jamuiya  yetu ndogo kampeni ya chanjo dhidi ya virusi inayohusika na COVID-19 inaanza haraka iwezekanavyo. Kiukweli ni kwa njia ya chanjo itakayooenea na kutolewa kwa idadi ya watu wengi  ndio itawezekana kupata faida halisi kwa upande wa afya ya umma ili kupata udhibiti wa janga hili. Kwa maana hiyo ni jukumu letu kuwapa wakaazi wote, wafanyakazi na familia zao fursa ya kupatiwa chanjo kutokana na ugonjwa huu mbaya.

Je ni chanjo ipi imechaguliwa na kwanini? Je! Na wengine watatumia pia?

Iliamuliwa kuanza na chanjo iliyotengenezwa na Kampuni ya dawa ya Pfizer, ya kwanza kuletwa katika matumizi ya kliniki, ambayo imeonyeshwa kuwa na ufanisi wa asilimia 95%. Hivi sasa chanjo hii ndiyo pekee ambayo iko kwenye mchakato unaondelewa kwa idhini ya mamlaka ya afya ya Ulaya na Marekani. Kama inavyojulikana, kampeni ya chanjo na uzalishaji wake huo ni tayari imeanza nchini Uingereza. Baadaye, chanjo zingine zinazozalishwa na njia tofauti zinaweza kuletwa baada ya kutathmini ufanisi wao na usalama kamili.

Katika miezi ya hivi karibuni, umefunguliwa mjadala mpana juu ya chanjo ya COVID-19: kwa upande mmoja tumeshuhudia vita dhidi ya wakati ambao imeshirikisha jamuiya nzima ya kimataifa, kwa upande mwingine mashaka mengi na hofu. Je chanjo ni salama?

Inaeleweka kuwa kunaweza kuwa na hofu kwa sababu ya  chanjo ambayo imetengenezwa kwa muda mfupi, lakini vipimo muhimu sana vya usalama vimetekelezwa na kuna uhakikisho uliotolewa na mamlaka ya afya ulimwenguni kwamba kabla ya kutoa idhini ya uuzaji wanafanya mafunzo yenye nyeti sana. Kwa kuongezea, ni lazima izingatiwe kuwa chanjo zote zinaweza kusababisha dalili fulani, ambazo kwa ujumla hutegemea na hali halisi mahalia (kimsingi dalili hizi zina maumivu na uvimbe kwenye sehemu ya kudungwa sindano). Katika hali nyingine, homa na maumivu ya kichwa pia yanaweza kutokea. Hata baada ya sindano ya chanjo ya COVID-19, imeelezewa kwamba inawezekana kuonekana katika dalili hizi tofauti.

Vatican, haipendekezi chanjo kufanywa kwa walio chini ya miaka 18 na huko Uingereza mahali ambapo kampeni kubwa imeanza tayari, vile vile mamlaka ya afya hawashauri kutumia chanjo kwa wagonjwa wanaoteseka na alegia iwe kwa muda mrefu na hata kwa muda mfupi …

Kuhusu chanjo chini ya miaka 18, hakuna tafiti ambazo zimefanywa na ambazo zinajumuisha kikundi hiki cha umri kwa maana hiyo hazijajumuishwa katika mpango wa chanjo na kwa upande wa wale wenye alegia kila wakati inashauriwa kuwa na tathmini ya matibabu kutoka kwa daktari kabla ya kufanyiwa chanjo ya aina yoyote.

12 December 2020, 07:41