Tafuta

Vatican News
Uteuzi wa makardinali wapya 13 Uteuzi wa makardinali wapya 13 

Wasifu wa makardinali wapya kutoka kona za ulimwengu!

Wasifu wa makardinali wapya hao ni kutoka kona za ulimwengu,Africa,Asia(Brunei na Ufilippine),Amerika ya Kasikazini na Kusini,lakini pia Ulaya nchini Italia.Na umakini zaidi kwa namna ya pekee ni watoto wa Mtakatifu Francisko wa Assisi katika mwaka wa Waraka wake wa Fratelli tutti.

Na Sr. Angela Rwezaula-Vatican.

Wafuatao ni wasifu wa makardinali wateule: Kardinali Mteule Mario Grech Katibu Mkuu wa Sinodi ya Maaskofu, alizaliwa huko Qala (Malta), jimbo la Gozo, tarehe 20 Februari  1957. Majiundo yake msingi na sekondari huko Victoria, Gozo; ikiwa ni pamoja na falsafa na taalimungu katika seminari ya Gozo. Baadaye aliendelea na Masomo ya juu  katika Chuo kikuu  cha kipapa la Laterano na pia  kwa kujipatia udaktari wa Sheria za Kanisa katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Antony Aquine (Angelicum). Tarehe 26 Novemba 211 Papa Mstaafu Benedikto XVI akamteua kuwa Askofu wa Gozo, hadi tarehe  2 Oktoba  2019 alipotangazwa na Papa kuwa Katibu Mkuu mwandamizi wa Sinodi ya Maaskofu. Tarehe 5 Septemba 2020 akateuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Sinodi ya Maaskofu.

Kardinali Mteule Marcello Semeraro Rais wa Baraza la Kipapa la mchakato wa kuwatangaza Watakatifu, alizaliwa huko Monteroni ya Lecce Italia, tarehe 22 Desemba 1947.  Akapata daraja la Upadre tarehe 8 Septemba 1971. Majiundo yake ya kikuhani ni kuanzia Seminari ya Kipapa ya Kikanda  ya Pio XI huko Molfetta, Puglia. Na baadaye aliendelea na mafunzo katika kitivo cha taalimungu cha Chuo Kikuu cha Kipapa Laterano, Roma mahali alipopata shahada ya udaktari wa Taalimungu Takatifu. Aliendelea na kufundisha taalimungu katika Taasisi ya kanda ya Puglia,  hata masomo ya Kikanisa katika Kitivo cha taalingumu cha P.U.L. Alichaguliwa kuwa Askofu tarehe 25 Julai 1998  na kuamishwa katika Kanisa la Jimbo la Albano kunako tarehe 1 Oktoba  2004 hadi tarehe 15 Oktoba 2020 alipoteuliwa na Papa Francisko kuwa Rais wa Baraza la Kipapa la Mchakato wa kuwatangaza watakatifu.

Askofu Mkuu  Antoine Kambanda wa jimbo kuu katoliki Kigali (Ruanda,alizaliwa tarehe 10 Novemba1958 jimbo kuu  Kigali. Kwa bahati mbaya ndugu zake  wa familia waliuwawa wakati mauaji ya kimbari 1994 na akabaki na kaka yake ambaye kwa sasa anaishi Italia. Masomo yake ya msingi alisomea Burundi na Uganda, na kuhitimisha baadaye sekondari nchini Kenya. Alirudi nchini Rwanda akiwa amehitimisha masomo ya Falsafa na Taalimungu Mungu kwa miaka miwili. Alipata daraja la upadre kunako tarehe 8 Desemba 1990 mikononi mwa Mtakatifu Yohane Pauli II wakati wa ziara yake ya kichungaji nchini Rwanda. Baada ya daraja alishughulika na masuala ya seminario kama Gombera na kufundisha masomo katika seminari ya ndogo ya Ndera Kigali.  Alendelea na Mafunzo ya juu katika Taasisi ya Alfonsiana, Roma, na kupata shahada ya udaktari wa Taalimungu maadili. Aliporudi Rwanda akawa Mkurugenzi wa Caritas Jimbo kuu  Kigali na Tume ya Jimbo kwa ajili ya Haki na amani. Profesa wa Taalimungu maadili katika seminari kuu ya taalimungu Nyakibanda. Kunako tarehe 7 Mei 2013 aliteuliwa kuwa Askofu wa Jimbo la Kibungo hadi tarehe 19 Novemba 2018 ambapo Papa  Francisko alimetua kuwa Askofu Mkuu wa jimbo Kuu Kigali.

Kardinali Mteule, Askofu Mkuu Wilton D. Gregory wa Washington. Alizaliwa tarehe 7 Desemba 1947 huko Chicago (Illinois) Marekani.  Baada ya shule ya msingi na huko Chicago, alijiunga na Seminari ya maandalizi ya Quigley.  Masomo ya kifalsafa huko taasisi ya Niles na baadaye taalimungu katika Seminari ya Mtakatifu Maria huko Mundelein (Illinois) Marekani. Aliendelea  na masomo ya juu na kupata shahada ya  Udaktari wa Liturujia Katika Taasisi ya Mtakatifu Anselmi Roma(1980). Alipata daraja la Upadre tarehe 9 Mei 1973 jimbo kuu katoliki la Chicago. Baada ya upadrisho akashika nyadhifa mbali mbali za jimbo. Na baadaye akarudi tena kuwa mwanafunzi  Roma (1976-1979). Aliteuliwa kuwa Askofu Mkuu msaidizi wa  Atlanta (Georgia) kunako tarehe 4 Desemba 2004. Amewahi kuwa Rais wa Baraza la Maaskofu Marekani (2001-2004). Tarehe 4 Aprili 2019 aliteuliwa na Papa Francisko kuwa Askofu Mkuu wa Washington.

Kardinali Mteule, Askofu Mkuu  Jose F. Advincula wa Capiz (Ufilippine). Alizaliwa huko Dumalag, Jimbo Kuu katoliki la  Capiz, tarehe  30 Machi  1952. Baada ya masomo yake ya  msingi huko Dumalag, aliendelea na seminari ya Mtakatifu Pius X  mji wa Roxas mahali ambapo aliendelea hata na masomo ya kifalsafa, na baadaye  Taalimungu katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Tomas huko Manila. Alipata daraja la upadre jimbo Kuu la Capiz tarehe 14 Aprili  1976.  Baada ya daraja alishika nafasi mbali   za Kanisa lakini baadaye akaendelea na Mafunzo tena  katika Chuo Kiuu cha Mtakatifu Tomas Angelicum, Roma kwa kupata Uzamifu wa Sheria za Kanisa. Amekuwa mhamasishaji wa Haki na amani katika Mahakama ya Jimbo Kuu la  Capiz.  Aliteuliwa kuwa Askofu kunako tarehe 15 Julai 2001 kuwa Askofu wa Mtakatifu Carlos, na kusimikwa tarehe 8 Septemba mwaka huo. Tarehe 9 Novemba 2011 aichaguliwa  kuwa Askofu Mkuu wa Capiz, katika kisiwa cha  Panay, Ufilippine ya Kati .

Kardinali mteule, Askofu mkuu Celestino Aós Braco, o.f.m. kap wa  Santiago ya Chile. Alizaliwa Artaiz, Jimbo Kuu la Pamplona (Uhipagna), tarehe  6 Aprili 1945. Majiundo yake ya kifalsafa huko Zaragoza na taalimungu  Pamplona. Amepata uzamili wa masomo ya saikolijia chuo Kikuu cha Barcellona (Uhispagna). Alifunga nadhiri za muda katika Shirika la Ndugu wadogo wakapuchini, tarehe 15 Agosti 1964 huko Sangüesa na za milele tarehe 16 Septemba 1967 huko Pamplona. Alipata daraja la Upadre huko Pamplona tarehe  30 Machi 1968. Alichaguliwa kuwa Askofu wa Copiapó, tarehe  25 Julai 2014, na kuwekwa wakfu tarehe  18 Oktoba mwaka huo huo. Tarehe 23 Machi  2019 aliteuliwa kuwa Msimamizi wa Kitume katika jimbo  kuu lisilo na Askofu la  Santiago ya Chile. Tarehe 27 Desemba  2019  Papa Francisko amteua kuwa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la  Santiago ya  Chile.

Kardinali mteule, Askofu  Cornelius Sim wa Puzia ya  Numidia na Msimamizi wa Kitume wa Brunei. Alizaliwa huko Seria (Brunei) tarehe 16 Septemba 1951. Majiundo ni kuwa na shahada ya uhandisi kutoka Chuo Kikuu cha Dundee, Scotland, Uingereza. Ana Shahada ya Uzamili katika Taalimungu kutoka Chuo Kikuu cha kifranciskani cha Steubenville, Ohio, Marekani. Alipata daraja la Upadre tarehe  26 Novemba  1989. Baada ya kufanya shughuli za uchungaji wa parokia, alitangazwa kunako mwaka 1995 kuwa Msimamizi mkuu wa Brunei na tarehe  21 Novemba  1997 akateuliwa  Kuwa balozi. Mnamo tarehe 20 Oktoba 2004, Mtakatifu Yohane Paulo II aliinua Jimbo la Kitume la Brunei na kumteua kuwa Msimamizi wa kwanza wa Kitume,na kuwa na makao ya uaskofu wa Puzia ya Numidia.

26 October 2020, 15:33