Waamini Katoliki nchini China wakiwa katika sala Waamini Katoliki nchini China wakiwa katika sala 

Upaisho wa Mktaba kwa miaka miwili tena kati ya Vatican na China

Taarifa zimetolewa kuhusu mkataba huo tarehe 22 Oktoba siku ambayo ulikuwa unaisha muda wake.Sababu za makubaliano zimetangazwa katika makala ya Osservatore Romano kwamba umekuwap na mwanzo mzuri na hiyo ni shukrani kwa mawasiliano mazuri na ushirikiano kati ya pande zote mbili.

VATICAN NEWS

Mkataba wa  muda kati ya Vatican  na Jamhuri ya Watu wa China juu ya uteuzi wa maaskofu umeongezwa  muda wake kwa miaka mingine miwili. Hii imetangazwa katika taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Wanahabari Vatican iliyochapishwa siku ambayo mkataba huo wa muda ulikuwa unaisha, tarehe 22 Oktoba 2020. Katika taarifa hiyo inabainisha kuwa Vatican ikizingatia kuwa uzinduzi wa utekelezwaji wa Mkataba uliotajwa hapo juu wa dhamana ya kimsingi ya kikanisa na ya kichungaji kuwa mzuri, na kwa sababu ya mawasiliano mazuri na ushirikiano kati ya sehemu zote mbili katika jambo lililokubaliwa, inakusudia kuendelea na mazungumzo ya wazi na yenye kujenga na  kukuza maisha ya Kanisa Katoliki na wema wa watu wa China”.

Taarifa hiyo imesindikizwa na makala ndefu iliyoandaliwa na Gazeti la Osservatore Romano, ambalo linaeleza bayana sababu za uchaguzi huo. Sehemu zote mbili  kwa mujibu wa makala,  zimetathmini mantiki mbalimbali ya  maombi yake, na wamekubaliana, kupitia  kubadilishana rasmi maandiko, kuongeza muda wa uhalali wake kwa miaka mingine miwili, hadi tarehe 22 Oktoba 2022”.

Lengo msingi la makubaliano ni lile la kusaidia na kuhamasisha utangazaji wa Injili nchini China kwa kujenga kikamilifu na uwazi wa umoja wa Kanisa. Kuhusu masuala ya uteuzi wa maaskofu na umoja wa maaskofu na Mfuasi wa Mtakatifu Petro ni muhimu sana kwa ajili ya maisha ya Kanisa, iwe kwa ngazi mahalia na kwa ngazi ya ulimwengu”. Hasa kipengere hiki, kilichochea mazungumzo na kilikuwa kumbukumbu katika uandishi wa maandishi ya Mkataba, ili kuhakikisha kidogo umoja wa imani na muungano kati ya maaskofu na huduma kamili kwa jamuiya Katoliki nchini China .Tayari leo hii, kwa mara ya kwanza katika miongo mingi, maaskofu wote nchini China wako kwenye muungano na Askofu wa Roma na shukrani kwa utekelezaji wa Mkataba huo, hakutakuwepo tena  na mipango isiyo halali kuweka wakfu.

Katika makala pia wanaeleza kwamba katika mkataba hawakubaliana na masuala yote yaliyofunguliwa au hali ambazo zinachochea bado wasiwasi kwa ajili ya Kanisa, bali mada tu wa uteuzi wa maaskofu. Wakinukuu hotuba ya hivi karibuni ya Katibu wa Vatican, Kardinali Pietro Parolin katika mkutano wa PIME huko Milan, Italia, makala hiyo inakumbusha kwamba kuhusiana na mada hii yameibuka masuala ya kutoelewana.  Mengi ya haya yalitokana na Mkataba, ambapo katika maoni hapakuwapo uunganisho sahihi kuhusu masuala ya kisiasa ambayo kiukweli hayana uhusiano wowote na Mkataba wenyewe.

Saini iliyotiwa huko Beijing kunako Septemba 2018 ni hatua ya kuwasili kutoka safari ndefu lakini juu ya yote ni mwanzo wa makubaliano mapana na ya kuona mbali. Makubaliano ya muda, ambayo maandishi yanabainisha  hali halisi  yake ya majaribio, yalibaki kwa namna moja yamehifadhiwa  na ambayo sasa  ni matokeo ya mazungumzo ya wazi na ya kujenga.

Mtazamo huo wa mazungumzo, uliomwilishwa na heshima na urafiki, unatamaniwa sana na kuhamasishwa  na Baba Mtakatifu Francisko, ambaye anafahamu vizuri vidonda vilivyoukabili muungano wa Kanisa hapo zamani, na baada ya mazungumzo ya muda mrefu, yaliyoanzishwa na kufanywa na watangulizi  wake na katika mwendelezo usio na mashaka wa mawazo nao, alianzisha tena ushirikiano kamili na maaskofu wa China waliowekwa  wakfu bila kuwa na mamlaka ya kipapa na kuidhinisha kutiwa saini kwa Mkataba juu ya uteuzi wa maaskofu, ambao rasimu yao ilikuwa tayari imeidhinishwa na Papa mstaafu  Benedikto XVI.

Katika makala hiyo aidha wanabainisha kwamba baadhi sekta zingine za kisiasa za kimataifa zilijaribu kuchambua kazi ya Vatican hasa kulingana na mazingira yao ya kijiografia. Lakini kwa upande wa masharti ya Mkataba wa Muda, hata hivyo, kwa upande wa Vatican ni suala la kidini. Kwa kuongezea, kuna ufahamu kamili kwamba mazungumzo haya yanakuza utafutaji wa matunda zaidi kwa faida ya wote na kwa wema wa Jumuiya nzima ya kimataifa.

22 October 2020, 15:20