Mti wa sherehe za Noeli umefika Uwanja wa Mt.Petro

Maandalizi ya kupamba kwa ajili ya sherehe za siku kuu ya Noeli umeanza katika Uwanja wa Mtakatifu Petro.Asubuhi wamewekwa Mtu mrefu mwakundu kutoka nchini Solvenia ambao utaambatanishwa na Pango lenye sanamu na udongo wa mfinyanzi wa Italia.Uzinduzi mapambo hayo ni tarehe 11 Desemba

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Jumatatu asubuhi tarehe 30 Novemba kazi za wanaume pamoja na vifaa vya kiufundi, ili kuusimamisha Mti mrefu sana katika uwanja wa Mtakatifu Petro umefanyika, pamoja na maandalizi ya kupamba pango la siku kuu ya kuzaliwa kwa Bwana. Uzinduzi wa mapambo hayo yote ulitangazwa mwezi mmoja uliopita kwamba ni  tarehe 11 Desemba saa 10.30 jioni, licha vizuizi vilivyowekwa na janga, lakini afla hiyo itakuwa na watu wachache  na kuongozwa na Mwenyekiti na Katibu Mkuu wa Serikali ya mji wa Vatican. Mti huo na pango vitabaki kwa kutembelewa hadi tarehe 10 Januari 2021 katika Siku kuu ya Ubatizo wa Bwana.

Katika uwanja wa Mtakatifu Petro kwa maana hiyo vitaweka vipande vichache tu vya mkusanyiko dhaifu wa sanamu 54. Zitawekwa pembeni kwenye jukwaa lenye taa la karibu mita za mraba 125 ambazo zinazunguka sehemu ya obelisk kwenye mteremko kidogo. Sanamu zinawakilisha Mamajusi; katikati, kwenye sehemu ya juu kabisa ya jukwaa, ni kikundi cha Malaika wakati wa kuzaliwa kwa Yesu na kitakachowekwa juu ya Familia Takatifu kuashiria ulinzi wake juu ya Mwokozi, Maria na Yosefu. Katika Uwanja wa Mtakatifu Petro kutaweka Mti mrefu mzuri wenye  urefu wa mita 28 na kipenyo cha sentimita 70, ambao ni kutoka kusini-mashariki mwa nchi ya Slovenia, hasa kutoka manispaa ya Kočevje, kwenye mto Rinža. Eneo la Kočevsko ni moja ya maeneo ya Kislovenia ambayo ni yenye asili ya kupendeza zaidi misitu misitu hufunika asilimia 90% ya eneo lake.

Miti hiyo aina ya (Spruce) ilienea sana huko Slovenia katika nusu ya pili ya karne ya 18, ambayo inawakilisha zaidi ya ya rasilimali 30% za msitu na ndio aina  muhimu zaidi ya miti kutegemea  mantiki ya  kiuchumi nchini humo. Tangu nyakati za zamani imekuwa ishara ya kizazi na katika tamaduni maarufu mara nyingi hutumiwa kwenye hafla ya sherehe kama sikukuu ya  mwezi Mei  Mosi au sherehe za Kuzaliwa kwa Bwana.  Katika mkoa wa Bela Krajina, kwa sikukuu ya Mtakatifu George ilikuwa ya kiutamaduni kubeba mti wa aina hiyo (spruce) katika maandamano, iliyosafishwa na kupambwa na maua na vitambaa. Spruce ndefu zaidi ya Ulaya  inaitwa ‘Sgermova smreka’ ambayo ina urefu wa mita 61.80 na iko kwenye milima ya Pohorje huko Slovenia. Ina umri wa miaka 300, na mzunguko wa mita 3 na sentimita 54 na kipenyo cha zaidi ya mita moja.

30 November 2020, 17:44