2019.02.14 Watakatifu Cirilly na Methodius 2019.02.14 Watakatifu Cirilly na Methodius  

40° ya watakatifu Cirilly na Methodius kutangazwa kuwa wasimamizi wa Ulaya!

Matashi mema ya Kardinali Kurt Koch Rais wa Baraza la kipapa la uhamasishaji wa Umoja wa Wakristo aliyoeleza kwa njia ya video wakati wa fursa ya miaka 40 tangu kutangazwa kwa watakatifu Cirilly na Mathodius pamoja na Mtakatifu Benedikto kuwa wasimamizi wa Bara la Ulaya.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Umetolewa Ujumbe kwa njia ya video  unaobeba  matashi mema kutoka kwa Kardinali Kurt Koch, Rais wa Baraza la Kipapa la kuhamasisha Umoja wa Wakristo wakati wa fursa ya kumbu kumbu ya miaka 40 tangu kutangazwa Watakatifu Cirily na Methodius kuwa wasimamizi wa Bara la Ulaya pamoja na Mtakatifu Benedikto. Katika ujumbe wake  Kardinali anasema, “katika siku ya mwisho 2020 unadhimishwa miaka 40 tangu kutangazwa kwa Watakatifu Cirilly e Methodius wasimamizi wa Bara la Ulaya waliotangazwa na Mtakatifu Yohane Paulo II kwa barua ya kitume “Egregiae Virtutis”, yaani kuandika wazo lisilofutika.

Barua ya uthibitisha  huo ilichapishwa tarehe 31 Desemba 1980 katika tukio la maadhimsho ya miaka 100 tangu kutangazwa Waraka wa ‘Grande Munus’ (1880), ambapo Papa Leone XIII alikuwa anakumbusha Kanisa lote kuhusu sura muhimu za shughuli za kitume za hawa watakatifu Cirilly na Methodius na katika fursa hiyo, ilianzishwa siku kuu ya liturujia kwenye kalenda ya Kanisa Katoliki.

Rais wa Baraza la Kipapa la kuhamasisha Umoja wa Wakristo, anaelezea matashi yake mema katika fursa hiyo ya kumbu kumbu, huku akisisitiza kuwa “watakatifu Cirilly na Methodius, wanao heshimiwa sana katika Nchi za Mashariki na Magharibi; na kwa sisi sote ni mashuhuda wa umoja usiogawanyika wa asili, wenye uwezo wa kuhifadhi na kuweka pamoja tofauti. Kwa maana hii maisha yao yatutie msukumo katika mchakato wa safari yetu ya kuelekea umoja”.

31 December 2020, 16:47