Tafuta

Askofu Mkuu Ivan Jurkovič, Askofu Mkuu Ivan Jurkovič, 

Vatican Jurkovič:kusaidia waathiriwa wa silaha za maangamizi makubwa

Lazima Kusikiliza na kusaidia wahanga wa silaha za maangamizi ndiyo maombi ya Askofu Mkuu Ivan Jurkovič,Mwakilishi wa kudumu wa Vatican katika ofisi za Umoja wa Mataifa huko Geneva,katika mkutano uliofanyika tarehe 26 Novemba kuhusu mapitio ya Mkataba juu ya kupinga usambazaji wa silaha za maangamizi makubwa.

Sr. Angela Rwezaula-Vatican.

“Hakuna wakati wa kupoteza hasa kwa sababu kila mtu anahesabiwa na kila mwathiriwa anahesabiwa ndivyo Askofu Mkuu Jurkovič Mwakilishi wa kudumu wa Vatican katika ofisi za Umoja wa Mataifa huko Geneva amesisitiza umuhimu wa kutoa msaada na kutoa sauti kwa wahanga hawa wa kuathiriwa na silaha za maangamizi katika mkutano wa mapitio wa Hati ya  Mkataba juu ya kupinga  usambazaji wa silaha za maangamizi makubwa.  Hiki Chombo halali cha kufanikisha lengo hilo amesisitiza Askofu Mkuu Jurkovič na kwamba  ni Mkataba maalum ambao, “tangu ulipoanza kutumika, umefanya mabadiliko, hasa kati ya waathiriwa na kati ya wale ambao umesaidia kuwalinda.

Hati hii, kiukweli, ni uthibitisho wazi wa uhusiano usioweza kueleweka kati ya upokonyaji silaha na maendeleo, kwa sababu unamweka mwanadamu katikati. Hii inaonyesha kuwa kadri tunavyowekeza zaidi katika kupunguza silaha, ndivyo tunavyohitaji rasilimali kidogo katika msaada wa kibinadamu. Kwa maana hiyo anakumbusha Mwakilishi wa Kudumu kwamba wamefanya juhudi za kinga na elimu kwa ajili ya  amani, kama zana muhimu ili kukidhi shauku ya usalama na utulivu ambao ni moja wapo ya shauku ya moyo wa mwanadamu na ambao inahitaji majibu ya kutosha ambayo huenda zaidi  tu ya mwelekeo wa kijeshi.

Wakati huo huo, mwakilishi wa Vatican alielezea juu ya wasiwasi wa Vatican kwa ongezeko la majeruhi ya raia na ukweli kwamba silaha za maangamizi hayo bado zinaendelea kutumiwa hadi  leo. Sio hivyo tu, kuna ugumu wa sasa umezidishwa na janga linaloendelea ambalo pia litakuwa na athari za muda mrefu kijamii na kiuchumi katika mikoa mingi, hasa katika nchi zinazoendelea. Walakini hii ndiyo matakwa ya Askofu Mkuu Jurkovič, kwamba  ni muhimu sana majukumu yaliyofanyika, hasa kuhusiana na msaada wa waathiriwa, yazingatiwe. Nguvu ya Mkataba, kiukweli, iko katika wazo la ushirikiano na ushirikiano kati ya Mataifa; kwa maana hiyo, kama familia ya mataifa, amesema “tukitazama malengo yale yale chini ya Mkataba huu, ucheleweshaji na kutofaulu kwa nchi ziliyosaini ni kufeli kwa wote na kufaulu kwa mmoja ni kufaulu kwa wote”.

Akitaja kifungu cha waraka wa ‘Fratelli tutti’ yaani  ‘wote ni Ndugu’ wa  Papa Francisko, mwakilishi wa  Kudumu amesisitiza kwamba “vita ni kutofaulu kwa siasa na ubinadamu, kujisalimisha kwa aibu, kushindwa mbele ya nguvu za uovu. Kwa njia hiyo lazima tuishie kwenye majadiliano ya kweli na si kinadharia, tuwasiliane na vidonda, tuguse nyama ya wale wanaopata uharibifu. Tugeuze  macho yetu kwa raia wengi waliouawa kama 'uharibifu wa dhamana'. (…) tuchunguze ukweli wa waathiriwa wa vurugu, tuangalie ukweli kwa macho yao na tusikilize historia zao kwa moyo ulio wazi. Kwaa kufanya hiyo tutaweza kutambua kwa kina ule uovu uliopo katikati ya vita na ukweli kwamba sisi hututachukuliwa kama wajinga kwa sababu tumechagua amani na ambayo haitatukasirisha”.

Katika suala hilo Askofu Jurkovič amesema ni muhimu kwamba nchi zilizotia saini zisikilize sauti za wahanga, kuwajumuisha katika utekelezaji wa Mkataba kwa roho ya kweli ya udugu na uwajibikaji, ili kuhakikisha kuwa mahitaji yao yanashughulikiwa vya kutosha na kwamba haki zao zinalindwa. Uingiliaji wa wa mwakilihsi huyo ulihitimishwa kwa matumaini kwamba mataifa yaliyosaini kwenye Mkataba yatachukua majukumu yao ya kuzuia vikundi vya kutengeza silaha za maangamizi kakubwa  kutoka kuwa tishio kwa maisha na kikwazo kwa maendeleo fungamani ya watu ambao wamepata na wanaendelea kupata migogoro”.

28 November 2020, 13:06