Tafuta

2020.09.03 PATRIAKI Bartlholomew 2020.09.03 PATRIAKI Bartlholomew 

Patriaki Bartholomew kuhusu “Fratelli tutti”:tuache kutokujali na roho ngumu!

Vatican News imefanya mahojiano na Patriaki wa Kiekumene kuhusiana na Waraka wa Papa Francisko wa “Fratelli Tutti” ambapo amesisitiza kuwa tuote ndoto ya kuwa na ulimwengu wetu kama familia ya binadamu iliyoungana.Wakristo wa Kanisa wanaozaliwa kwa upya kati yao wanaitana Ndugu.Huo ndiyo udugu wa kiroho na Kristo katikati ni kiini cha ndugu asili.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Tunaunga mkono mwaliko wa Papa Francisko wa changamoto ya kutojali na ugumu wa moyo  ambao unatawala maisha yetu ya kiekolojia, kisiasa, kiuchumi na kijamii kwa ujumla, kama mambo msingi juu yake ili  uweza kuota ndoto ya ulimwengu wetu kama familia ya binadamu iliyoungana. Ndiyo maneno ya Patriaki wa Kiekumene  Bartholomew ambaye yupo jijini Roma akitoa maoni yake kuhusu Waraka wa hivi karibuni wa Papa Francisko wa  “Fratelli tutti”  yaani "Wote ni ndugu" katika mahojiano na Dk. Andrea Tornielli, Mhariri Mkuu wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano. Akijibu swali kuhusu mtazamo wake juu ya Waraka wa 'Fratelli tutti', amesema kabla ya kufahamu huo Waraka wa Fratelli Tutti wa kaka yake Papa Francisko walikuwa tayari na uhakika kuwa ungekuwa inaelezea mfano mwingine wa jitihada zake muhimu kwa ajili ya ubinadamu. Mpendwa wa Mungu kwa njia ya maonesho yake ya mshikamano kwa ajili ya wote, wanaoelemewa, wanaozidiwa, na wenye kuhitaji na ambao angeweza kupendekeza mambo ya dhati kwa ajili ya kukabiliana na changamoto kubwa za wakati huu  hasa kwa kuongozwa na kisima kisicho kauka cha utamaduni wa kikristo,na ambacho kinabubujika ndani ya moyo wake uliojaa upendo.

Patriaki Bartholomew amesema matarajio yao yamekuwa chanya baada ya kukamilisha tathmini muhimu sana ya Waraka huo ambao haimaanishi tu muhtasari au muhtasari wa nyaraka zilizopita au maandiko mengine ya Baba Mtakatifu Francisko, lakini kuhitimisha na kufurahisha kwa kutoa mafundisho yote ya kijamii. Katika roho hiyo, Patriaki ameonesha matashi mema na matumaini kuwa waraka wa 'Fratelli tutti' uweze kuwa kisima cha kuchota upendo wa kidungu na mazungumzo yenye tija kwa kuchukua wajibu na msimamo wa kweli katika mipango yote ya kijamii, kidini, kisiasa pamoja na kibinadamu.

Katika sura ya kwanza inazungumzia kivuli kilichopo ulimwenguni na kwa maana hiyo ni matumaini gani ambayo yanaweza kuonekana katika ulimwengu yatokanayo na Injili ? Patriaki amesema katika maana yake ya kibinadamu, kijamii na kiroho, Papa Fransko anabainisha na kutaja vivuli katika ulimwengu huu na hivyo hii ina maana kuzungumzia juu ya dhambi za kisasa na ikiwa tulizoea kusisitiza juu ya dhambi ya asili kwa sababu haikutokea katika nyakati zetu na wala katika karne yetu leo hii lakini hatuwezi kuwazia wakati uliopita. Licha ya hayo yote tuna wasiwasi mkubwa kwa sababu ya maendeleo ya kisasa ya  kiufundi na kisayansi ambayo yameongezea nguvu kwa binadamu. Mafanikio ya sayansi lakini hayajibu zile tafiti zetu msingi za uwepo, na wala haziondoi. Tunapata maarifa ya kisayansi kwamba hayaingii katika kina cha roho ya mwanadamu. Mtu huyo anajua hili, lakini anafanya kana kwamba hajui, amesisitiza Patriaki.

Papa anazungumzia pia pengo kubwa lililopo kwa walio navyo na wasio na kitu, ambapo Patriaki amesema maendeleo ya kiuchumi hayakupunguza utofauti wa matajiri na maskini. Na zaidi umeongezea kuwa na kipaumbele cha faida dhidi ya ulinzi wa walio wadhaifu na kuchangia matatizo makubwa ya mazingira. Sera za kisiasa zimegeuka kuwa hifadhi ya uchumi. Haki za binadamu na sheria za kimataifa zimefafanuliwa na kutimiza madhumuni yasiyohusiana na haki, uhuru na amani. Shida ya wakimbizi, ugaidi, ghasia za serikali, kudhalilisha hadhi ya binadamu, aina za kisasa za utumwa na janga la Covid-19 sasa zinaweka siasa mbele ya majukumu mapya na kufuta mantiki yake ya ubadhirifu.

Kwa kujibu muktadha huo Patriaki anasema mapendekezo ya maisha ya Kanisa ni kufanya mabadiliko hasa ya kuwa wamoja na ndiyo ulazima, ndiyo upendo, ndiyo ufunguzi wazi kwa mwingine na kuwa na utamadunu wa mshikamano na watu.  Kabla ya mungu wa kiburi,  mtu kiburi tunahubiri, Mungu-mtu, amesisitiza Patriaki. Tunakabiliwa na uchumi, tunatoa nafasi ya uchumi wa ikolojia na shughuli za kiuchumi kulingana na haki ya kijamii. Katika sera ya haki ya wenye nguvu zaidi, tunapinga kanuni ya kuheshimu haki zisizoweza kutolewa kwa  raia na sheria za kimataifa. Mbele ya kukabiliwa na shida ya kiekolojia, tunaitwa kuheshimu kazi ya  uumbaji, unyenyekevu na ufahamu wa jukumu letu la kukabidhi mazingira ya asili kwa kizazi kijacho. Jitihada zetu za kushughulikia shida hizi ni muhimu, lakini tunajua kwamba yule anayefanya kazi kupitia sisi ni Mungu rafiki wa wanadamu.

Akifafanua kuhusu picha ya Msamaria mwema ambayo ni muhimu kwa wakati huu, Patriaki amesema mfano wa  Msamaria mwema uko karibu (Mt 25,31-46 na Lk 1025-37). Maandishi ya biblia yanatuonesha ukweli wote wa amri ya Upendo. Katika mfano huo kuna  kuhani, na  Mlawi wanawakilisha dini, ambazo zimefungwa binafsi, zinajikita kuhifadhi sheria tu na kudharau kama tabia ya kifarisayo waliokuwa wakijali sheria  tu na kusahau(Mt 23,23) upendo na msaada wa jirani. Msamaria mwema anaonesha kuwa mgeni wa karibu ambaye baada ya kumwokoa mtu aliyejeruhiwa na majambazi. Katika swali kwa mwalimu wa sheria ni nani jirani yangu (LK 10, 29), Kristo anajibu kwa swali “ ni nani kati ya hawa watatu wanafikiri alikuwa ni jirani ya yule aliyejeruhiwa? (Lk 10, 36). Katika hili mwanadamu hana ruhusa ya kuuliza bali anaombwa na kuitwa kutenda kwa dhati. Daima ni lazima ajitokeze wjirani, ndugu aliye mbele au  walio mbali,yaani  mgeni na adui. Lazima kuzingatia kuwa mfano wa Msamaria mwema , unakwenda sambamba na swali la mwalimu wa sheria ambalo linamjaribu Kristo je nifanye nini ili nipate kurithi maisha ya milele (Luka 10, 25), katika jibu lake  ni upendo kwa jirani na ambalo ni wazi katika hali hiyo. Huo ndiyo ujumbe kwa mtazamo wa hukumu.

Kwa nini ufikirie kuwa wote ni ndugu na kwa nini ni muhimu kugundua kwa upya kwa ajili ya wema wa binadamu? Wakristo  wa Kanisa wanaozaliwa kwa upya kati yao wanaitana Ndugu. Huu ndiyo udugu wa kiroho na Kristo katikati na ni kiini cha ndugu asili. Kwa wakristo kusema ndugu, haina maana ya kuwa  wajumbe wa Kanisa moja  tu bali watu wote. Neno la Mungu limechukua asili yake ya kibinadamu na kuunganishwa yote ndani mwake. Kama wote biadamu tumeumbwa na Mungu ndivyo wote tumeingizwa katika mpango wa wokovu. Upendo wa mwamini hauna mpaka na wala vizingiti. Unakumbatia uumbaji wote na unawaka katika moyo wa uumbaji  wote  (Isacco il Siro).  Upendo kwa ndugu daima haulinganishwi. Hiyo siyo hisia ya mbali au kufikikirika kwa binadamu, ambayo kwa kawaida udharau jirani. Ukuu wa muungano binafsi na wa udugu hutofautisha upendo wa Kikristo na udugu na ubinadamu wa kufikirika.

20 October 2020, 14:06