Tafuta

Kila mwaka wanazaliwa  watoto njiti milioni 15. Kila mwaka wanazaliwa watoto njiti milioni 15. 

Siku ya mtoto njiti duniani-Ask.Mkuu Paglia viumbe dhaifu vinapambana

Katika fursa ya Siku ya mtoto njiti (premature day)duniani ambayo huadhimishwa tarehe 17 Novembaya kila mwaka,Askofu Mkuu Vincenzo Paglia Rais wa Taasisi ya kipapa ya Elimu ya Maisha amemwandikia barua Rais wa Chama cha Italia cha Utoto akiwaombea watoto wanaozaliwa njiti katika hali hii ngumu na nyeti kwenye muktadha wa janga.Anawapongeza madaktari bingwa wa watoto na wauguzi katika mawadi ya watoto na wazazi.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Askofu Mkuu Vincenzo Paglia, Rais wa Taasisi ya kipapa ya Elimu ya Maisha amemwandikia barua Profesa Fabio Mosca, Rais wa Chama cha Italia cha Utoto, katika fursa ya Siku ya Mtoto njiti(premature day)duniani ambayo huadhimishwa tarehe 17 Novemba kila mwaka ulimwenguni kote. Awali ya yote ameanza na wazo sala kwa ajili ya watoto wote waliozaliwa kabla ya  kufikisha mwisho wao yaani watoto njiti, na kwa ajili ya familia ambazo zinajikuta na kukabiliana na hali halisi ya sasa ambayo ni nyeti. Askofu Mkuu kwa wao amesema ni kutaka kuwapa umakini na utunzaji katika Siku hii ambayo imewekwa kwa ajili yao. Askofu Mkuu Paglia amesema kila mwaka ni watoto njiti milioni 15 wanaozaliwa  kwa maana ya kwamba ni mtoto mmoja kati ya kumi anayezaliwa akiwa njiti. Ni viumbe vidogo ambavyo kweli ni vidhaifu sana lakini vikipambana kwa kusindikizwa na changamoto hii ya kuishi na wazazi wao, madaktari wao wa watoto na wauguzi wa wadi za wazazi.

Askofu Mkuu Paglia anasali kwa Bwana kwa ajili ya mama na baba wa watoto hao ambao wanakabiliana na majaribu hayo ya njiti,  hata wadaktari wa watoto na wauguzi ambao wanafanya kazi katika vyumba vya mahututi na ambao kwa ujuzi wao,  kwa kujitoa kwao na utunzaji wao wa upendo wanawahaudumia kila siku watoto hawa wadhaifu zaidi, kuwasaidia washinde matatizo yanayotokana na kuzaliwa kabla ya wakati, hata wanapobainisha kuwa na matatizo mengine ya asili ambayo yanawaweka katika hatari  zaidi ya maisha yao wenyewe.

Katika wakati huu wa kihistoria, Askofu Mkuu Paglia ameongeza, daima wanazaliwa watoto wachache, lakini mabingwa wa watoto na wauguzi wamekuwa wa dhati na wahudumu wa Mungu ili kuwasaidia wazazi na familia zao  katika mpango mkubwa wa maisha. Hata Papa Francisko, anawatia moyo madaktari  wote na wahudumu wote wa afya wanaoendelea katika jitihada hizi muhimu za kutunza na kujikita katika utume wao ambao ni kielelezo cha uaminifu na huduma ya dhati katika maisha yanayozaliwa hasa zaidi walio wanyonge na wadhaifu. Hatimaye Askofu Mkuu Paglia anahitimisha kwa kuwatakia baraka ya Bwana na ulinzi wa mama wa Mungu, Maria Mtakatifu huku akiwaombea wazazi na watoto hao mashujaa kwa ajili ya maisha

17 November 2020, 16:31