Asubuhi ya Papa katika maombi ya kuombea Roma na ulimwengu
Tarehe 8 Desemba 2020 ni siku ambayo Mama Kanisa anaadhimisha Siku Kuu ya Bikira Maria Mkingiwa dhambi ya Asili. Katika mwanga wa mapambazuko ya siku na ukimya ya mji wa Roma kutokana na mvua iliyokuwa ikinyesha, Papa Francisko amefika saa 1:00 kamili asubuhi katika Uwanja wa Hispania kwa ajili ya tendo la kutoa heshima kwa Bikira Maria mkingiwa wa dhambi ya Asili. Chini ya miguu ya Sanamu ya Maria, Papa amesali huku akielekeza macho juu ya Mama wa Mungu. Baadaye ameweka shada la maua ya mawiridi meupe.
Maombia hayakusindikizwa kama ilivyo kiutamaduni katika fursa kama hiyo yaani kwa kawaida kuzungukwa na umati mkubwa wa watu, kwa maana katika siku hii, Papa amekwenda katika muda ambao siyo wa kawaida katika uwanja wa Hispania, yaani asubuhi na siyo mchana kwa sababu ya hali halisi ya kiafya ili kuzuia hatari la mkusanyiko wa watu wengi ambao wanaweza kusababisha maambukizi, kama walivyokuwa tayari wameshatoa taarifa.
Kwa mujibu wa msemaji wa vyombo vya habari Vatican, Papa amemkabidhi Mama Maria watu wote ambao katika mji huu na katika ulimwengu wanasumbuliwa na ugonjwa na kukata tamaa. Kabla ya saa 7:15, asubuhi, Papa Francisko ameacha uwanja huo wa Hispania na kuelekea katika Kanisa Kuu la Bikira Maria Mkuu na kusali mbele ya Picha ya Maria Salus Popoli Romani na ameadhimisha Misa katika Kikanisa cha Mtakatifu Yosefu na baadaye kurudi mjini Vatican.