Tafuta

2020.11.12 Mkutano na  waandishi mjini Vatican 2020.11.12 Mkutano na waandishi mjini Vatican 

Upendo wa Papa unaendelea kwa ajili ya maskini ulimwenguni!

Askofu Mkuu Rino Fisichella amewawasilisha katika Ofisi ya Wanahabari Vatican mipango ya Siku ya IV ya Maskini Ulimwenguni itakayofanyika Jumapili tarehe 15 Novemba na Misa iltakayoongozwa na Papa katika Kanisa kuu la Mtakatifu Petro,Vatican mbele ya watu mia moja.Mtandao wa mshikamano umeanzishwa kwa ajili ya kutoa chakula,barakoa na msaada kwa maelfu ya familia.

Na Sr Angela Rwezaula – Vatican

Wape maskini kwa ukarimu (Sir 7,32), ni mada inayoongoza ujumbe wa Papa Francisko wa Siku ya Maskini duniani 2020, itakayo adhimishwa Jumapili tarehe 15 Novemba. Ni siku maalum ambayo katika majimbo yote ulimwenguni inaangaza na kuhamasisha kubaki yaweze hai kwa maana ya udugu mbele ya watu wenye kuhitaji zaidi. Misa ya Papa Francisko katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro  itaanza saa nne asubuhi, ambayo itawakilishwa na watu mia moja tu, maskini wa ulimwengu pamoja na watu wa kujitolea na wafadhili. Baadhi yao watasoma masomo ya liturujia ya siku. Maadhimisho ya Ekaristi yatatangazwa moja kwa moja na Televisheni ya Baraza la Maaskofu Italia TV2000, RAI, Telepace na nyingine pamoja na majukwaa na  tovuti ya Vatican News.

Katika ujumbe wa Siku ya IV ya Maskini Ulimwenguni uliotolewa tangu Juni mwaka huu umetengwa katika vifungu 10 ambavyo vinafafanua jinsi ya kuwa karibu na maskini ambao Mungu anajitambulisha kupitia sura yao. Ujumbe unakumbusha kipindi cha janga, wahudumu wa afya wakiwa mstari wa mbele kuwa mashuhuda. Kuna maonyo kwa wale wasiojali, wenye kutengeza silaha, wafisadi. Aidha ujumbe uelezea kuwa  mgogoro wa kiuchumi, kifedha na kisiasa hautaisha ikiwa hakuna utambuzi wa uwajibikaji kwa ajili ya  wengine na kila mtu, na kwa maana hiyo mtu  na hadhi yake ndiyo ndivyo vinapaswa kuwekwa katikati ya mambo yote. Tarehe 12 Novemba, umefanyika mkutano kwa waandishi wa habari Vatican kwa njia ya mtandao ili kuwakilisha juu ya mipango iliyanzishwa kwa ajili ya harakati za Siku IV ya Maskini Duniani.

Katika uwakilishi wa siku hiyo Askofu Mkuu  Rino Fisichella Rais wa Baraza la Kipapa la kuhamasisha unjilishaji mpya amesema ambaye ameelezea juu ya shughuli mbambali ambazo zimetendwa kwa miaka hii na Kanisa na zaidi katika kipindi hiki kigumu. Mtandao wa mshikamano umeanzishwa kwa ajili ya kutoa chakula, barakoa  na msaada kwa maelfu ya familia. Kwa mujibu wa Askofu Mkuu anasema katika Siku ya Maskini duniani, hata kama kuna vizingiti vingi vya kuanza shughuli kwa ajili ya maskini kutokana na hali janga duniani, lakini bado inabaki kuonesha kuwa majimbo mengi duniani  yamekuwa  yakiendelea kuwa na msimamo hai kwa namna ya umakini wa kidugu mbele ya watu ambao wanahitaji zaidi na maskini.

Shughuli za upendo zilizoandaliwa mwaka huu, ili kusaidia maparokia na hali halisi za kikanisa zimeweza kufikiriwa kama chombo hai kwa sababu Siku ya Maskini duniani haina kikomo kwa mwanga wa mipango ya upendo na ni  sehemu zote, iliziweze kusadiwa pia kwa njia ya sala binafsi na ile ya kijumuia. Sala ambazo zimesindikizwe daima na ushuhuda thabiti. Kama ilivyo kila mwaka, maelekezo kamili yametolewa katika  toleo kitaliano lililochapishwa na Paulinus, kwa kutafsiriwa  kwa ligah tano (Kingereza, Kispanyola, kifaransa , kireno na kipoland (na uhusiano wa toleo hilo unapatikana moja kwa moja katika Tovuti ya Baraza la Kipapa la Uhamasishaji wa Uinjilishaji mpya (pcpne.va).

Maneno ya Baba Mtakatifu Francisko katika Ujumbe wake ,Askofu Mkuu akiendelea  amesema yanaonesha wazi kusudi la mipango hii. Papa anaandika: “Katika matendo yako yote, kumbuka hatima yako (Sir 7:36) ... Sehemu  hiyo ina tafsiri mbili. Ya kwanza inaonyesha kwamba tunahitaji kukumbuka kila wakati mwisho wa uwepo wetu. Kukumbuka hatima ya kawaida kunaweza kusaidia kuishi maisha ya kujitoa kwa wale walio maskini  zaidi na ambao hawajapata fursa sawa na sisi. Pia kuna tafsiri ya pili…Ni lengo la maisha yetu ambalo linahitaji mradi ufanyike na safari ikamilike bila kuchoka. Kiukweli, kusudi la kila tendo letu haliwezi kuwa lingine isipokuwa ni upendo ... Upendo huu ni kushiriki, kujitoa na huduma, lakini pia huanza na kugundua kuwa tunapendwa kwanza na kuamshwa hisia za kupenda. Mwisho huu unaonekana wakati mtoto anakutana na tabasamu ya mama na anahisi kupendwa kwa dhati wa uwepo wake . Hata tabasamu ambalo tunashirikishana na maskini ni chanzo cha upendo na linatuwezesha kuishi kwa furaha. Kuwapatia mkono wa kwa ukarimu, basi, unaweza daima kutajirisha na tabasamu la wale ambao hawakubali uwepo wao na msaada unaotolewa, lakini wanafurahi tu kuishi mtindo wa wafusi wa Kristo (n. 10). Ni kwa roho hii ndio tunajiandaa kuishi Siku hii ya IV ya Maskini.

12 November 2020, 16:17